Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Mkuu hakuna haja yamaelezo mengi hivyo kataa ndoa tu save kibunda piga tembea
Unaweza kataa ndoa ila siyo kutaa familia. Kama mwanamme uliyekamilika lazima uwe na watoto ambao utazaa na mwanamke mwenye maadili mema.

Ukipuuzia mambo madogo madogo kama haya ya kuoa binti asiyetambua ndugu yeyote upande wa baba lazima baada ya miezi 3 utaanza kukataa ndoa.
 
Uliza ukoo au kabila lenu utaratibu KWA asiye na ndugu upande wa baba unakuaje. Wengine upokea waliomlea, wengine wajomba.
Kama hatambui ndugu yeyote upande wa baba hakuna kuoa.
 
Kwani hiyo mahari unatoa ili iweje????? Inafaida gani???

Unaenda tu kuchochea mgogoro wa hiyo familia kwa vitu vilivyopitwa na wakati.
Tatizo mnaendekeza usasa usiyo na maana hata kidogo. Kama hujui maana ya mahari, kaa kimya ujifunze kwa wakubwa zako
 
Kuna wanaokwepa majukumu ya malezi wanakaa mbali wanapokeaje utu uzima.Ukikaa mbali endelea kukaa mbali hivyo hivyo
Siyo kweli. Hata kama kakwepa majukumu lazima binti ajue ndugu zake upande wa baba yake. Tofauti na hapo hafai kuolewa.
 
Mkuu kupokea mahali ni jambo linaendeshwa kimila hasa kama sio muislamu, kwa baadhi ya makabila ujombani wanapokea mahali kama huyo mtoto anayeolewa hakutolewa mahali hata kama baba yake anamjua.
Bt haya mambo ni very complicated kuna dada kalelewa na kusomeshwa na baba wa kambo lakini kwenye mahali ameshirikishwa mama tu baba wa kambo na baba mzazi wapo
Issue kubwa ni kujua baba au ndugu wa baba. Siyo kila binti anastahili kutolewa mahari na kuolewa. Ukizingua hapo umeisha.
 
Kwanza mahari siyo ya baba, Bali mahari ni ya binti anayeolewa.

Kwenye mtiririko wa mahari kuna wanaostahili kupata vitu vinavyotambulika kimila lakini siyo pesa.

Kuna mkaja wa mama atasema anataka shilling ngapi,

Muolewaji atasema anataka shilling ngapi,

Kuna kitu la babu

Blangeti la bibi

Na vingine vitakuwa applicable kutokana na mila na desturi za makabila mbalimbali.

Kwa case kama hii wanaomuozesha binti ni wajomba, upande wa Baba hauna haki yoyote ile msijitie upofu.

Tena Kwa dini ya kiislamu mtoto wa nje ya ndoa ni wa mama hata kama baba upo na unawajibika Kwa mtoto.

Kwa kifupi hapo ndipo kwenye nguvu ya wajomba ndio wanachukuwa nafasi ya Baba.
Title ya uzi moderators wamebadilisha. Maana yangu ilikuwa inauliza kwamba binti ambaye hajui ndugu yeyote upande wa baba kama anapaswa kutolewa mahari.
 
Siyo lazima, kama Hujui kitu kaa kimya, tena mtoto ana haki ya kutumia ubini wa mama yake yani ujombani, usipotoshe vitu usivyovijuwa.

Unaelewa ni Kwa nini Yesu anaitwa Issa bin Mariam?
Je binti ambaye hajui ndugu yeyote upande wa baba anafaa kutolewa mahari?
 
1. Shangazi, baba mkubwa, bibi mzaa baba, baba mdogo, hao wote hawapo?!

Haya mambo ya wanawake wakishindwana na mwanaume basi wanasusa ukoo mzima wa baba mtoto huwa yanaleta changamoto za hovyo sana baade.

Kwanza unaanzaje kupata hadi kulea mtoto ambaye haujatambulishwa upande wa baba yake.

Kesho na keshokutwa hawa watoto wa baba yake na mtoto wanaweza kutana huko na mtoto wako wakafanya yao kumbe ni ndugu wa damu hii mbaya sana.
 
1. Shangazi, baba mkubwa, bibi mzaa baba, baba mdogo, hao wote hawapo?!

Haya mambo ya wanawake wakishindwana na mwanaume basi wanasusa ukoo mzima wa baba mtoto huwa yanaleta changamoto za hovyo sana baade.

Kwanza unaanzaje kupata hadi kulea mtoto ambaye haujatambulishwa upande wa baba yake.

Kesho na keshokutwa hawa watoto wa baba yake na mtoto wanaweza kutana huko na mtoto wako wakafanya yao kumbe ni ndugu wa damu hii mbaya sana.
 
Komeni kuwaandama single mothers, ni ukosefu wa nidhamu na ni kinyume na utu.

Unasema mahari ipokelewe na baba ambaye hata hamjui binti. Hapo kuna baba kweli.

Unasema binti hafahamiani hata na ndugu mmoja upande wa baba, hapo undugu uko wapi?

Halafu taratibu za mahari za kwenu ni tofauti na watu wengine. Upande wa bi harusi ndio unaoandaa taratibu zote za mahari na namna gani mahari ipokelewe, sio wewe unayepanga.
Ukitaka kuharibu ukoo then endekeza hizi tabia za ukoo wa mwanamke kupanga future ya mtoto utajua haujui. Haya mambo yana misingi yake na maudhui yake kuyapindisha ni kwenda kinyume na asili.

Kitendo kwanza cha mwanamke kuzaa na mwanaume ambaye hajatambulishwa kwao wala yeye binti kutambulishwa kwa familia ya huyo mwanaume ndipo makosa huanzia hapo bonge la kosa hilo na madhara huja siku za baadae.

Ni vema tukajifunza na kusimamia sheria za kijamii. Baba ni kiongozi mama ni msimamizi na msaidizi. Inapotokea unafanya jambo lolote kwenye haya maisha jaribu kuzingatia mfumo huu wa asili itakuwa ngumu sana kujenga koo yenye mambo ya hovyo.

Koo nyingi sana miaka hii zimekuwa na mambo ya hovyo sababu ya kudharau misingi. Na kuharibu huanza na mwanamke kiburi asiyesikia na kujiamulia maamuzi yake binafsi sababu kachagua kufanya anachojisikia.

Sasa huyu binti ataolewa bila upande wa baba yake kujua. Huko mbeleni kizazi chake kitakuja kutana na uzao wa baba yake bila kujua na kwasababu tayari mama kaanzisha msingi mbovu wa kumaliza mambo bila kuhusisha upande wa baba mtu ndio matokeo yake tunapata 'inbreeding' jambo ambalo hata wanyama hawatakiwi kufanya maana lina madhara. Haya matatizo,dosari na magonjwa ya kimwili kama presha, kisukari, matatizo ya akili, udumavu wa maumbile etc chanzo chake ni haya maamuzi ya kipuuzi.

Ila shida wanawake wasasa ni wajuaji hata kwa wasichojua. Na sisi wanaume tumeamua kuwaachia na maviburi yenu maana hamuambiliki wala kuelewa. Hapa tunazungumzia maswala ya ushoga, watoto wa kike kuzalia nyumbani, mabinti kutojua wanaume sahihi wa kuchumbiwa nao na kuanzisha nao familia, malezi mabovu, lishe mbovu, udumavu wa watoto kiafya, kushuka kwa intelligence ya watoto wa kiume, ushoga, kusambaratika kwa familia, ustawi mbovu wa jamii, haya yote yanatokana na yana asili ya nature ya mwanamke kutokuwa chini ya usimamizi wa mwanaume na kile kiburi cha kususa na kujitenga na mwanaume kuwa "nitafanya mwenyewe bwana sihitaji mwanaume kwani lazima".

Sasa kama kawaida yenu wanawake na ubishi wenu endeleeni. Mtakuja jifunza kwa gharama kubwa sana siku za mbeleni. Anayeiharibu dunia ni mwanamke kwa kuendekeza kiburi.
 
Tatizo mnaendekeza usasa usiyo na maana hata kidogo. Kama hujui maana ya mahari, kaa kimya ujifunze kwa wakubwa zako
Weka hapa hiyo maana ya mahari na faida zake kwa wanandoa
 
Kwanini mahari ni ya baba na si ya wote?
Kwa akili yako hapo umeona mali ila haujauna ujumbe wa mahali. [emoji23][emoji23][emoji23] Wanawake tamaa ndio iliwaweka mbali na MUNGU na kuwavuta kwa shetani hii tabia inachefua sana kwakweli mpo rahisi sana kuuza roho zenu kwa shetani mkisikia pesa au mali imetajwa.

Mahari si pesa wala kitu cha thamani ya pesa, mahari ni ujumbe wa shukurani, ndio maana unaweza enda familia ukawapa hata 50,000 ili tu kutoa taarifa ya shukurani kwa kuletewa binti.

Baba ndie mtoa mbegu na uzao wa watoto bila baba mayai ya mama hayana maana. Baba mbegu yake ndio inaumba mtoto ndio baraka ya uzao. Ndio maana mwanaume asipoweza tungisha ujauzito basi na ukoo unakomea hapo hapo. Hapo watoto unaojivunia hawawezekani bila mwanaume kutia mbegu yake katika mji wako.

Nenda katazame hata katika kilimo na ufugaji, wakulima huangaika na mbegu maana ndio hutoa matokeo ya kazi yake unaweza kuwa na banda zuri la mifugo ukikosea mbegu basi ufugaji wako utakuwa wa hasara sana. Unaweza kuwa na hekari nyingi ila aina ya mbegu unatia katika udongo ndio itabariki kilimo chako kikawa na faida au hasara.

Kama haujasoma vema vitabu vya MUNGU (Bible/Quran tukufu) hakuna kitu utaelewa juu ya uzito wa mahari na kwann anatakiwa kupokea baba.

Tatizo wanawake mnajilinganisha na mwanaume kwa kila kitu mnahisi maisha ni mashindano makalio yenu ila uzuri mnaiibishwa mchana kweupe na shetani anayewatuma tokea pale bustani ya Eden.

Mahari inapokelewa upande wa kiumeni. Wewe kukosea choice ya mwanaume ndio ujilaumu maana hadi unalala na mwanaume unazaa nae kwann haukujipa muda wa kuichunguza familia anayotoka. Kama yeye ana mambo ya hovyo ila familia yake ina wazee wenye hekima na busara na ndugu wenye hekima na busara umeshindwa nini kwa adabu kuwashirikisha ili washiriki, na mtoto kwann haujaenda mkabidhisha kwa maana ya kumtambulisha kwa upande wa baba yake.

Ndio maana watoto wa siku hizi hawaeleweki akili za hovyo sababu wanawake wanazaa na mwanaume huyu wanagombana, halafu anaenda tambulisha mtoto kwa mwanaume mwingine anasema huyu ndio baba yako na anataka mtoto aishi akiamini ukoo wa huyu baba bandia ndio ukoo wake, hivi hizi ni akili au tope?

Rudini kwenye mstari. Mnakera bana aaaagh
 
Huyu binti kalelewa na mama yake pekee yake. Baba yake yupo hajafa ila binti hajawahi kukutana ana kwa ana na baba yake wala katika upande wa baba yake hamjui ndugu yeyote.

Je, kwa scenario kama hiyo binti anafaa kutolewa mahari na kuolewa?

Na taratibu za mahari zipoje? Kwani navyojua mahari ni ya baba na kama baba hayupo mahari ipokelewe na yeyote upande wa baba yaani shangazi au baba mdogo au mkubwa.
Hili swali kama liko upande wa kiislam basi ni simple
 
Àache dharau...binti ana mama kabisa afu anaulizia pa kupeleka mahari....na waliofiwa na wazazi wote si mtawachukua bure sasa
Tatizo taratibu hamzijui mnaanza kutengeneza idea zenu za kipuuzi.

Unakuwa kama mtu ambaye ametokea kijijini kafika mjini hajawahi tumia choo cha ndani cha kukaa kwa kiburi anaona asiulize anaenda kujisaidia asijue namna ya kuflush kwann usiulize kabla aibu haijakuvaa. Kuuliza sio ujinga ni sehemu ya kujifunza.

Hata kama mtoto wazazi wake wote wamefariki ndugu watabakia upande wa baba yake na upande wa mama yake. Hawa ndio watapokea mahari. Kama ukoo wa baba yake walikufa wote kuanzia bibi na babu wa baba hadi wajukuu then wazazi kuna mlezi watamuachia baraka za kupokea mahari huyo ndie atashiriki kama muwakilishi wa upande wa kiume hata kama sio damu yake, ila ndie amekaimu mamlaka ya upande wa baba, ila kama wapo ndugu ndio utawashirikisha kusimamia hilo zoezi mkishirikiana nao.

Kosa linaanza na namna mahusiano yanavyoanza. Wewe unakutana na kijana sijui Pub huko, au chuo, au njiani au popote ambapo mlikutana. Kama vijana na mihemuko ya ngono mnaanza mahusiano. Kwann kabla mambo hajakolea sukari ninyi wawili kama hadi mnafikia hatua ya kupeana ujauzito tendo linalotafsiriwa ni kuunga koo mbili yaani ya wazazi wako na wazazi wake kwann haikujii akilini kuongea na huyo mwenzako akaongee na wazazi wake na wewe kuongea na wako kuwa taratibu zifuatwe at least hatua ya posa tu ifanyike ili hata mkipata mtoto isiitwe wa bahati mbaya?!

Hii itasaidia hata mkipishana ninyi wawili koo huwa hazigombani ninyi mkiachana kwa sababu zenu binafsi. Mtoto bado upande wa boyfriend wako yaani baba yake ni nduguzake na upande wa mama yake ni ndugu zake. So mahari ikitolewa inatakiwa wajulishwe kwa adabu zote tu na wanatakiwa kushiriki kwa taratibu zao maana huko ndipo mbegu ya mtoto ilipotoka.

Kufanya kinyume chake ndio matatizo yanaanzia hapa unaanza vuruga future ya mtoto. Ndio maana kuna wanawake amesoma vizuri amesomesha watoto mwenyewe ila watoto wanaanza tabia za hovyo utu uzimani na kwenda na mambo ya tofauti na maadili sababu hakuwakabidhisha upande wa baba kwasababu zake personal.
 
Wape upande wa mama,waliolea binti inatosha....
Haitoshi ni kosa. Huwa mnafanya kimazoea ila ni kosa kubwa sana. Unaanzisha laana ya ukoo kwa mtoto hapo bila kujua. Mtoto ana ancestry line ya kufuata ambayo ni ya baba yake.

Kama ulizaa na jambazi ulitegemea nini sasa unaanz akukwepa kuwajibika.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom