Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Aulizwe mama mtu ndie anajua hata mtoto alipatikanaje , wapi, saa ngapi, kitanda gani, shuka likikuwa rangi gani etc, yaani mama asijue baba ni nani kwan alipata ujauzito kwa kunywa chai hotelini.
 
Kwenye hii scenario upande wa baba hauhusiki kwenye hiyo mahari wala haihitaji mjadala.
Kama haujui desturi na mila uwe unakaa kimya. Huu ukisasa ndio unaleta mambo ya hovyo kwenye jamii. Halafu watoto wakianza haribikiwa mnaanza kusema shetani kafanya nini kumbe watoto wanakuwa haunted na ancestors blood. Watoto hawatulii akili sababu mizimu ya ukoo wa baba yao imechukia mbegu yao haijatambulishwa kwao sasa hamtakaa nayo kwa amani italeta mikosi.
 
Achana nao hao, hawajui mila, ulizia zaidi kwa wakubwa mahari sio jambo dogo la mzaha, usukumani inapotokea hivyo upande wa kiume hupokea mahari na hugawanywa kwa makaka wa dada
Kwa wanawake wanatazama swala la kupokea mahari kama swala la kupokea malipo ya kuuza mtoto. Kumbe mahari sio hivyo. Mtu ambaye hajui maana ya jambo huwa hawezi elewa taratibu zake.
 
Sijawahi kuona mtoto ambaye familia ya mwanaume wamethibisha ni wao kwa kukagua na kujiridhisha halafu itokee issue kama ya mahari wakate shiriki kwasababu kijana wao na binti upande wa pili hawapo pamoja.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah nimcheka balaa
 
Ogopa mapel binti anaelelewa na mama tu hafai kuwa mke ,hamsikii tu kwa sasa ndoa ni utapeli wa hali ya juu?
Ndio maana tunawaelekeza hapa ukiona unaenda kwenye familia ya binti unakuta mama ndie kiherehere na mwisho wa siku anataka yeye kumaliza kila kitu sepa mapema. Hiyo siyo familia ya kuoa.
 
Siyo lazima, kama Hujui kitu kaa kimya, tena mtoto ana haki ya kutumia ubini wa mama yake yani ujombani, usipotoshe vitu usivyovijuwa.

Unaelewa ni Kwa nini Yesu anaitwa Issa bin Mariam?
Ni kosa. Mtoto hapewi jina la mama yake uzao unakuwa na mushkeri na utapandikiza mbegu ya umalaya. Kama unabisha tazama jamii ambazo watoto hupewa ubini wa mama sifa yao kubwa ni nini?! Hata kama hawapewi ubini wa mama ila tu kitendo cha malezi bila baba around shida huanzia hapo.
 
Kuna maswali ya kipumbavu sana na yanakera. Hapa majority tumelelewa na single mothers. Na hata ukute mtoa mada amelelewa na single mother. Nature ya sisi waaftica inajulikana.

Mfano, huwa wanasema watoto waliozaliwa na mama wakiwa waislam bila ndoa watoto huwa mali ya mama. Mahari hupokea nani? Kwamba hujawahi kuona mahari ikipokelewa upande wa mama? Wababa wangapi wameescape majukumu na hawajulikani watoto wamelelewa umamani? Mahari hupokea nani? Baba apokee kwa kipi ama nduguze? Unataka kuescape kulipa mahari ama? Binti angekua yatima je ama analelewa na bibi tu tena umamani je? Acha ubabaifu wewe... ina maana hata mkaja wa mama wataka upeleka ubabani?
 
Fikiri kwa mapana usijifungie kwenye chungu ukahisi wewe ndio unazijua mila na desturi.

Just imagine wewe ndio babu wa binti ambaye baba yake humfahamu na wewe ndio umelea na mwanaume mwenye mtoto hajawahi kanyaga kwako wala kuhusika kwenye malezi. Ukifika muda wa binti kuolewa unahisi ndio utakuwa muda sahihi wa wao kuhusika na binti ili wapokee mahari? Hizo zitakuwa mila na desturi za aina gani unazifuata kama sio kujiaibisha?

Ili baba awe na haki na mtoto ana wajibu wa kuhakikisha upande wa mzazi mwenzie wanafamfahamu kuwa yeye ndio baba na anawajibika katika malezi vinginevyo asubiri busara za mtoto na wendawazimu wake
 
Huyo Kabila lake la Muhammad wala usipate shida kumuuliza hilo swali, labda uliza mila za Waarabu ndio mtaelewana, huyo siyo Mwafrica huyo ni mwislamu na Mwarabu.

Pole yake,kwahiyo ameukana uafrika wake kisa waarabu.
 
Issue kubwa ni kujua baba au ndugu wa baba. Siyo kila binti anastahili kutolewa mahari na kuolewa. Ukizingua hapo umeisha.
Sasa unamuhukumu Binti kwa kutomjua Baba ake kwani kosa ni lake au Wazazi wake!?

Wewe sio Muoaji pita kuleeeeee usimchezee zaidi kihisia binti wa Watu la sivyo Karma itakutenda vibaya sana.
 
Wala huelewi hata hoja unayoisimamia, unahororoja tu.

Baba ambaye hajahusika Kwa lolote na malezi ya binti hana haki ya kuhusika na shughuri za upokeaji mahari, hiyo ni nafasi ya wajomba.

Kabla hujanichosha wewe ni Kabila gani kwanza ili nikuelewe ni mtu wa aina gani.
 
Unaposema hapa majority mmelelewa na single mother unamaanisha nini?

Ulifanya wapi research hiyo lini kwa methodology sample ipi kujuwa kwamba members wa majority wamelelewa na single mother?
 
Tatizo mnaendekeza usasa usiyo na maana hata kidogo. Kama hujui maana ya mahari, kaa kimya ujifunze kwa wakubwa zako
Weka hapa hiyo maana ya mahari na faida zake kwa wanandoa
Tatizo mnaendekeza usasa usiyo na maana hata kidogo. Kama hujui maana ya mahari, kaa kimya ujifunze kwa wakubwa zako
Tatizo mnaendekeza uzamani usiyo na maana na umepitwa na wakati. Kutoa mahari ni kufanya biashara kama zilivyo biashara zingine.

Weka hapa maana ya mahari unayoijua wewe ili.
1. Tuipime inaendana na maisha ya sasa
2. Tupime inafaida gani kwa wanandoa
3. Tupime isipokuwepo kuna hasara zipi kwa wanandoa.

Usije na habari za zawadi, kwa sababu zawadi haina negotiation ( nipe hiki, hapana sina nakupa kile). Zawadi ni jambo la hiari.

Usije na habari eti binti anatoka kwao anakufuata ( haendi kifungoni) huyu binti anakwenda kutengeneza familia yake isiyokuwa na mipaka, watoto wanao uhuru wa kutembelea, kujumuika hata kusaidia ndugu wa pande zote bila masharti yoyote.
 
Kuna umri unakulimit kujuwa baadhi ya vitu, subiri ukikuwa wala hutohitaji kuambiwa na mtu utaijuwa dunia Kwa mapana yake.

Omba Mungu akupe miaka mingi ya kuishi.
 
Ndio maana tunawaelekeza hapa ukiona unaenda kwenye familia ya binti unakuta mama ndie kiherehere na mwisho wa siku anataka yeye kumaliza kila kitu sepa mapema. Hiyo siyo familia ya kuoa.
Kwl kbsa mkuu kwa sasa mambo ni mabaya mno ni kuviziana tu
 

Hizo ni tamaduni za huko unakokujua,ila kwa jamii nyingi za kiafrika kibantu mahari ni kwaajili ya wazazi,
 
Kuna vitu vingine havihitaji degree kutoa maamuzi .
Binti tangu azaliwe mpaka anakuwa mkubwa hajalelewa na baba wala ndugu wa upande wa baba hawamfahamu! Moja kwa moja mahari inaenda kwa mama au wajomba.
Halafu mbona mnawadharau sana wanawake? Mama amemlea binti yake kwa Hali na mali bila uwepo wa baba mzazi halafu suala la mahari unataka upeleke kwa upande usiowajibika kwa lolote!!!
 
Hizo ni tamaduni za huko unakokujua,ila kwa jamii nyingi za kiafrika kibantu mahari ni kwaajili ya wazazi,
Wewe sijui kama unaelewa kusoma na kama huelewi kiswahili nikiandika English utaelewa?

Kama mahari ni ya Wazazi blangeki la bibi na koti la babu ni vya nini kwenye mahari? Mkaja wa mama ni wa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…