Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Kuna umri unakulimit kujuwa baadhi ya vitu, subiri ukikuwa wala hutohitaji kuambiwa na mtu utaijuwa dunia Kwa mapana yake.

Omba Mungu akupe miaka mingi ya kuishi.
Kwa majibu haya nitakuwa sahihi kusema ya Kwamba mahari imegeuzwa ibada, kundi kubwa linaabudu mahari na halijui ni kwa sababu zipi.

Kiujumla hakuna hasara yoyote itakayopatikana kwenye ndoa endapo mahari isipotolewa

Pia hakuna faida yoyote itakayopatikana kwenye ndoa endapo mahari itatolewa.
 
Labda tu nikueleze kitu ambacho huwezi kuamini kama kipo.

Kuna jamii hapa Tanzania mpaka leo hazijui kunya kwenye choo, nilipata tabu sana nilipokwenda trip kwenye jamii hizo tena siyo porini ni vijiji viko ziwani na watu wapo smati kabisa.

Sasa jamii za aina hiyo usitegemee wawe waelewa kwenye mambo ya Ki jamii, hawaelewi lolote ni primitive society.
 
Vijana wengi waliozaliwa miaka ya 2000 wamezaliwa na roho lakini hawana nafsi, tunawaangalia tu ulimwengu ndio Mwalimu bingwa kabisa hapa duniani, utawafunza Kwa njia ngumu sana.

Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu, weka hili akilini.
 
Wajomba
 
Vijana wengi waliozaliwa miaka ya 2000 wamezaliwa na roho lakini hawana nafsi, tunawaangalia tu ulimwengu ndio Mwalimu bingwa kabisa hapa duniani, utawafunza Kwa njia ngumu sana.

Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu, weka hili akilini.
Umekosa hoja za kutetea mahari umekuja na vitisho hewa.

Jambo sahihi hujitetea lenyewe, faida zake hulitetea jambo husika.

Mahari ni biashara ambayo sasa inaonekana wazi, sababu zote zinazotolewa hazina mashiko na hazina faida kwa wanandoa.
 
Kikurya baba hata kama hamuelewan kias gan lazima aje akae hapo kama pambo apokee kisha awape aondoke kama baba kafa baba wadogo
Wakirya mama au wajomba hawawez kupokea mahali ni aibu kubwa sana
 
Kama binti amelelewa na upande wa mama yake pekee, kuna wajomba wataenda kuipokea hiyo mahari kisha watakuja kukabidhi kwa dada yao. Kumbuka mahari ni zawadi ya wazazi (balashishi), inaweza kutolewa ama isitolewe. Mbona wengine walilelewa na wajomba zao na majina ya ubini wakatumia ya wajomba na sio ya baba!
 
Tatizo siyo kupokea mahari bali ni kwanini binti hajui ndugu yake yeyote upande wa baba? Unadhani huyo binti anaweza kuwa mke mwema?
Wewe unafikiri ni kosa la nani? Umempenda binti au umeupenda ukoo wake upande wa baba?

Binti anaweza kuwa na majibu mazuri kwa nini hamjui ndugu yeyote upande wa baba hivyo aulizwe yeye humu hutapata majibu. Na ni vizuri kujua historia nyuma ya pazia kutoka kwa familia ya binti itakusaidia kufanya maamuzi..

Lakini kuwa mke mwema si wakati wote kunategemea mtu amelelewa na nani. Na malezi ya single mother hayamtengenezi mke wa hovyo, wapo mabinti ni wake bora japokuwa wamelelewa bila wazazi wote. Jambo la msingi ni kujua sababu za msingi kwa nini baba asihusishwe na unapaswa kuheshimu hilo kama unampenda huyo binti. Wapo wanaume wamekataa watoto wao wa nje wala wasihusishwe nao kwa sababu ya status zao kwenye jamii au kulinda ndoa na kitendo cha wewe kuliibua hili unaweza kuletea mtafaruku mkubwa uliokwepwa zamani.

Mambo haya hayahitaji kutumia nguvu wala maamuzi kurupushi. Ni hekima kidogo tu na kuwa muelewa wa mambo.
 
Katika uislaam mahari ni ya bint mwenyewe...na anaweza pokea mwenyewe mbele ya mashahidi...ila atakayemuozesha ni IMAM WA MSIKITI KAMA HANA NDUGU UPANDE WA BABA MWANAUME.
 
Naongezea atafute hela,huwezi ukawa na hela alafu ukataka kufatilia mpaka hela ilikoenda,kama mtoto amelelewa ujombani unachouliza hapa ni nini?
 
Je, uoni umuhimu wowote upande wa baba kushiriki katika kupokea mahari?

Unajua umuhimu wa pande zote mbili kushiriki kamuozesha binti?
 
Umeeleweka kiongozi, hao wanaopinga ni kwamba hawaoni mbali na hawajui misingi ya familia. Na asilimia kubwa ni wadada ambao wamezalishwa na kukimbiwa kwa makosa yao wenyewe na sasa wanalea binti zao bila kushirikisha upande wa baba na wakitegemea binti zao watakua na kuozeshwa. Na wanasahau ya kwamba maji ufuatao mkondo, kama binti umemlea mwenyewe naye atafanya chini juu alee watoto wake mwenyewe.

Mwanamke hata kama amezalishwa na akakimbiwa, ni jukumu lake kuhakikisha mtoto wake anamjua baba yake na ndugu zake upande wa baba. Hilo ni jukumu la mama kuwa daraja la kuunganisha ndugu za mtoto pande zote mbili.
 
Hivi muoaji mambo ya kwamba nani anapokea mahari yanakuhusu nini?

Wewe peleka mahari ,, wakupokea mahari hawez kukosekana.
Wee hujui nini maana ya kuoa. Ndo maana familia hazidumu siku hizi. Inamaana unaweza kuoa binti ambaye unajua ndugu zake wa upande wa mama pekee yake?
 
hapo inategemea na nature ya kabila husika, coz issue yenyewe ya mahali imekaa kitamaduni.
 
jitahidi tupate kabila la huyo mwanamke upande wa mama na wa baba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…