Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Huyu binti kalelewa na mama yake pekee yake. Baba yake yupo hajafa ila binti hajawahi kukutana ana kwa ana na baba yake wala katika upande wa baba yake hamjui ndugu yeyote.

Je, kwa scenario kama hiyo binti anafaa kutolewa mahari na kuolewa?

Na taratibu za mahari zipoje? Kwani navyojua mahari ni ya baba na kama baba hayupo mahari ipokelewe na yeyote upande wa baba yaani shangazi au baba mdogo au mkubwa.
Binti Mhaya?
 
Komeni kuwaandama single mothers, ni ukosefu wa nidhamu na ni kinyume na utu.

Unasema mahari ipokelewe na baba ambaye hata hamjui binti. Hapo kuna baba kweli.

Unasema binti hafahamiani hata na ndugu mmoja upande wa baba, hapo undugu uko wapi?

Halafu taratibu za mahari za kwenu ni tofauti na watu wengine. Upande wa bi harusi ndio unaoandaa taratibu zote za mahari na namna gani mahari ipokelewe, sio wewe unayepanga.
Komeni kuzaa kama fashion kabla ya ndoa.

Mahari ya binti asiyelelewa na baba hupokelewa na mjomba
 
Achana nao hao, hawajui mila, ulizia zaidi kwa wakubwa mahari sio jambo dogo la mzaha, usukumani inapotokea hivyo upande wa kiume hupokea mahari na hugawanywa kwa makaka wa dada
Sasa upande wa kiume hajulikani hata mmoja.
 
Huyu binti kalelewa na mama yake pekee yake. Baba yake yupo hajafa ila binti hajawahi kukutana ana kwa ana na baba yake wala katika upande wa baba yake hamjui ndugu yeyote.

Je, kwa scenario kama hiyo binti anafaa kutolewa mahari na kuolewa?

Na taratibu za mahari zipoje? Kwani navyojua mahari ni ya baba na kama baba hayupo mahari ipokelewe na yeyote upande wa baba yaani shangazi au baba mdogo au mkubwa.

Kama ni.ndoa.ya kiisilamu Mahari ni mali ya muolewaji.
 
Kwani waoaji wanataka kumpatia nani? Pia, waoaji watataka kumuona baba wa mtoto. Kwani huyo baba aliikataa hiyo mimba au huyo mtoto?

Kama kalelewa kwa mama na baba hakuwa na mchango wowote na kumkataa directly au indirectly, mjomba anapokea hiyo mahari, ingawaje sijui kwa makabila mengine.
Kama binti hamjui ndugu yeyote upande wa baba, je anafaa kuwa mke?
 
Kwa waislamu (tukiacha posa maana sina ujuzi nayo) mahari anapewa muolewaji. Mahari ni zawadi ya bwana kumpa bibi na wala si thamani ya binti kwamba ananunuliwa kwayo!

Utofauti wa zawadi hii na zawadi nyingine ni kuwa muoaji haamui tu yeye mwenyewe bali lazima amuulize huyo mwanamke anayetaka kumuoa kwamba angependa zawadi gani.

Kwahiyo mahari atakayotaja bibi basi bwana ataileta na itapokelewa na walii wa muolewaji (walii ni baba wa muolewaji au mwanaume yeyote wa upande wa baba wa muolewaji aliyepewa jukumu la kumuozesha binti)

Akishapokea huyo walii atampa binti mahari yake yote iliyotolewa kisha ndoa inafungwa. Maamuzi ya mahari achukue au awaachie wazazi au atumieje yanabaki kwa binti mwenyewe.

Watu sasa (hasa watu wa mila za Kitanzania) kwa kuona sheria hiyo wakaingiza mambo kibao hapo ili wapate ulaji kupitia ndoa. Mara mkaja, mara blanketi, mara makosa, mara... Yaani unakuta unataka kuoa lakini unawalipa hela wana ukoo wote wa binti! Matokeo yake kukitokea jambo kidogo mtu anakimbilia kwenye mahari anaanza kuwianisha thamani ya ndoa au mtu na mahari.
Sawa umeeleweka kuhusu utaratibu wa mahari kwa dini ya kiislam. Ila nauliza utaratibu upike kama binti hajui ndugu yeyote upande wa baba? Je anafaa kuolewa?
 
Siwezi peleka upande mmoja. Huyu binti atakuwa afai kuwa mke
Elewa kuwa km ni Islamic kuna baba aina 3, baba mlezi, baba aliyekusomesha, na baba mzazi. Hao woote hakuna kuna Baba wa hiari, Kuna wakati mtoto anaweza kuwa wa mama peke yake sbb baba yake kamkataa na Mjomba akasimama km Baba. Kama hutaki unalo lako linalokusibu.
 
Sidhani kama mleta mada kauliza kwa ubaya.

Kama mtu unafahamu taratibu, ni bora kumuelimisha kuliko kumzodoa na kumuona kwamba ni mzinguaji.

Hata kama upande wa kiume hautambuliki, lakini haiondoi ukweli kwamba mtoto lazima awe na baba mzazi. Na kuna sababu nyingi, zinazoweza kupelekea upande mmoja usiweze kutambulika.

Mzee wetu Mohamed Said njoo utupe elimu kidogo juu ya hili.
Kweli mkuu, tatizo humu jf wamejaa singo Maza wengi ambao wana binti zao na wanategemea kuwaozesha bila uwepo wa baba au ndugu wa baba wa binti.

Kwa mwanaume anayejielewa hawezi kuoa binti aliyekulia katika hayo mazingira kwani tabia ya binti uwa ni copy ya tabia ya mama yake na ndo maana ndoa nyingi hazikai kwa kipindi hiki kwa sababu ya watoto walio lelewa upande mmoja
 
Hapa mnahangaika bure kuwa na mjadala mrefu. Upande wa baba hauhusiki kwa jambo lolote mahari inapokelewa na wajomba.

Huyo baba anayezungumzwa yeye mwenyewe hatambuliki na familia ya mama wa binti. Na hii inaonyesha wazi pia huyo baba wa binti hajawahi jitambulisha kama ndio mwenye mtoto wala kutoa mahari yoyote kwa mzazi mwenzie na hata malezi ya mtoto. Anakuja kuhusikaje kupokea mahari? Mtoto mpaka anafikia umri wa kuolewa baba yupo tu hafanyi jitihada zozote kuhusu mtoto wake. Uhalali wa kuwa mzazi unakuja na wajibu.
Tatizo siyo kupokea mahari bali ni kwanini binti hajui ndugu yake yeyote upande wa baba? Unadhani huyo binti anaweza kuwa mke mwema?
 
Ni Kweli kabisa.
Mwanamke asiyelelewa na baba ni janga sana. Angalau Binti apate malezi ya baba ajue hekaheka za kufokewa mara nyingine na baba au ukali Wa baba japo Wa baba SIO wakali sana Kwa Binti zao lakini baba hawapeandi Kuona mabinti wanakua na uhuru Wa kuzurura mitaani au kusimama simama na wanaume mitaani.

Sasa ambaye ni single mother Hali ni Tofauti Inabidi umlelee kikekike na wanawake Wana ubinafsi Wa kutaka uhuru mkubwa Karne hili . Atataka uhuru aliokua anaiona Kwa mama yake aishi hivyo hivyo,yaani single maza Hata akiamua Kulala NJE hakuna Wa kumuuliza na haogopi chochote. Akiamua kubadili wanaume usiku na mchana hakuna Wa kumuuliza. Sasa Binti Aliyekulia kwenye mazingira yasiyo na utaratibu Wa kibaba na kimama ndani ya Ndoa ni Mungu tu ataweza kumfanya awe Mwanamke Bora.

Hata hivyo Kwa sana Ndoa kuvunjika ndani ya Miezi mitatu imeshakuwa ni jambo la Kawaida
Kweli mkuu, kuna mambo madogo madogo waoaji huwa wanayapuuzia. Kama binti hatambui ndugu yeyote upande wa baba, technically hafai kuwa mke. La sivyo utamuona leo baada ya wiki kesharudi kwao.

Na pili cha kujiuliza ni kwamba mkizaa mtoto akawaletea mchumba ambaye ni ndugu wa upande wa baba wa mke wako je utamfanya nini mtoto wako?
 
Kama alivyosema Mwanamayu kwa usukumani iwapo baba yupo na haeleweki ama keshatangulia basi uJombani wanapokea mahari kiroho safi tu yani

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama mahari inapeleka ujombani lakini binti anatambua ndugu zake upande wa baba hiyo haina shida.

Shida nao kwamba binti hatambui ndugu yeyote upande wa baba. Je huyo binti anafaa kuwa mke?
 
Komeni kuwaandama single mothers, ni ukosefu wa nidhamu na ni kinyume na utu.

Unasema mahari ipokelewe na baba ambaye hata hamjui binti. Hapo kuna baba kweli.

Unasema binti hafahamiani hata na ndugu mmoja upande wa baba, hapo undugu uko wapi?

Halafu taratibu za mahari za kwenu ni tofauti na watu wengine. Upande wa bi harusi ndio unaoandaa taratibu zote za mahari na namna gani mahari ipokelewe, sio wewe unayepanga.
Kwa mim ninavyoelewa mahari maana yake ni shukran ya mume kwa wakwe(wazazi wa anaeolewa) kama ni mzaz mmoja ndo amewajibika kumlea mtoto tangu yupo tumbon huyo ndo anastahili hyo shukrani.

Mm naelewa hvyo
 
Kiislaam, hata baba akiwepo na kamlea na anaishi nae, mahari ni ya anaeolewa si ya baba wala ya mwengine yeyote.
Sawa anaweza kupokea binti. Ila binti kutotambua ndugu yeyote upande wa baba je ni sawa?
 
Huyu binti kalelewa na mama yake pekee yake. Baba yake yupo hajafa ila binti hajawahi kukutana ana kwa ana na baba yake wala katika upande wa baba yake hamjui ndugu yeyote.

Je, kwa scenario kama hiyo binti anafaa kutolewa mahari na kuolewa?

Na taratibu za mahari zipoje? Kwani navyojua mahari ni ya baba na kama baba hayupo mahari ipokelewe na yeyote upande wa baba yaani shangazi au baba mdogo au mkubwa.
Pesa yasumbuwa sana binadamu. Kwani lazima huyo binti atolewe mahari? Kwani binti anaozeshwa au anauzwa kama mbuzi? Kwani lazima wazazi wote wagombanie mahari?
 
Back
Top Bottom