Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Gana

Member
Joined
Oct 27, 2021
Posts
79
Reaction score
139
Miaka yangu 26 ( me)..

1. Kiwanja ninacho 1
2. Bank nina mil 3
3. Tayari nimeshatoka nyumbani kitambo (najitemegea)
3. Nimeajiriwa kwenye N.G.O ( afya) kwa mkataba wa miaka 3.

Je, naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye hicho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
3. Nawaboost wazazi kusomesha mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa 1..
4. Kuhonga kwa akili
5. Kuwaboost wana & ndugu pale ninapohitajika
 
huo ni mtazamo wako, wahindi karibu wote mjini hawana nyumba ila wana biashara. Nyumba siyo asset bali liability. ukikua utakuja kujua
Usilazimishe tufanane nao.

Jenga Mzee, likitokea lolote upo kwako, uwe tajiri uwe masikini, uwe mzima au mgonjwa, uwe na ajira ua laa upo ndani kwako.

Hata ukishindwa kumaliza nyumba, utakua umeongeza thamani kiwanja chako utauza.
 
Lakini wahindi hawajaajiriwa, huyu kaajiriwa. Mjini hapa ukifungua biashara ukampa mtu asimamie umekwisha.
Wengi wenu hamna experience ya ujenzi, mnafikiri ujenzi ni rahisi, kama hauna usimamizi ni kama unagawa hela zako kwa mafundi. Utaibiwa mpaka mchanga na kokoto site.

The good idea, aanzishe biashara ata mkataba utakapoisha aikute biashara imesimama aendelee nayo. Ukijenga ukiwa hauna source nyingine ya income, ultimately utaiuza hiyo nyumba.
 
Back
Top Bottom