Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Miaka yangu 26 ( me)..

1. Kiwanja ninacho 1
2. Bank nina mil 3
3. Tayari nimeshatoka nyumbani kitambo ( najitemegea)
3. Nimeajiriwa kwnye N.G.O ( afya) kwa mkataba wa miaka 3.

?? Je naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye icho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine..?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
3. Nawaboost wazazi kusomesha mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa 1..
4. Kuhonga kwa akili
5. Kuwaboost wana & ndugu pale ninapohitajika
Kwenye ujenzi kinachofanyika ni kuzamisha hela na sio kupata hela. hiyo milioni 3 kama ni nyumba kubwa ya familia hata msingi haumalizi. Kama umedhamiria kuachana na mambo mengine yote kwanza endelea ila uwe determined kuwa kila unachopata unatupia hapo.

Kintume na hapo kama lengo lako ni kuzalisha hela kafanye biashara, hicho kiwanja endeleza kidogo kidogo. anza kwa kutafuta ramani na taratibu za vibali. then mwaga mawe. Ukikimbilia ujenzi kichwa kichwa utalia.
 
Wengi wenu hamna experience ya ujenzi, mnafikiri ujenzi ni rahisi, kama hauna usimamizi ni kama unagawa hela zako kwa mafundi. Utaibiwa mpaka mchanga na kokoto site. The good idea, aanzishe biashara ata mkataba utakapoisha aikute biashara imesimama aendelee nayo. Ukijenga ukiwa hauna source nyingine ya income, ultimately utaiuza hiyo nyumba.
Utaiuza Kwa faida. Yaani itakuwa ni kama umefanya biashara tu.
 
Mh ujenzi sio lele mama kaka nakushauri hyo pesa endelea kuikuza kuza maana hujui kwamba mkataba utaweza kuongeza au vip kuna maisha baada ya mkataba kuisha na hyo pesa kwa sasa usifanye biashara chonde chonde
Shukran!.. ata kama naamua kuanza kuanza ujenz sio kwa sasa.... pesa bado
 
Mwisho unarudi kwenye wazo langu la biashara
Mzee baba utakua unaish sana humu ndani #rich dad poor dad View attachment 2477294View attachment 2477295
20230111_123836.jpg
 
Miaka yangu 26 ( me)..

1. Kiwanja ninacho 1
2. Bank nina mil 3
3. Tayari nimeshatoka nyumbani kitambo ( najitemegea)
3. Nimeajiriwa kwnye N.G.O ( afya) kwa mkataba wa miaka 3.

?? Je naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye icho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine..?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
3. Nawaboost wazazi kusomesha mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa 1..
4. Kuhonga kwa akili
5. Kuwaboost wana & ndugu pale ninapohitajika
Nyumba inakuwa asset pale tu itakapoisha ukaishi mwenyewe na kusaidia ku-save kiasi ambacho ungelipa kodi au kuleta rent kama umeipangisha, otherwise kwa ujenzi wa miaka yetu 5-10 ni liabillity kwa kipindi chote hicho....... On my views, kama muda, akili na utashi wa biashara vipo basi anza ku-invest kwa kuwekeza hiyo pesa izalishe, faida ndo uwe unaitia kwenye ujenzi!!.....
 
Mzee baba utakua unaish sana humu ndani #rich dad poor dad View attachment 2477294View attachment 2477295View attachment 2477296
Honestly, sijawahi kusoma hicho kitabu ila nilimnunulia dogo. Ni katika hali ya kawaida, ukinjenga nyumba una invest hela nyingi na mara nyingine return yake inachukua muda mrefu au usipate. So, kwa watu wazima wenye kutaka comfort, fine, ila kwa wewe kijana, pambana changamsha akili, fanya uwekezaji. Umefanya vyema kununua kiwanja, tena ukijenga jenga nyumba ya biashara na wewe ukae humo humo.
 
Nyumba inakuwa asset pale tu itakapisha ukaishi mwenyewe kwa kusaidia kusave kiasi ambacho ungelipa kodi au kuleta rent kama umeipangisha, otherwise kwa ujenzi wa miaka yetu 5-10 ni liabillity kwa kipindi chote hicho....... On my views, kama muda na akili na utashi wa biashara vipo basi anza kuinvest kwa kuwekeza hiyo pesa izalishe, faida ndo uwe unaitia kwenye ujenzi!!.....
Poa poa mkuu
 
Honestly, sijawahi kusoma hicho kitabu ila nilimnunulia dogo. Ni katika hali ya kawaida, ukinjenga nyumba una invest hela nyingi na mara nyingine return yake inachukua muda mrefu au usipate. So, kwa watu wazima wenye kutaka comfort, fine, ila kwa wewe kijana, pambana changamsha akili, fanya uwekezaji. Umefanya vyema kununua kiwanja, tena ukijenga jenga nyumba ya biashara na wewe ukae humo humo.
Kwenye icho kitabu muandish!... anaandika nyumba ni liability!.
 
Back
Top Bottom