Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Kwa 3M fanya biashara ya kuku utoboe tu. Hata ukifa bila nyumba sio mbaya cha msingi sehemu ya kulala unayo[emoji28][emoji28] natania tu
Kiufupi fanya kwanza biashara, nyumba utajenga pale utakapokuwa stable kifedha
 
Jenga kwanza, anayekuambia ufungue biashara hakupendi au hajui maisha.

Maisha ni nyumba mkuu, mambo yote yakikwama unarudi home.
Mambo yakikwama hata hiyo nyumba atauza. Kazi anayofanya ni ya mkataba, ipo siku anaweza kukosa hiyo ajira.

Kuna siku atakuja kukumbuka ni bora angekua na kibiashara chake sehemu kipindi ambacho kazi hana
 
Ikitokea ukakosa kazi ndio utajua kuwa nyumba ni upumbavu kabisa. Utakua unashinda humo na stress zote huku hata pesa ya kula shida, na mwisho kabisa unaweza fikiria kuiuza au kuikopea mkopo ufanye mishe yoyote. Na hapo ndio itakua mwisho wako

Tafuta biashara hata ya pesa ndogo, anzisha na komaa nayo. Siku ukipoteza kazi, hiyo biashara ndio itakua sehemu ya wewe kukuondolea stress ya kukaa tu bure.
 
Miaka yangu 26 ( me)..

1. Kiwanja ninacho 1
2. Bank nina mil 3
3. Tayari nimeshatoka nyumbani kitambo ( najitemegea)
3. Nimeajiriwa kwnye N.G.O ( afya) kwa mkataba wa miaka 3.

?? Je naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye icho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine..?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
3. Nawaboost wazazi kusomesha mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa 1..
4. Kuhonga kwa akili
5. Kuwaboost wana & ndugu pale ninapohitajika
Kujenga inawezekana hata kama utaanza na laki tatu kikubwa uwe na flow nzuri ya income tu
 
Jenga kwanza, anayekuambia ufungue biashara hakupendi au hajui maisha.

Maisha ni nyumba mkuu, mambo yote yakikwama unarudi home.
Maisha ni nyumba kwa watu wenye mtazamo kama wako.

Kama hana familia nyumba anajenga ya nini awekeze akuze mtaji.

Nyumba inawezekana kujenga hata kwa mwezi mmoja kama atakuwa na hela ya kutosha.
 
Miaka yangu 26 ( me)..

1. Kiwanja ninacho 1
2. Bank nina mil 3
3. Tayari nimeshatoka nyumbani kitambo ( najitemegea)
3. Nimeajiriwa kwnye N.G.O ( afya) kwa mkataba wa miaka 3.

?? Je naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye icho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine..?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
3. Nawaboost wazazi kusomesha mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa 1..
4. Kuhonga kwa akili
5. Kuwaboost wana & ndugu pale ninapohitajika
Ushauri wa watu humu wengi ni vitu havina uhalisia wowote wa maisha ya MTANZANIA wa kawaida .... mara Nyumba ni liability,mara Wahindi hawana nyumba hivi vitu vyote ni bushshit unacho takiwa kufanya jiangalie wewe kama binafsi umeplan nini katika maisha yako baadae kuwa mfanyabiashara au kuwa muajiriwa nakusuhi usifate mkumbo tu maana kama unatoka family maskini ukianguka unaweza kuwa ndio moja kwa moja huna back up yoyote nyuma.

Umri ulio kuwa nao 26yrs old hardly unayo miaka 5 tu mbele utahitaji kuwa na family yako hapo ndio maisha halisi unakuja kuyaona.

Ushauri kama unakiwanja na una hela BANK na una kazi kwa sasa nenda kaanze kujenga taratibu wacha kabisa kufikiria biashara kwa sasa concentrate na kazi yako huu ni ushauri tu.

Sent from my SM-S901B using JamiiForums mobile app
 
Kwa milioni tatu mdogo wangu, toa milioni moja ingiza kwenye biashara. Usitoe mil 3 yote unaweza kuja kua kichaa. Pambana na hiyo biashara ikikua unaitanua hiyo hiyo. Hakikisha mtaji wako wa kwanza ni hiyo milioni moja. Kadri inavyozidi kujizungusha ile faida unaigawa unafanya mambo yako kidogo kidogo.

Kiufupi nnachotaka kukushauri usijengee stagnant money. Yaani ela ambayo inatoka tu haiingii wala haiingizi faida. Utajikuta umerundika matofali huna hela ya kula una nauli tu ya kuendea site kulinda matofali.

Kikubwa hongera kwa umri huo kuwaza jambo hilo.

Kila la kheri. Utaweza👍🏼
 
Kila la kheri. Utaweza[emoji1360]
Kwahiyo ache kazi anayo fanya ? ambaye ndio msingi wa yote aliye kuwa navyo akaanze kufanya biashara au .

Sent from my SM-S901B using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo ache kazi anayo fanya ? ambaye ndio msingi wa yote aliye kuwa navyo akaanze kufanya biashara au .

Sent from my SM-S901B using JamiiForums mobile app
Kwa akili yako we unadhani wafanya biashara wote mjini hawana kazi? Au kwamba wafanya kazi wote hawana biashara? Ni kichwa cha mtu. We kaa hapo tegemea mshahara wako kwa maisha haya. Sio lazima afanye biashara anayojiegesha hapo 24/7.

Muwe mnasoma kuelewa sio kusoma ili ujibu kuna sehemu nimemwambia aache kazi?

Akijiona mwepesi kufanya biashara anafanya na wateja wake ni hao hao anaofanya nao kazi au we unadhani biashara zote ni za kutembeza?

Na ndo maana nimemwambia asiingize hela yote achukue milioni maana yake ni kwamba anajaribu na akifanya uchaguzi sahihi si haba hawezi kukosa. Maamuzi ni yake
 
Biashara anaijua...kuna jirani yangu mwaka jana wamechukua mkopo wa million 20 wakasema wanafanyia baishara .

Kufupisha story baada ya mwaka baishara imekufa wamebaki na gari. Mkopo wanaendelea kulipa wakiwa nyumba za kupanga.
Usikope kuanzisha biashara usiyoijua su ambayo huna uzoefu nayo. Kopa kuendeleza biashara unayoielewa. Japo sijajua scenario yao ila biashara ina mambo mengi balaa
 
Ikitokea ukakosa kazi ndio utajua kuwa nyumba ni upumbavu kabisa. Utakua unashinda humo na stress zote huku hata pesa ya kula shida, na mwisho kabisa unaweza fikiria kuiuza au kuikopea mkopo ufanye mishe yoyote. Na hapo ndio itakua mwisho wako

Tafuta biashara hata ya pesa ndogo, anzisha na komaa nayo. Siku ukipoteza kazi, hiyo biashara ndio itakua sehemu ya wewe kukuondolea stress ya kukaa tu bure.
Nimekuelewa sana
 
Back
Top Bottom