Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Miaka yangu 26 ( me)..

1. Kiwanja ninacho 1
2. Bank nina mil 3
3. Tayari nimeshatoka nyumbani kitambo (najitemegea)
3. Nimeajiriwa kwenye N.G.O ( afya) kwa mkataba wa miaka 3.

Je naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye hicho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
3. Nawaboost wazazi kusomesha mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa 1..
4. Kuhonga kwa akili
5. Kuwaboost wana & ndugu pale ninapohitajika

Tujue kwanza Huko NGO unapokea walau kiasi gani kwa Mwezi..
 
Njia nzuri ya kuweka pesa za kujengea nyumba ni kuanza kuijengea hiyo kama utakuwa na flow ya income unaweza kumaliza boma na usijiue hata limeishaje.

Mwaka jana nilianza ujenzi nyumba kubwa tu lakini nilikuja kumaliza boma kimasihara sana.
Hongera sana
 
1. Jenga 'kipolisi post' uhamie wakati unasuribi kujijengea uwezo wa nyumba kubwa.

2. Sababu kazi yako ni ya mkataba, anza kufanya biashara ili usiadhirike mkataba ukiisha
Una maanisha ajenge chumba kimoja?

Chumba kimoja

Ramani ya Chumba kimoja

●1 masterbedroom

MAHITAJI

●Tofali za Msingi 250
●Tofali za Boma 520
●Cement mifuko 5(Msingi)
●Cement mifuko 8(Boma)
●Cement mifuko 4(Mkanda)
●Cement mifuko 3(Lintel)
●Nondo pc 5(Mkanda)
●Nondo pc 4(Lintel)
●Rings 7×4 pc 20(Mkanda)
5×4 pc 15(Lintel)

●Mchanga trip 1 lorry la 4 cubic metre.
●Kokoto trip 1 lorry la 4 cubic metre
●Mbao za 2×2 pc 18(Kupaua&brandering)
2×4 pc 20(Kupaua)
1×10 pc 10(Mkanda&Lintel)
1×5 pc 5(sahani)
●Misumari ya nch 4 kg 5(Kupaua)
nch 3 kg 3(Mkanda)
Kofia kg 5(Kupaua)
●Bati pc 10 za futi 10(Simba Dumu)

GHARAMA YA MATERIAL NYUMBA NZIMA NI ML 2.7
 
Wengi wenu hamna experience ya ujenzi, mnafikiri ujenzi ni rahisi, kama hauna usimamizi ni kama unagawa hela zako kwa mafundi. Utaibiwa mpaka mchanga na kokoto site.

The good idea, aanzishe biashara ata mkataba utakapoisha aikute biashara imesimama aendelee nayo. Ukijenga ukiwa hauna source nyingine ya income, ultimately utaiuza hiyo nyumba.
Wewe unafanya biashara gani?
 
Miaka yangu 26 ( me)..

1. Kiwanja ninacho 1
2. Bank nina mil 3
3. Tayari nimeshatoka nyumbani kitambo (najitemegea)
3. Nimeajiriwa kwenye N.G.O ( afya) kwa mkataba wa miaka 3.

Je naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye hicho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
3. Nawaboost wazazi kusomesha mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa 1..
4. Kuhonga kwa akili
5. Kuwaboost wana & ndugu pale ninapohitajika
Nilianza ujenzi nikiwa na mil 1.4 iliyopatikana baada ya kuuza kigari changu.
Anza na hii ramani. Mambo yakiwa mazuri, utajenga kubwa kwa mbele.
20220709_105225.jpg
 
Je naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye hicho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
 
mawazo yangu binafsi juu

kwa fact.. tutasema ufanyebiashara kwanza ukuze kipato ndio uanze ujenzi.. nakukumbusha tu kuwa makini na biashara unayotaka kufanya maana biashara ni zaidi ya kuajiriwa pia ni zaidi ya maono (imaginations) uliyonayo. Unaweza waza juu ya biashara fulani ukaona kabisa na mahali utakapopigia mpunga lakini ukaingia field ikaja na mambo mengi mnoo mpaka ukahisi kuchanganyikiwa. Kama utaamua kuanza na biashara nakushauri kwepa biashara za kuuza kwa mtumiaji wa mwisho,,, huwa ni ngumu mno kuliko biashara inayokukutanisha na mafundi au wanunuaji wanaoenda kuuza na wao(jitahidi uwe na uelewa wa kutosha kabisa juu ya biashara yako)

Tukija kwenye suala la ujenzi,hapa ndio kwenye uhalisia wenyewe, kulingana na fedha ulizonazo jenga nyumba isiyo na mambo mengi ili uweze kuimaliza kwa wakati yaani ndogo tu, usitake mambo mengi.Mfano unajenga kama vyumba ukiwa na malengo baadae utakapo jenga nyumba yako ya familia basi hapo utaweka wapangaji. Hii itakusaidia ujenzi usikufilisi sana

Jambo ambalo nimeliona kwako ni unatamani kufanya biashara ila unauoga wa kuumizwa na biashara na hutaki kupoteza kitu, so nakushauri jenga room hata mbili ili zikupe confidence ya kuingia kwenye biashara kwamba mambo yakiwa magumu una pa kuanzia.. maana kodi utakua hudaiwi
 
Yah mkuu upo sahih
 
Huu ndio ukweli Anza kujenga then ufungue biashara baadae utakuja kunishukuru,,

Ila ukianza biashara kabla hujajenga ,,utajikutq unamaliza nyumba za kupanga TU,,...

Mfanyabiashara hapendi kutoa hela kwenye biashara na kupeleka kwenye mambo km hayo...

Huenda mnamdanganya kaka wa watu nyie au na nyie pia hamna elimu ya kutosha kuhusu haya mambo. Kuna watu wameishia kwenye umaskini kwa sababu walidanganywa kuwa kujenga ndo kila kitu. ngoja nikuambie. Mwalimu au mfanyakazi wa serikali anayeweza kuchukua mkopo benki, ili ajenge nyumba nzuri ya familia anahitaji kati ya milioni 50 hadi 70 kutegemea na factors mbali mbali kama vile ukubwa wa nyumba, sehem ilipo na gharama za vifaa na pia design. Mtumishi huyu atachukua mkopo benk wa milioni 50 au 60 ambapo atakatwa kwa miaka 7. Milioni 60 hadi umalize marejesho benki watakuwa wamechukua milioni kama 90 hivi pamoja na riba zao. Assume hiyo nyumba umepangisha kwa kodi ya laki 3 kwa mwezi (assume hii nyumba haipo city centre). kwa mwaka utakusanya milioni 3.6, miaka 10 itakuwa 36 million. itakuchukua takriban miaka 25 kurudisha hela ulizokatwa benki. Hapo bado nyumba inadai ukarabati. Nakuambia kama hauna mzunguko mwingine wa hela lazima ufe kwa pressure.
 
Anza kujenga mdogo mdogo
Achana na biashara
Asilimia 95 ya biashara mpya hufa kibudu, mind you not to fool yourself that you will be smarter than those 95% who are failing
Kama Una mshahara ambao Unaweza kutoa walau laki 4 Kila mwezi na tayari Una 3M, Anza kujenga mkuu, mambo mengine yatajiseti taratibu mbeleni
 
Ushauri wangu ni uanze na ujenzi
1. Tafuta ramani simple pref 3 bedrooms with 1 master only
2. Fikia mpaka hatua ya kuezeka..
3. Weka Grill zote na mlango wa mbele na nyuma.
4. Izibe upande mmoja na fanya finishing upande utakaoweza kuanza kutumia pref master or 1 bedroom and toilet, dining, and kitchen.
5. Ukijipanga utamalizia kulikobakia
 
Shukran mkuu..
 
Shukran mkuu
 
Back
Top Bottom