mawazo yangu binafsi juu
kwa fact.. tutasema ufanyebiashara kwanza ukuze kipato ndio uanze ujenzi.. nakukumbusha tu kuwa makini na biashara unayotaka kufanya maana biashara ni zaidi ya kuajiriwa pia ni zaidi ya maono (imaginations) uliyonayo. Unaweza waza juu ya biashara fulani ukaona kabisa na mahali utakapopigia mpunga lakini ukaingia field ikaja na mambo mengi mnoo mpaka ukahisi kuchanganyikiwa. Kama utaamua kuanza na biashara nakushauri kwepa biashara za kuuza kwa mtumiaji wa mwisho,,, huwa ni ngumu mno kuliko biashara inayokukutanisha na mafundi au wanunuaji wanaoenda kuuza na wao(jitahidi uwe na uelewa wa kutosha kabisa juu ya biashara yako)
Tukija kwenye suala la ujenzi,hapa ndio kwenye uhalisia wenyewe, kulingana na fedha ulizonazo jenga nyumba isiyo na mambo mengi ili uweze kuimaliza kwa wakati yaani ndogo tu, usitake mambo mengi.Mfano unajenga kama vyumba ukiwa na malengo baadae utakapo jenga nyumba yako ya familia basi hapo utaweka wapangaji. Hii itakusaidia ujenzi usikufilisi sana
Jambo ambalo nimeliona kwako ni unatamani kufanya biashara ila unauoga wa kuumizwa na biashara na hutaki kupoteza kitu, so nakushauri jenga room hata mbili ili zikupe confidence ya kuingia kwenye biashara kwamba mambo yakiwa magumu una pa kuanzia.. maana kodi utakua hudaiwi