Je, Ndoa ni Jela ya Wanaume? Je, walioko ndani wanatamani kutoka?

Jela kivipi? Hiyo jela unaitengeneza kichwani mwako tu. Ndoa haina matata kwa mtu anayetumia akili zake vema. Ila, kama akili ni za kushikiwa ndiyo utaipata fresh ya shamba. Unakuwa ni "the captivity of your own prison"!
Ukute ndoa yako ina changamoto kinoma,ila unaandika kua INAHITAJI MTU ANAYETUMIA AKILI.
 
Maamuzi ni yako! Ukitaka iwe jela inakua ukitaka isiwe inakua!

Kwa wakristo Ni jela haswaaaa Wala sio utani,mwanamke akiipata ndoa ya kikristo ataanza kuitumia atakavyo kama malengo binafsi yakitimia!!
 
Ndoa ngumu ila mwanaume bila ndoa maisha yako yataharibika sana kuliko hata huo usumbufu wa mwanamke
 
Tafuta mwanamke ambaye Hana chembe chembe za ufenism uoe uache kuishi kihuni.
Mwanaume kuna umri ukifika bila ya kuwa na mke unakuwa fala Fulani tu.
Kwamba niache kufanya mambo yangu nianze kutafuta mwanamke wa kumuoa. Hiyo stage ya kutafuta wanawake nishavuka mdogo angu. Mimi nipo kwenye stage ya kutafutwa na wanawake. Infact nishaoa lakini sio huo upuuzi wa kusainishana mikataba. Kwanza unajua kama kuoa na ndoa ni vitu viwili tofauti
 
Inategemea umeoa mwanamke wa aina gani, ukioa mwanamke mpumbavu utatamani utoke kwenye ndoa hata kesho. Ila ukioa mwanamke sahihi nawewe ukawa mwanaume sahihi( right mindset ) maisha yanakuwa bora sana.
Mimi kwa kweli sina mpango wa kuishi maisha ya kibachelor tena, yale maisha hayakuwa mazuri. Hata kama okitokea mke wangu akizingua ( Mungu aepushe mbali) ndoa ikavunjika itabidi tu nioe mke mwingine.
 
Mwanamke ni msaidizi, Mungu alimuumba mwanamke ili awe msaidizi kwa mumewe. Mimi huyu mke wangu amenisaidia vitu vingi, amefanya maisha yangu yawe bora zaidi, akisafiri huwa najiona kabisa ninavyo struggle. Kwanza mke ndio anafanya nyumba kuwa home, nyumba bila mke ni pango tu la kupumzishia fuvu.
Kukataa kuoa ni sawa na kuamua kuacha kutumia bodaboda na kutembea kwa miguu eti kwa sababu bodaboda zinasababisha sana ajali.
 
Ukute ndoa yako ina changamoto kinoma,ila unaandika kua INAHITAJI MTU ANAYETUMIA AKILI.
Ndio maana kasema ndoa inahitaji mtu mwenye akili ya kutatua changamoto.
Ndoa inachangamoto kama yalivyo mambo mengine , hakuna kitu ambacho hakina changamoto. Kazi zinachangamoto ila hatuaachi bali tunazitatua au kutafuta njia ya kuchukuliana nazo. Vile vile na biashara, na ndugu pia wana cchangamoto, kila sehemu kuna changamoto.
 
Tuacheni kwanza tutibu madhara ya nyeto tukipona tutaoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…