Je, Ndoa ni Jela ya Wanaume? Je, walioko ndani wanatamani kutoka?

Je, Ndoa ni Jela ya Wanaume? Je, walioko ndani wanatamani kutoka?

Wengi wenye dhamira halisi na upendo wa ndoa wanaishi maisha mazuri sana. Ndoa imewafanya watulie, wawe na faraja na baraka katika maisha. Ndoa imewaepusha na majanga mengi. Heshima yao imepanda mtaani, mjini , katika familia na na marafiki.

Usisikie porojo za wapinga ndoa, tafuta mwenza anaefaa kwa ndoa kutoka familia inayo thamini ndoa.
 
Kijiweni hapa Nyasaka!
Jana nilitoa mada kuhusu vijana kutokufanya maamuzi magumu ya kuwa na familia (ndoa) na kutulia na mwanamke.

Wengi wao waliona heri atafute watoto tu ila sio kukaa na mwanamke sababu wengi hawaeleweki nini wanataka.

Nilipowauliza swali vijana waliooa walisema ingekuwepo nafasi ya 2 kichagua kuoa au kuendelea na maisha yao single walichagua kubaki single sababu ya mtiti wa familia.

Sasa najiuliza na kuuliza kwenu mlio na wanawake na wenye familia, inshu ni matunzo ya familia na majukumu ndio yanabana kiasi cha kutaka kukimbia au hawa hawakuwa tayari na walikurupuka?

MLIO NA WAKE NDANI TUPENI USHAURI KABLA SISI HATUJAWEKA MIGUU HUMO.
Mimi nipo kwenye ndoa 2,moja ina miaka 30 na nyingine 40,sijioni nipo jela bali najiona nipo kwenye funua ya raha,furaha,amani na ushirikiano na wake zangu
 
Tatizo SI ndoa (kuoana). Tatizo ni umasikini.
Ndoa tamu sana aisee.
Shida ukiwa masikini, ndoa inakuwa chungu kwa sababu ya majukumu kuongezeka, kukosa muda wa binafsi na pesa ya kustarehe/kujifurahisha. Ndo umaanza kuhusu uko jela.
We jamaa hauko serious hata kidogo kwahiyo akina Bill gates, Elon Musk? Na saa hii Obama kitawaka sio muda mrefu. Wote hawa hawana hela au?
 
Mkuu mi nimesha toka ku collect divorce paper jana. Am free, hayo masuala kwasasa tumewaachia wengine
Screenshot_20250726_212557_WhatsAppBusiness.jpg
 
Mlizoea kuona vichaa wa kiume,soon mtaanza kuona idadi kubwa ya vichaa wa kike. Hali sio nzuri. Shetani amewashika wanawake wa kizazi hiki kwa nguvu sana.
 
Back
Top Bottom