Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Genius

Asante sana. Umetoa somo mubashara sana Chief.

Wengi sana wakichukua mikopo hufanya makosa kama ulivyoainisha hapo juu nakuishia kulia na kuhangaika. Sometimes mkopo hubadilika kua laana. Asilimia kubwa sana ya watu hawana elimu uliyotoa hapa - wengi sana
Usikope kuanzisha mradi ama biashara, kopa ili kuendeleza....si maneno yangu bali ni maneno ya kijana wangu mmoja aliepo makao makuu CRDB.

Mimi ni nani hata nikope bank, wacha nife maskini tu.
 
Mkuu mm nimeamua ku-invest kwenye Career & biashara za vifaa vya ujenzi at least kila mwezi na-save 500,000/= kutoka kwenye mshahara pia nina Hardware Tegeta hata ikitokea lolote naweza ku-survive kwa kipindi kirefu. Sasa wewe jiloge ukajenge Msata kazi izingue utakula tiles

Umefanya maamuzi makini naya busara sana
 
Mimi ndo nataka nijilipue hivyo mkuu daah...nataka outlander na nifanye ujenzi..biashara ipo lakini inasua sua nimeshaweka kama 10m kwenye biashara lakini mzunguko bado sio mkubwa unanishauri vipi hapo mkuu..?

Chief

Ni biashara gani unafanya. Tunaweza kukusaidia mawazo yakimkakati
 
Ni kweli kwa hilo wahindi wanapatia sana

Nilifanya kazi benki kati ya mwaka 2013 mpaka 2015 na nilikua na process applications za products fulani ambazo zililazimu kuona salary slips na savings za watu. Nilishangaa kuona wahindi wengi wana hela benki kati ya million 50 mpaka 100 na zaidi lakini kwenye makazi wameandia STAYING WITH PARENTS
Uoe/uolewe afu bado mkae kwa wazazi kibongo bongo hivii?..

Tutofautishe family model jmn
Afu Wanaoana ndugu

Na wana trauma ya kutaifishuwa vitu na serikali
 
Mm nimeanguka mara 12 zote chali juzi nimefanya mahesabau nanwife 100m zemeenda biashara inachangamotk zake sanankwa hapa tanzania uliwa mkweli hupati faida kbs

Unachoongea ni kweli

Biashara zina changamoto sana sana hapa tanzania - sio lelemama. unaweza kutaja biashara tatu au 4 ulizofanya zikafeli mkuu? Tuweze kujadili kidogo
 
Kiukweli wahindi hawanaga usenge wa kupanga matofali kabisa na wana hela mbaya kabisa. Huo ufala tunao sisi weusi 😂😂😂 ati nyumba ni heshima.
Ni heshima tena kubwa sana

Hasa nyumba ya kuishi ya familia

Tena ukiona mtu kajenga kamaliza msalimie shkamoo kujenga si mchezo..unamimina pesa htr
 
This is far better kuliko ujenzi
Unajenga nyumba ya 50Mil kusubiri kodi ya almost 800K kwa mwaka.
Mwaka wa tatu tu utasikia bomoa, mara uchakavu mara makao makuu yamehama mara sijui nini
🤣🤣🤣🤣🤣 kweli it was a great idea ila kwa Vodacom, haikuwa mahala sahihi pa kuweka pesa. Kampuni ilikuwa ina struggle na biashara hisa ilikuwa lazma ziporomoke tu. Maswala ya hisa niambie kwenye kampuni za madini huko tutaelewana.
 
Kidogo
Hata asie na experience tizama tu majengo ya kupangisha hata ofisi

Yako wazi..mengine hata floor za chini tu ambazo zina demand kubwa ziko wazi

Ama kama wapo hayajajaa..

Na mengine yako maeneo mazuri kabisa mf kariakoo

Zama hizi mhhh...

Ni kweli zama hizi the business landscape has truly changed
 
Ni heshima tena kubwa sana

Hasa nyumba ya kuishi ya familia

Tena ukiona mtu kajenga kamaliza msalimie shkamoo kujenga si mchezo..unamimina pesa htr
Ya family ni hakika hata mimi lazma nijenge kuweka address ya wanangu sawa. Ila kwa nyumba ya biashara ni uongo.
 
Achana na hao
Nenda kwenye makampuni makubwa ya kibiashara Vodacom airtel benk n.k
Wote hawa kuishia kupanga tu na sio kujenga mzee
Ujenzi ni dead project Mzee
Leo tunalaumu mifuko ya hifadhi za jamii kwakuwa mpesa yote wamepeleka kwenye ujenzi
Mojawapo ya demand for the 'stimulus package' pale USA ilikuwa ni wadau kuchukua pesa yao na kuizamisha kwenye ujenzi
Pata hela fanya biashara huwezi tia kwenye fixed account au kanunue hisa huko
Huwezi hayo yote ni bora upige tu chipsi zege na mayai na kuku sio ujenzi mkuu
Uwekezaji ktk real estate (ujenzi wa majengo) ni dead project??? Siyo kweli hata kidogo.

Tatizo kubwa zaidi kwa Waafrika na watu wengi duniani, sema Watu hawana mitaji ya kutosha ya kuwekeza, pia hawana Elimu ya kutosha sana juu ya uwekezaji huu wa real estates.
 
Biashara hua haipo hivyo hakuna biashara ya kusema mwezi mzima ninaweza kujaza vyumba viwe full sana sana utajaza nusu vyumba..robo etc biashara hua haipo constant kiivyo..hapo hujapiga hesabu ya kuibiwa hata vyumba vikiwa full utaletewa i.em watu watano au 10 ndo walilala

Angalizo zuri sana hili. Jamaa anaongea kama wale wanaofanya biashara za kilimo cha kupiga simu morogoro. Wewe uko dar umeajiri watu morogoro wanakulimia shamba lako - wote walipata hasara na walichemsha wote
 
Majumba mengi yako mikononi mwa mabenki wanataka yauza ila hakuna wateja. Wateja wanaogopa TRA watawafatilia kujua vyanzo vyao vya mapato. Mabenki yameamua kuwa wapole tu
 
Uko sahihi mkuu..
Mimi huwa naamini nyumba hazipandi thamani bali hela yetu inashuka thamani na kusababisha vitu kuwa ghali hivyo nyumba nayo inapanda bei. Ibadili kwa dollar ndio utajua huwa haipandi bei
 
Uwekezaji ktk real estate (ujenzi wa majengo) ni dead project??? Siyo kweli hata kidogo.

Tatizo kubwa zaidi kwa Waafrika na watu wengi duniani, sema Watu hawana mitaji ya kutosha ya kuwekeza, pia hawana Elimu ya kutosha sana juu ya uwekezaji huu wa real estates.
Real Estates ni kupiga Apartments na maofisi. Sio kujenga kanyumba kamoja kisha unasubiria kodi zije. Halafu nadhani kuna namna ya management ya Real estates.

Donald Trump ni Mogul wa hizo biashara toka enzi. Labda tumuulize
 
Uwekezaji kwenye real estate, shares au Treasury bill una faida mbili (1) Ni return on investment (2) Appreciation in value of investment. Nyumba kama nyumba utaona hiyo kodi ya TZS 600,000 ni ndogo sana lakini ukiuza hiyo nyumba utapata zaidi mfano hiyo nyumba ya TZS 150,000,000 unaweza ukauza TZS 300,000,000.
Kwa wale tunaowekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wetu; bado kuwekeza kwenye nyumba ni bora zaidi kuliko "Fixed deposit" kwani wakati nyumba ikiongezeka thamani kuendana na wakati, Principal amount kwenye Fixed Deposit haiongezeki thamani kinyume chake inapungua thamani (inflation).
Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida
Nyumba mbali na kuifanyia biashara ni assets kwako, waweza itumia kupata mkopo na kufanya biashara. Usitegemee kodi ya pango kuwa mapato yako. Rafikio anaetaka uza nyumba akafanye biashara mshauri. Akikwama biashara ataumia sana.
 
Back
Top Bottom