Je, ni halali na haki kwa baadhi ya Watumishi wa Mungu kujimilikisha kazi Mungu?

Je, ni halali na haki kwa baadhi ya Watumishi wa Mungu kujimilikisha kazi Mungu?

Kollebundle

Senior Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
176
Reaction score
109
Natumai wadau nyote mu wazima, tafadhalini naombeni mrejee kichwa cha habari hapo juu.

Je ni halali na haki watumishi baadhi wa Mungu nyakati hizi kujimilikisha kazi ya Mungu ikiwa ni kweli wanaifanya hiyo kazi kwaajili ya Mungu na siyo kujinufaisha wao? Na kama ni halali je, huo uhalali wameutoa wapi na kama upo wapi umeandikwa katika biblia?

Limekuwa likiniumiza kichwa na kunipa ukakasi sana suala la kwanini nyakati hizi watumishi wengi wa Mungu; hawa wahubiri, waimbaji wa nyimbo za injili na za kusifu na kuabudu, wamekuwa wakisema wanamtumikia Mungu ni kitu ambacho ni kizuri sana.

Lakini wakati huo huo hizo kazi zao za huduma yaani (mahubiri ya neno la Mungu, nyimbo za injili, nyimbo za kuabudu kusifu), wakisha zitengeneza basi hawataki kabisa wala kuruhusu mtu mwengine tofauti na wao kuzitumia hizo kazi zao za huduma, aidha kwaajili ya kuzisambaza, hapa nazumgumzia kusizambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ya mtu binafsi kama vile facebook, Twitter, Tik Tok, YouTube, tovuti.

Sasa swali linalonipa ukakasi wa kujiuliza mara mbili mbili ni kwamba;

1. Ikiwa ni kweli watumishi wa aina hii lengo lao ni kufanya huduma kuhubiri injili ili kumtumikia Mungu na kumletea mavuno mengi je, ni kwanini hawataki na hawaruhusu watu wengine wenye nia kama yao ya (kuhubiri injili kupitia izo kazi zao za mahubiri,nyimbo za kuabudu na kusifu, nyimbo za injili ambazo wamezitengeneza) wazitumie kazi zao aidha kwenye kurasa zao binafsi za mitandao ya kijamii au popote pale ili nawao wamletee Mungu mavuno mengine?

2. Je, huku kujimilikisha kwamba wao wenyewe tu ndiyo wenye haki ya kuihubiri injili kupitia hizo kazi zao na siyo watu wengine wameutoa wapi?

Na kama ni kweli, Biblia imeruhusu kuwa mtumishi wa Mungu akifanya huduma ile kazi ambayo ataitengeneza kwa kutoa maneno ya Mungu kutoka kwenye Biblia na kisha kutengeneza kazi aidha ni mahubiri, au nyimbo za injili, au za kusifu na kuabudu itakuwa ni mali yake binafsi na haitaruhusiwa mtu mwengine kuitumia mahali popote pale? Na kama ni kweli hii wameruhisiwa, imeandikwa wapi katika Biblia na mastari gani huo?

3. Pia huku kujimilikisha kazi ya Mungu wanayohubiri na kuzuia watu wengine kuzitumia hizo kaz ili kumuongezea Mungu mavuno zaidi, je, huku siyo kudumaza kazi ya Mungu isifike mbali?

4. Na je, hivi wadau kweli kitendo hiki watumishi wa Mungu wa aina hii wanavyofanya hivi kujimilikisha kazi ya Mungu wanayohubiri na kuzuia watu wengine wasizitumie kusimbaza na kumwongezea Mungu mavuno ya watu zaidi hivi kweli Mungu atakuwa anapendezwa na kitendo hiki kweli?

Sababu Mungu mwenye alisema tumletee mavuno, sasa mbona wao wanakazana sana kuwazuia watu wengine wasizitumie kusimbaza kazi ambazo wanasema wanamtumikia nazo Mungu? Mbona wao wanatumia neno la Mungu bure (maandiko ya kwenye Biblia) wala hawajazuiwa na Mungu kama ambavyo wao wanakazana kuwazuia watu wengine tofauti na wao walizozitengeneza wasizitumie au kuzisambaza izo kazi popote pale?

Sasa wao huu uhalali wa kuzuia watu wengine wenye nia njema ya kuendelea kuzisambaza kazi ya Mungu, ikiwa ni kweli wao wanamtumikia nazo Mungu, wameutoa wapi na huo ujasiri wameutoa wapi hata bila kuwa na aibu wala hofu? Kweli mwanadamu leo anafanya kitu kama hiki? 😳😳🙉🙉

Naombeni watumishi wa Mungu pamoja na wadau wengine mje hapa mtupe majibu sababu, sidhani kama Mungu atakuwa anafurahishwa na kitendo hiki kibaya wanacho kifanya bila hata kuona chembe ya aibu!
 
Back
Top Bottom