Je, mapungufu yana upungufu katika upungufu wake? Kwa sababu mapungufu hayajakamilika?
Hivyo, je, kwa kuwa hayajakamilika katika kukamilika, yamekamilika katika upungufu wake?
Au, hayajakamilika hata kwenye upungufu, kwa kuwa yangekamilika kwenye upungufu yasingekuwapo na yasingejulikana kuwa ni mapungufu?
Ukifikiria sana utaona, kitu ambacho hakina mapungufu hakipo. Kipo, lakini, kuwapo kwake kuna maana hakipo.
Kitu hicho ni nothingness, nothingness ni kutokuwepo chochote, hata vacuum in space si nothingness, kwa sababu ina space. Nothingness yenyewe hata space haina. Haina space, haipo kwenye time. Haipo. Inafikirika tu.
Hiyo nothingness haipo. Kwa kuwa kuwapo kwake ni kutokuwapo.Ikiweza kuwapo nje ya hapo tu, inakuwa si nothingness tena.
Hiyo dhana ya nothingness, kinadharia, ndiyo haina makosa. Kwa sababu ina lowet entropy, hauwezi kupunguza entropy hapo. Huwezi kuharibu, ili uharibu, inabidi uitoe kwenye nothingness.
Hiyo nothingness ndiyo haina mapungufu.
Kitabu cha kusoma ni "Why Does The World Exist: An Existential Detective Story" cha Jim Holt.