Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Natafuta kitu ambacho hakina kasoro hapa duniani, kitu kikamilifu kwa 100% kitu ambacho huwezi kukuta mawaa ndani yake.

Nimeangalia kama dini, zote zinamapungufu ndani yake.

Kama ni elimu zote zina mapungufu ndani yake, zimekosa majibu mengi.

Kama ni sera za vyama, sera za vuama vyote vimejaa mapungufu

Kama ni kazi za sanaa, zote zina kasoro.
 
Natafuta kitu ambacho hakina kasoro hapa duniani, kitu kikamilifu kwa 100% kitu ambacho huwezi kukuta mawaa ndani yake...
Je, mapungufu yana upungufu katika upungufu wake? Kwa sababu mapungufu hayajakamilika?

Hivyo, je, kwa kuwa hayajakamilika katika kukamilika, yamekamilika katika upungufu wake?

Au, hayajakamilika hata kwenye upungufu, kwa kuwa yangekamilika kwenye upungufu yasingekuwapo na yasingejulikana kuwa ni mapungufu?

Ukifikiria sana utaona, kitu ambacho hakina mapungufu hakipo. Kipo, lakini, kuwapo kwake kuna maana hakipo.

Kitu hicho ni nothingness, nothingness ni kutokuwepo chochote, hata vacuum in space si nothingness, kwa sababu ina space. Nothingness yenyewe hata space haina. Haina space, haipo kwenye time. Haipo. Inafikirika tu.

Hiyo nothingness haipo. Kwa kuwa kuwapo kwake ni kutokuwapo.Ikiweza kuwapo nje ya hapo tu, inakuwa si nothingness tena.

Hiyo dhana ya nothingness, kinadharia, ndiyo haina makosa. Kwa sababu ina lowet entropy, hauwezi kupunguza entropy hapo. Huwezi kuharibu, ili uharibu, inabidi uitoe kwenye nothingness.

Hiyo nothingness ndiyo haina mapungufu.

Kitabu cha kusoma ni "Why Does The World Exist: An Existential Detective Story" cha Jim Holt.
 
Hakuna kasoro katika kuokoka, kuamin Yesu Kristo aliyemwokozi wako, kuliamin jina na damu take.

Ni kasoro sana kumwamin Kristo bila kuokaka.
Ni kasoro kumwamin Yesu Kristo bila kuliamin jina na damu yake.

Happy dominika kwa wote
 
Hakuna kasoro katika kuokaka, kuamin ni Yesu Kristo aliyemwokozi wako, kuliamin jina na damu take.

Ni kasoro sana kumwamin Kristi bila kuokaka.
Ni kasoro kumwamin Yesu Kristo bila kuliamin jina na damu yake.

Happy dominika kwa wote
Yesu ana kasoro.

Aliwachia nguruwe wasio na kosa waangukie ziwani na kufa.

Angekuwa anaishi leo watu wa PETA (People for the Ethical Treatment of Animals) wangemshitaki kwa ukatili wake dhidi ya wanyama.
 
Upungufu ni mtazamo wako ,wengine upungufu kwao ni neema na si mapungufu.

Kuna mdau amesema udongo/ardhi hauna mapungufu - Udongo upo wa aina nyingi kuna tifutifu ,mfinyazi ,kichanga etc kwa wengine waliopo kwenye udongo mfinyazi watakwambia una mapungufu kwasababu kipindi cha mvua ni majanga na pia hauwezi kupanda mihogo ila mtu wa sanaa za kutengeneza vyungu vya maua /majiko etc kwake si mapungufu bali ni neema , udongo wa kichanga kwa wenye sector ya ujenzi ni neema ila wachimba vyoo kwao ni mapungufu maana ukichimba vibaya unaweza kujizika mwenyewe.
 
Back
Top Bottom