Je, ni kweli Adhabu ya Viboko inasaidia kuongeza Nidhamu na Uelewa kwa Mtoto?

Je, ni kweli Adhabu ya Viboko inasaidia kuongeza Nidhamu na Uelewa kwa Mtoto?

Bila viboko kutakua na ongezeko kubwa la mashoga mtoto lazima aonywe kwa fimbo kiasi
Wee huwa huna hoja ya maana, kuna shoga alikupurura pesa na kizibo hakukupa why so uko bitter kwao. Poleeeee
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Adhabu ya viboko kwa mtoto ni akizo la Mungu mwenye akili kuliko tunaojadili.

Lengo la Viboko ni kuondoa ujinga kichwani. Hapa inamaanisha mambo ambayo mtoto anafanya kusudi ambayo akiendelea atakuwa sugu.

Kwenye mambo mengine mfano mtoto kakosea jibu kwa sababu mwalimu haeleweki, au kavunja sahani moja wakati mwaka mzima havunji hapo kiboko hakimsaidiii na ni makosa kumchapa.

Ni hayo tu.
 
Kwa maoni yangu viboko viendelee kuwepo ila KWA KIASI si KWA KUTESA yaani mwalimu asichape kwa kutumia HASIRA bali Kwa KUONYA kwa sababu muda ambao mzazi hayupo na mtoto shuleni mwalimu ndo anabeba jukumu la malezi.

Lakini hata maandiko ya BIBLIA yanakazia kuhusu hilo

1. MITHALI 22:15
Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto lakini fimbo ya Adhabu itaifukuzia mbali.

2. MITHALI 23:13
Usimnyime mtoto wako mapigo maana ukimpiga kwa fimbo hatokufa.

3. MITHALI 22:6
Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atapokuwa mzee.

Over.
 
Kuna changamoto katika uekelezaji wa utoaji wa adhabu mashuleni, kwa mfano sheria inamtaka kabla mwalimu hajatoa adhabu, lazima apate kibali kutoka kwa mkuu wa shule, lakini pia na idadi ya viboko anayotakiwa kuchapwa mwanafunzi ni viboko vinne.

Lakini kuna baadhi ya walimu wachache hawafuati taratibu hizo, naiomba Serikali itoe tamko rasmi kwa walimu wote nchini juu ya wao kufuata sheria za utoaji adhabu kwa wanafunzi
Serikali ndiyo chanzo /kisababishi no.1 cha kuporomoka kwa maadili hapa nchini.
 
Miaka ya mwanzoni mwa 1990, Shule niliyosoma Sekondari alikuja Mwalimu kutoka Swedish Volunteers Service (SVS) na alikaa miaka miwili. Alikuwa akipinga sana sisi kuchapwa viboko. Alikuwa anatwambia sisi wanafunzi pamoja na walimu wenzake kwamba viboko kwa mwanafunzi ni vibaya na blah, blah, blah zingine. Kipindi hicho alikuwa haingii zamu na shule ilikuwa ya bweni na kutwa halafu kutwa ni mchanganyiko!🤪🤪🤪

Sasa bwana, walimu wazawa wakakaa kikao chao wakaona na yeye apewe zamu ya wiki nzima!!! Siku ya Kwanza ikapita. Ya pili. Unaambiwa siku ya tatu walimu wakiwa kwenye mapumziko ya chai staff, Volunteer akasemaje, "I think, it's not bad to cane a student a little......! Ahahahahaha!!!
 
Kabla ya kuanza kuongelea kufuta adhabu ya viboko tuanze kuangalia zamani ambalo viboko shuleni ilikuwa lazima, maadili yalikuwaje?
Maadili yalikuwa mazuri kwa sababu ukichapwa shuleni utahakikisha taarifa hazifiki nyumbani kwani zikifika lazima utapata adhabu kubwa zaidi.
Lakini tuangalie maadili ya Sas yakoje, wazazi wengi hawalei watoto wao na badala yake wajibu huo wameachiwa wasaidizi wa nyumbani.
Matokeo yake watoto hata wakikatazwa kufanya kitu hawataki, hawaheshimu watu wazima wasio wazazi wao lakini unataka watoto wako wakienda shuleni wawafanyie walimu Kama wanavyowafanyia wasaidizi wa nyumbani.
Lakini tunapiga kelele adhabu za viboko zifutwe je tumeshaenda kwenye vyuo vinavyoandaa walimu na kuwafundisha njia mbadala ya kuwadhibu wanafunzi bila kutumia viboko?
Jibu ni hapana hivyo badala ya kuwaambia serikali wafute viboko no afadhali waende kwenye vyuo vya ualimu na kuwafundisha mbinu mbadala ya kudeal na wanafunzi wakorofi
 
Watoto wafundishwe ukakamavu mashuleni na swala la Lishe bora mashuleni Serikali iwajibike pia Michezo irudi kama zamani.

Mboko kuchimba mashimo kama kawa! Wale Walimu wavaa KOMBATI mashuleni warudishwe.

Fedha za mavietii zimwagwe Wizara ya Elimu kuongeza bajeti ya Elimu. Walimu waheshimike kama zama za Mwalimu.

Kibaha Elimu SUPPLY irudi kama zama za Mchonga.
Hii ndio product na akili ya mtu aliyechapwa viboko na kuwa treated kama ng'ombe asiyejitambua. Unatema pumba bila kujitambua!

Watu kama wewe ndio utakuta na utu uzima wako unalala chini ili upigwe bakora na kiongozi mkubwa, kizazi bogus kabisa. Pathetic.
 
Mtoto wa Tz akinyimwa fimbo ni bomu.
Well, kitu kizuri ni mtoto wa Tanzania hajanyimwa fimbo! Je mpaka leo mtoto wa Tanzania na nchi imefaidika vipi na matumizi ya viboko?

Hivi mnafikiria kweli kabla ya kuandika? Au wewe ndio faida ya viboko? Kutokujitambua?
 
Serikali ndiyo iliyoanza kuvuruga maadili kwa kuruhusu uwepo wa mashirika ya kijinga ya utetezi wa haki za watoto, wanawake, vijana/mtoto wa kike,mashoga n.k, baadhi yakijificha nyuma ya mgongo wa dini na mengine kwenye siasa.
2/. Serikali kuingiza siasa kwenye malezi -kifamilia/kijamii mpaka shuleni na kuwajaza watoto wetu ujinga kuwa wakichapwa wakimbilie polisi kumshitaki mzazi/mlezi, hivyo imepora mamlaka ya malezi.
3/.Zamani ualimu ulikuwa ni wito [kipindi cha walimu wa UPE ]na moja ya vigezo vya kuwa mwalimu, ulikuwa ni nidhamu/maadili mema,siku hizi hakuna hiyo,na sasa waalimu wengi wana shida ya kimaadili,hawana sifa/vigezo vya kuwa walezi.
4/. Wazazi/walezi wengi wameiga malezi ya kizingu ya kuwadekeza watoto na baadhi huwaogopa watoto wao kiasi cha kushindwa hata kuwakaripia.
 
Nimesoma ila sijamaliza sababu nimeona wahusika wanajadili vipigo na sio viboko mashuleni.

Kuna tofauti kubwa kati ya kumchapa mtoto viboko na kumpa kipigo.

Viboko havina historia ya kuua mtoto especially haya matoto majeuri yasiyokwenda bila bakora.

Bakora ni tiba ya akili ya kumpa mtoto ukumbusho na mipaka kuwa akirudia yale ambayo amekatazwa na kupigwa marufuku basi yale maumivu aliyopata atapata tena.

Bakora ni sehemu ya matokeo ya utomvu wa nidhamu na zinatolewa kama namna ya kumtia adabu mtoto mkaidi asiyeshika mafunzo ya adabu na utaratibu.

Miaka yote viboko havikuwahi kuwa tatizo ila miaka hii ndipo vimekuwa tatizo?

Halafu iweje maswala ya watoto wetu wazungu ndio waje kutushauri namna ya kuwalea wao umewaona watoto wao namna wanawalea?

Matoto yao ni majeuri yanajiamulia yanachotaka na anaweza kumjibu mzazi kama mtoto mdogo kwa kufokea, je ndipo huko mnataka tuelekee?

Nadhani mnachotafuta sasa ni kutukosea adabu kama Jamii ya watanzania na waafrika kwa ujumla, hizo elimu za darasani mlizopewa zisiwatoe kwenye uhalisia wa tamaduni zetu za kiafrika.

Watoto wetu tunaendelea kuwatandika bakora popote watakaopokosea adabu ambacho kinatakiwa kukemewa ni vipigo kwa watoto ila sio adhabu ya viboko kuondolewa.
 
Mboko zikizidi sana kwa mtoto husababisha hofu, kutojiamini, Usugu/ununda kwa mtoto. Mboko iwe kiasi, mzazi usichoke kusema na mtoto mfanye kuwa rafiki. Unapomchapa sana utatengeneza kiambaza baina yako na yeye.
Hiyo kazi waachie walimu wa discipline wao ndio wanajua namna ya kudeal na matoto matukutu hadi yanakuja kunyooka.

Hebu msiingilie kazi ya malezi ndio maana siku hizi matoto yenu adabu zero.
 
Nina imani unaongelea Bakora na Nidhamu badala ya Bakora na Akili au Uelewa.

Adhabu ya viboko kamwe haikusaidia, haitosaidia na haisaidii kujenga nidhamu ya mtoto.

Kwanini?
Ukiangalia muda ambao adhabu ya viboko imekuwa ikitumika kwenye shule za serikali. Utagundua maadili duni yapo na yalikuwa palepale tangu enzi inzo.

Mimba za utotoni.
Ujinga.
Ufaulu duni.
Matumizi ya madawa, bangi na pombe.
Ujeuri.
Lugha mbovu, or just matusi.
Ngono zembe.
Magonjwa ya ngono.
Mavazi ya uchi. Etcetera.

Naweza kulist tabia za utomvu wa nidhamu siku nzima na nisifike mwisho.

Simply sababu nidhamu haijengwi na shule wala taifa. Bali mtu binafsi. Ninaposema mtu binafsi namaanisha na mtoto vilevile. Sababu kuna watu wanadhani Mtu Binafsi ni mpaka awe analipwa mshahara.
Na "utu" binafsi wa mtu hujengwa na watu wa karibu. Wazazi.
Wazazi ndio wanaamua na kuchangia mtoto wao aje kuwa mtu wa aina gani tangu siku anazaliwa kutokana na malezi na tabia zao, genetics zinachangia vilevile. Na mtoto atatoka na tabia alizopewa na Wazazi kwa miaka karibu 7 na kuja nazo shule. Baada ya saa 8, anarudi nyumbani kuziendeleza.

Wanaosema tabia ni kama ngozi wanamaanisha. Tabia za mtu ni sehemu ya utu wake, zipo wired kichwani kwake tangu amezaliwa. Maana yake kubadilisha tabia za mtu binafsi alizodevelop na kuwa nazo kwa zaidi ya miaka 7, simply physically kwa kutumia bakora ndani ya saa 8, ni haiwezekani hata iweje. It is impossible.

Bali utakachokuwa unafanya ni kumfanya a-adapt hiyo new life style ya bakora na kuendeleza hizo tabia zake kiumakini zaidi, ikichangiwa na ili kukuprove wrong. Simply anakukwepa tu, ukigeuza kisogo anarudi kwenye default settings zilizokomaa kwa zaidi ya miaka 7.

Hivyo kwa njia hiyo, mtoto aliyejifunza umalaya kutoka kwao, ataendelea kuwa malaya, mvuta bangi, na mjinga vilevile.
Simply ni kazi bure na kupoteza muda. Lakini even worse ni kufanya tabia hizo ziwe sugu.

Eidha mtoto ni mwenye nidhamu au hana nidhamu kutokana na wazazi. Na njia ya kumbadilisha mtoto mpaka ajenge tabia mpya zitachukua matumizi ya akili zaidi ili huyo mtoto aanze kujitambua na kukiuka ushawishi wa wazazi, jamii na mazingira, kitu ambacho ni too complex kwa walimu wa Tanzania waliokulia kwenye mazingira magumu, maisha duni na kuendelea kuishi maisha duni mpaka leo. Uwezo wa nchi yet na mazingira havisupport hiyo major change.

Hivyo simply, bakora hazijengi nidhamu, na kuziacha bila ya kuja na solution kutafanya tabia hizo kuwekwa hadharani tu na sio kwamba hazikuwepo.

Ukifikiria hili jambo kwa umakini na kwenda ndani zaidi utagundua kizazi kama kizazi kitaporomoka au kupanda kama an unstoppable chain reaction.

Conclusion ni kwamba watoto wenye nidhamu wataendelea kuwa na nidhamu na wasio na nidhamu basi wameshapotea.
 
Adhabu ya viboko inasaidia katika kumnyoosha mtoto.Ikifanywa kwa kaisi.Pia kuna umri mtoto akifikisha hasa akishabalehe adhabu ya viboko inabidi ipunguzwe au apewe adhabu mbadala kama kazi ngumu kidogo ambazo hazitamuathiri kiafya.Au kumnyima zawadi na kuwapatia wengine.
Lakini adhabu unapoitoa inatakiwa umuelekeze muonye kuwa atambue kosa alilolifanya na akiri kukosea na kuahidi kutorudia na afahamishwe ana adhibiwa kwa kosa gani na isiwe kosa la muda mrefu ,muda aliokosea aadhubiwe ndani ya muda.
Malezi ya watoto wetu wa kibongo bila adhabu mapigo wanakosa adabu tena kuna siku wanaweza kukuaibisha kwa watu kwa kumisbehave hata mbele za watu wengine na ikaonekana wamelelewa vibaya siku moja,tumeshashuhudia watoto wa dady ,mumy ,mabasi ya njano waliolelewa vobaya wanavyo misbehave jinsi wanavyoleta picha mbaya ya malezi mabaya waliyolelewa mbele za wageni .Mungu ametuagiza watoto wanapokosea tusiwanyime adhabu.Ila tuwaadhibu kwa haki,tusiwaadhibu kupita kiasi inakuwa ukatili dhidi ya watoto.Tusiwachokeze biblia inatuonya wazazi tusiwachokoze tusiwaonee watoto.
 
Back
Top Bottom