Nina imani unaongelea Bakora na Nidhamu badala ya Bakora na Akili au Uelewa.
Adhabu ya viboko kamwe haikusaidia, haitosaidia na haisaidii kujenga nidhamu ya mtoto.
Kwanini?
Ukiangalia muda ambao adhabu ya viboko imekuwa ikitumika kwenye shule za serikali. Utagundua maadili duni yapo na yalikuwa palepale tangu enzi inzo.
Mimba za utotoni.
Ujinga.
Ufaulu duni.
Matumizi ya madawa, bangi na pombe.
Ujeuri.
Lugha mbovu, or just matusi.
Ngono zembe.
Magonjwa ya ngono.
Mavazi ya uchi. Etcetera.
Naweza kulist tabia za utomvu wa nidhamu siku nzima na nisifike mwisho.
Simply sababu nidhamu haijengwi na shule wala taifa. Bali mtu binafsi. Ninaposema mtu binafsi namaanisha na mtoto vilevile. Sababu kuna watu wanadhani Mtu Binafsi ni mpaka awe analipwa mshahara.
Na "utu" binafsi wa mtu hujengwa na watu wa karibu. Wazazi.
Wazazi ndio wanaamua na kuchangia mtoto wao aje kuwa mtu wa aina gani tangu siku anazaliwa kutokana na malezi na tabia zao, genetics zinachangia vilevile. Na mtoto atatoka na tabia alizopewa na Wazazi kwa miaka karibu 7 na kuja nazo shule. Baada ya saa 8, anarudi nyumbani kuziendeleza.
Wanaosema tabia ni kama ngozi wanamaanisha. Tabia za mtu ni sehemu ya utu wake, zipo wired kichwani kwake tangu amezaliwa. Maana yake kubadilisha tabia za mtu binafsi alizodevelop na kuwa nazo kwa zaidi ya miaka 7, simply physically kwa kutumia bakora ndani ya saa 8, ni haiwezekani hata iweje. It is impossible.
Bali utakachokuwa unafanya ni kumfanya a-adapt hiyo new life style ya bakora na kuendeleza hizo tabia zake kiumakini zaidi, ikichangiwa na ili kukuprove wrong. Simply anakukwepa tu, ukigeuza kisogo anarudi kwenye default settings zilizokomaa kwa zaidi ya miaka 7.
Hivyo kwa njia hiyo, mtoto aliyejifunza umalaya kutoka kwao, ataendelea kuwa malaya, mvuta bangi, na mjinga vilevile.
Simply ni kazi bure na kupoteza muda. Lakini even worse ni kufanya tabia hizo ziwe sugu.
Eidha mtoto ni mwenye nidhamu au hana nidhamu kutokana na wazazi. Na njia ya kumbadilisha mtoto mpaka ajenge tabia mpya zitachukua matumizi ya akili zaidi ili huyo mtoto aanze kujitambua na kukiuka ushawishi wa wazazi, jamii na mazingira, kitu ambacho ni too complex kwa walimu wa Tanzania waliokulia kwenye mazingira magumu, maisha duni na kuendelea kuishi maisha duni mpaka leo. Uwezo wa nchi yet na mazingira havisupport hiyo major change.
Hivyo simply, bakora hazijengi nidhamu, na kuziacha bila ya kuja na solution kutafanya tabia hizo kuwekwa hadharani tu na sio kwamba hazikuwepo.
Ukifikiria hili jambo kwa umakini na kwenda ndani zaidi utagundua kizazi kama kizazi kitaporomoka au kupanda kama an unstoppable chain reaction.
Conclusion ni kwamba watoto wenye nidhamu wataendelea kuwa na nidhamu na wasio na nidhamu basi wameshapotea.