Wanabodi
Niko hapa Serena, kwenye mjadala wa kujadilli ubinafshaji wa Bandari, kwa kampuni ya DPW ya mwarabu wa Dubai. Bunge letu tukufu, limeelezwa ni Bunge dhaifu, na pia ni Bunge kibogoyo!. Hoja hiyo imetolewa na Mwanahabari ghuli, Jenerali Ulimwengu katika mjadala huu, swali langu ni Je ni kweli Bunge letu ni dhaifu?. Je ni kweli Bunge letu ni Bunge kibogoyo?.
Kwa vile mjadala huu uko live online,
nakutafutia video ili uweze kumsikia wewe mwenyewe, kwanini Jenerali Ulimwengu ameliita hivi hili Bunge letu tukufu kuwa ni dhaifu na kibogoyo?
Jenerali Ulimwengu alimalizia kwa kumpongeza Rais Samia, akifanya vizuri tumpogeze, akikosea tumkosoe, ila pia amempa angalizo Rais Samia, akemee wanaojiita chawa wa Mama, haipendezi Rais Wetu kuwa na chawa!.
Paskali