Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?

Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?

Waliotuvusha na kukamilisha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa mhusika rasmi kwa mujibu wa katiba bila shaka wanaona na watatuvusha tena ktk hili maana ndo watetezi wetu sisi wananchi na mipaka yetu.
 
Hakuna bunge mule

Wabunge wengi ni vilaza tu

Kuna wabunge sijui kama hata

Wanaweza kusoma makikataba na hayo mavitabu wanayopewa humo
Ndani

Ova
 
Wanabodi

Niko hapa ukumbi wa hoteli ya Serena, jinini Dar es Salaam, kwenye mjadala wa kujadilli ubinafshaji wa Bandari, kwa kampuni ya DPW ya mwarabu wa Dubai, ulioandaliwa na taasisi mpya kabisa ya habari inayoitwa MB (Media Brains), inayoundwa na Manguli wabobezi na wabobevu wa habari nchini Tanzania, Jesse Kwayu, Absalom Kibanda, Dennis Msaki na Neville Meena.

Kwenye mjadala huo, Bunge letu tukufu, limeelezwa kuwa ni Bunge dhaifu, na Bunge kibogoyo!. Hoja hiyo imetolewa na Mwanahabari ghuli, Jenerali Ulimwengu katika mjadala huu,
Na kwa vile mjadala huu ulikuwa live online, unaweza kuufuatilia hapa

Natumaini unaweza kumsikia wewe mwenyewe, kwanini Jenerali Ulimwengu ameliita hivi hili Bunge letu tukufu kuwa ni dhaifu na kibogoyo, swali langu ninalo uliza hapa ni Je ni kweli Bunge letu ni dhaifu na Bunge kibogoyo?. Hoja za Jenerali Ulimwengu zina ukweli wowote?.

Jenerali Ulimwengu alimalizia kwa kumpongeza Rais Samia kwa mambo mazuri anayoyafanya na kusisitiza, Rais Samia akifanya vizuri tumpogeze, akikosea tumkosoe, ila pia amempa angalizo Rais Samia, akemee wanaojiita chawa wa Mama, haipendezi Rais Wetu kuwa na chawa!.

Paskali
Ninavyofahamu Tanzania hutuna bunge kwa sasa.
Kilichopo ni mkutano maalumu wa ccm kujimilikisha kivuli cha bunge kwa nia ya kulamba mishahara minono na posho kede kede.
Genge hili linachota kiasi kikubwa cha pesa ya mlipa kodi kuliko genge jingine lolote nchini.
 
Pascal Mayalla

Ungana na wananchi wenyewe kupinga kubinafisishwa bandari zetu kwa mkataba wa milele

Achana na kina msukuma
Mkuu Kisamv , mnachohitaji ni kuelimishwa tuu kuhusu mikataba, hakuna mkataba wa milele hapa duniani!.
Ile IGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkataba ni HGA, utakuwa na time frame ya duration.
P
 
Mkuu Utingo , huku kuuliza kama tuna Bunge ni kuuliza gani wakati ni ukweli tuna Bunge?, lipo, tunaliona, linakutana, unapouliza kama tuna Bunge, unamaanisha nini?
P
ndiyo sababu nikasema "tuanzie hapo". Nawe umeanza vizuri....Mimi na wewe tujiulize.....wabunge hawa wanaounda bunge la sasa ni wabunge waliochaguliwa na wananchi kwa uhalali, kwa kura isiyo na mizengwe? Wao wenyewe wana ujasiri wa kutokea wakajigamba kuwa walichaguliwa na wananchi kwa 100% na hawakupata ubunge kwa nguvu ya dola au nguvu na utashi wa rais wa wakati ule? Je mbunge anayepatikana namna hiyo, yuko bungeni kutetea maslahi ya nani...aliyemuweka au mwananchi?
 
Humu ndani tuna two types of people, wishful thinkers na realists, wishful thinkers wao kazi yao ni ku wish tuu, hata kitu kiwepo physically na wanakiona kwa macho yao, wataji please hakipo!. Ma realist ni watu wanaukubali ukweli, hata kama hukubaliani nao ni ukweli na upo.

Bunge lipo, lina exist in reality, huwezi kuuliza kama Bunge lipo!.
P
 
Bunge hili sijawahi ona wakipinga mswada wowote
Miswada mingi wao nikuipitisha kwa kugonga meza tu kwakwakwa
Lile bunge ni sawa na kijiwe tu cha kukutana watu tu

Ova
 
Humu ndani tuna two types of people, wishful thinkers na realists, wishful thinkers wao kazi yao ni ku wish tuu, hata kitu kiwepo physically na wanakiona kwa macho yao, wataji please hakipo!. Ma realist ni watu wanaukubali ukweli, hata kama hukubaliani nao ni ukweli na upo.

Bunge lipo, lina exist in reality, huwezi kuuliza kama Bunge lipo!.
P
you are very very wrong. idealists ndiyo ninyi mnaoshabikia hilo bunge lililopatikana kwa mizengwe na dhuluma kubwa. na ccm wengi ni idealists mabingwa wa propaganda tu. you are always afraid of reality and truth.

Ni kama sasa kwa mfano (ni mfano tu) ccm wengi hawakubali kuwa kuna mambo ya kurekebishwa kwenye mkataba wa bandari ili uendane hata na sheria zetu-because they are just idealists kila kitu wanameza tu to please their idealistic mentality. But realists wanaona miaka mingi ijayo mkataba huu usipofanyiwa marekebisho unaweza kuleta shida za kufikishana hata kwenye vyombo vya usuluhishi na ukadumaza hata utendaji wa bandari kuliko ilivyo hivi sasa.

Realists always stands on the truth, purity and sustainability unlike idealists who stand on deception and they always don't care about the future as long as their short term agenda is met.
 
Mkuu Pascal asante kwa kueleza kuwa kichaa sio lazima aokote makopo ( kwa maana hiyo tuna wabunge wengi ambao ni vichaa!). Sasa kama hawaokoti makopo na ni vichaa hapo tunakuwa wishful thinkers au realists? Kwa mtizamo huo huo ni sawa nikisema bunge halipo ( kimaumbile lipo ila kiutendaji kwa mujibu ya katiba halitekelezi hivyo ni sawa na kusema halipo). Bunge linapokuwa ni rubber stamp ya serikali, mtu akisema hatuna bunge kwanini tuone hayupo sawa?
Maisha sio kile tu macho yanachoona (vingine vipo vinaishi ila macho hayavioni)NB: kama unavyosema yupo kwa Baba anapumzika, ndivyo wengine wameona na kusikia usichokiona na kukisukia wewe! Wasema wajapo hawa udhaifu wa aina hii hujirudia hivyo wakisema hawa ni dhaifu (lugha ambayo hata mimi siipendi), tunapaswa kutafakari sana hisi zao kuliko kusema wasiseme hivyo. Hili haliwezi kutusaidia sana zaidi tu kutugawa...
Asante.
 
you are very very wrong. idealists ndiyo ninyi mnaoshabikia hilo bunge lililopatikana kwa mizengwe na dhuluma kubwa. na ccm wengi ni idealists mabingwa wa propaganda tu. you are always afraid of reality and truth.

Ni kama sasa kwa mfano (ni mfano tu) ccm wengi hawakubali kuwa kuna mambo ya kurekebishwa kwenye mkataba wa bandari ili uendane hata na sheria zetu-because they are just idealists kila kitu wanameza tu to please their idealistic mentality. But realists wanaona miaka mingi ijayo mkataba huu usipofanyiwa marekebisho unaweza kuleta shida za kufikishana hata kwenye vyombo vya usuluhishi na ukadumaza hata utendaji wa bandari kuliko ilivyo hivi sasa.

Realists always stands on the truth, purity and sustainability unlike idealists who stand on deception and they always don't care about the future as long as their short term agenda is met.
Absolute true. Kwa realist gani akubali kuwa bunge hili lililopeleka wabunge Dubai kuona hao DPW walivyo linafanya hayo kwa maslahi ya watanzania ambao mpaka sasa wengi wameonyesha kutokubaliana na hilo? Pascal huwa namuona ni aina ya watu watakao wanaposema jambo basi lazima uingie kwenye ufahamu wake, haoni kuishi hivyo ni ideal tu maana haiwezekani!
Kwenye hili realists wote wanauliza huku kwetu ni Rais na Waziri wake wameiwakilisha nchi, hiyo nchi nyingine imewakilishwa na nani? HAKUNA JIBU!
Realists tena wanauliza bandari ni suala la muungano, kwanini upande mmoja wa muungano haujahusishwa? HAKUNA MAJIBU!
Realists wanauliza haya makubaliano ni IGA, mnasema mikataba tendaji bado, tunauliza pale waziri asemapo mapato yatapanda toka trilioni 7hadi trilioni sijui 24 makadirio haya anayapata kwa hesabu gani wakati hakuna mikataba inayoonyesha faida itapatikanaje? HAKUNA MAJIBU
Bro Pascal plz, usiwe idealist katika hili tusijeanza kuwa na idea kuwa nawe ulikuwemo kwenye Ile trip.
 
Back
Top Bottom