Wanabodi
Niko hapa ukumbi wa hoteli ya Serena, jinini Dar es Salaam, kwenye mjadala wa kujadilli ubinafshaji wa Bandari, kwa kampuni ya DPW ya mwarabu wa Dubai, ulioandaliwa na taasisi mpya kabisa ya habari inayoitwa MB (Media Brains), inayoundwa na Manguli wabobezi na wabobevu wa habari nchini Tanzania, Jesse Kwayu, Absalom Kibanda, Dennis Msaki na Neville Meena.
Kwenye mjadala huo, Bunge letu tukufu, limeelezwa kuwa ni Bunge dhaifu, na Bunge kibogoyo!. Hoja hiyo imetolewa na Mwanahabari ghuli, Jenerali Ulimwengu katika mjadala huu,
Na kwa vile mjadala huu ulikuwa live online, unaweza kuufuatilia hapa
Natumaini unaweza kumsikia wewe mwenyewe, kwanini Jenerali Ulimwengu ameliita hivi hili Bunge letu tukufu kuwa ni dhaifu na kibogoyo, swali langu ninalo uliza hapa ni Je ni kweli Bunge letu ni dhaifu na Bunge kibogoyo?. Hoja za Jenerali Ulimwengu zina ukweli wowote?.
Jenerali Ulimwengu alimalizia kwa kumpongeza Rais Samia kwa mambo mazuri anayoyafanya na kusisitiza, Rais Samia akifanya vizuri tumpogeze, akikosea tumkosoe, ila pia amempa angalizo Rais Samia, akemee wanaojiita chawa wa Mama, haipendezi Rais Wetu kuwa na chawa!.
Paskali