Je, ni kweli hii inapunguza gharama za ujenzi?

Je, ni kweli hii inapunguza gharama za ujenzi?

SIKILIZA NIKUAMBIE KITU...amini nakwambia huwezi pata hili kirahisi...wafanya biashara wa tofali huweka ratio ndogo kwa idadi ya tofali ili wapate faida....wasipokupunja kwenye inches za tofali watakupunja kwenye uwiano wa cement na mchanga au ubora wa mchanga....Faida utakayoipata
1.kama unajua mambo ya ujenzi na ubora wa mchanga unaootaka kutumia ukisimamia kuupata huo umepata faida ya kwanza
2.tofali hizo ni nyingi sana kama una mda wa kusimamia na kufanya manunuzi mwenyewe unaweza kupata ile free delivery ya cement or discount
3.kama unaweza kusimamia vizuri tenga muda hasaa maana hutakuwa na mashine ya kuchanganya...usikubali mafundi wakuambie tunapiga mifuko kadhaa kwa siku..maana jinsi mda unavyokwenda ndivyo wanavyochoka kuchanganya kunauwezekano wa kulipua kazi na kupata tofali za hovyo kabisa(cha kufanya tafuta mafundi wengi wape wastani wa tofali kwa siku na baada ya siku tatu wape mapumziko waje wakiwa fresh tena na maji uwe nayo ya kutosha)
4.faida nyingine utajua vitu vingi kama una jicho la tatu la kujiongeza
5.kama hela ni ya kuungaunga ni njia nzuri ya kufanikisha kwa urahisi.
Asante kwa maelezo haya mkuu.

Kusema ukweli nina uzoefu wa kujenga ila sijawahi kuwaza kuhusu ubora wa mchanga.Huwa naagiza tu gari fundi anajengea au kama tuko levo ya kupiga plasta fundi huwa anasema nikiagize niwaambie walete wa plasta.I gues nimekua nafanya mambo kienyeji.
Kwa hiyo mkuu mchanga bora ni upi?

Maji sio tatizo yapo uhakika na ninaamin nina jicho la tatu mpaka project iishe nitakua nimejifunza mengi mkuu.

Kwa faida ulizoainisha nashawishika kufyatua mwenyewe.
 
Una machine ya tofali?
Mchanga?
Cement za kutosha?
Umeme?
Maji yapo au ni ya kununua?
Mafundi unawalipaje?
Wabebaji je?
Ukijumlisha hizo gharama unakuta gharama inakuja pale pale bora ununue uokoe muda na gharama zaka
Machine nilitaka kukodesha ila nitanunua ili inifae wakati mwingine.

Mahitaji yote yapo na nina timu kubwa ya mafundi wazuri.

Asante kwa mchango wako mrembo😍
 
Kwa idadi hiyo ni kweli utaokoa gharama kubwa ya fedha, utapata ubora unaoutaka wa tofali. Mtaani watu wanafyatua hadi tofali 55-60 kwa mfuko mmoja. Ila wewe utaamua unatakaje, hata tofali 30 kwa mfuko, ni maamuzi yako na ubora unaotaka.
Ni kweli mkuu.

Hapa cha muhimu ni kutafuta muda niwe bega kwa bega mwanzo mwisho na pia niache hizi mvua zipite ndo mchakato uanze mana mvua inaweza kuharibu mambo.
 
Faida kubwa ni ubora wa tofali lakini pia kwa vile idadi ni kubwa ataokoa gharama kiasi, haya tunayonunua ukweli hamna kitu kabisa. Gharama ni maji, cement, umeme(kama atatumia machine za umeme) na makubaliano ya kufyatua.
Hivi zile machine za kawaida si zinaweza kufaa tu?

Vijana wa kufyatua wanalipwa kuanzia 5000 kwa mfuko
 
Kinachotakiwa ni usimamizi tu, maana hata hao mafundi wanaweza kuficha mifuko na kuiuza. Wadosi wanaweza kuuza hata mifuko 100 na asijue, uaminifu imekuwa lulu miaka hii, tofali 20,000 ni project kubwa hiyo.
Hapo kwenye kuibiwa niko makini nawajua hawaambuliagi kitu.
Niko makini vibaya sana mkuu.
Mafundi usipowajua wanakuumiza
 
Wewe umepiga hesabu umeona kabisa unaona 40% unaokoa sasa unauliza nn

Na kwakukuongezea tu ukifyatua mwenyewe utazingatia ubora na utamwagia maji kwa kiwango
 
Hapo kama una machine na hizo materials nyingine basi umewin fyatua za kutosha ugawie hadi majirani ☺
Itakua hivyo.

Zikibaki bora nikuite uje wewe ubebe 😁 nikigawia majiran nitazid kujiponza coz hapa tu washaanza kunijia na maombi niwaletee usafiri na kuwakwangulia barabara na sijui nani kawadanganya nina uwezo huo maskin ya Mungu ila InshAllah one day yes Mungu ni wetu sote
 
Itakua hivyo.

Zikibaki bora nikuite uje wewe ubebe 😁 nikigawia majiran nitazid kujiponza coz hapa tu washaanza kunijia na maombi niwaletee usafiri na kuwakwangulia barabara na sijui kwanin wanahis nina uwezo huo maskin ya Mungu ila InshAllah one day yes Mungu ni wetu sote
Onhooo ila tofali zinatumika sehemu nyingi
Yakibaki utajengea kisima, ukuta mnara wa kuweka simtank n.k
Ila hata mimi nitayapokea kwa mikono miwili 😊
 
Ikiwa uko Dar. Tofali za inch 5 bei ni 1,100/=

UKINUNUA
Tofali inch 5 pc 20,000 @1,100 = 22,000,000/=

UKIFYATUA MWENYEWE
Kwa tofali 20,000 za inch 5 ratio ya 35 utahitaji mifuko 600 ya cement, mfuko mmoja ni 16,000
●600×16,000: 9,600,000

●Vibrator na mixer: 6,000,000/=

●Mafundi mifuko 600 @4000: 2,400,000/=

Hadi hapo tayari 18,000,000/=

Sijapiga hesabu ya mchanga, umeme, maji, vibao vya kufyatulia tofali, wapanga tofali (nguzo)

Kwa kifupi hamna utakachookoa.

Iko hivi wengi wanaamua kupiga tofali zao ili wapate ile ratio bora kabisa wanayoitaka kama ni hivyo fyatua mwenyewe. Ila kama ni hizi ratio za kawaida za viwanda vya tofali bora ukanunue
 
Ikiwa uko Dar. Tofali za inch 5 bei ni 1,100/=

UKINUNUA
Tofali inch 5 pc 20,000 @1,100 = 22,000,000/=

UKIFYATUA MWENYEWE
Kwa tofali 20,000 za inch 5 ratio ya 35 utahitaji mifuko 600 ya cement, mfuko mmoja ni 18,000
●600×18,000: 10,800,000

●Vibrator na mixer: 6,000,000/=

●Mafundi mifuko 600 @4000: 2,400,000/=

Hadi hapo tayari 19,200,000/=

Asante kwa mchanganuo mkuu.

Nilipo cement ni 16,000
Tofali ni 900 na usafiri inakua 1000.
Ratio ya tofali 40 kwa mfuko nadhani sio mbaya.
Sitatumia mixer na vibrator.Tutaenda manual.
Vijana huku wanalipwa hadi 4000 kwa mfuko kwa kazi kubwa
 
Asante kwa maelezo haya mkuu.

Kusema ukweli nina uzoefu wa kujenga ila sijawahi kuwaza kuhusu ubora wa mchanga.Huwa naagiza tu gari fundi anajengea au kama tuko levo ya kupiga plasta fundi huwa anasema nikiagize niwaambie walete wa plasta.I gues nimekua nafanya mambo kienyeji.
Kwa hiyo mkuu mchanga bora ni upi?

Maji sio tatizo yapo uhakika na ninaamin nina jicho la tatu mpaka project iishe nitakua nimejifunza mengi mkuu.

Kwa faida ulizoainisha nashawishika kufyatua mwenyewe.
mchanga bora ni ule usio na vumbi jingi au hauna vumbi la udongo kabisa unapatikana mtoni au kwenye vijito au clashing dust za kokoto ni bora sana kama utazipata kwa tofali ..mchanga bora kwa tofali ni ule wenye punje kubwa na uwe una dust kidogo upatikane mtoni sehemu ambazo hazina chumvi au magadi...huo ndio mchanga bora kwa tofali...
mchanga bora kwa plasta uwe laini au punje ndogo usiwe na vumbi la udongo kabisa kama ni wakuchimbwa uchimbwe kwenye ardhi isiyo na asili ya chumvi ama magadi...ni hayo tu wataongeza wengine...wajenzi ama wajuvi....
 
Ikiwa uko Dar. Tofali za inch 5 bei ni 1,100/=

UKINUNUA
Tofali inch 5 pc 20,000 @1,100 = 22,000,000/=

UKIFYATUA MWENYEWE
Kwa tofali 20,000 za inch 5 ratio ya 35 utahitaji mifuko 600 ya cement, mfuko mmoja ni 18,000
●600×18,000: 10,800,000

●Vibrator na mixer: 6,000,000/=

●Mafundi mifuko 600 @4000: 2,400,000/=

Hadi hapo tayari 19,200,000/=

Sijapiga hesabu ya mchanga, umeme, maji, vibao vya kufyatulia tofali, wapanga tofali (nguzo)

Kwa kifupi hamna utakachookoa.

Iko hivi wengi wanaamua kupiga tofali zao ili wapate ile ratio bora kabisa wanayoitaka kama ni hivyo fyatua mwenyewe. Ila kama ni hizi ratio za kawaida za viwanda vya tofali bora ukanunue
Tofali imeshafika elfu 20 boss labda kama atanunua kiwandani moja kwa moja
 
Back
Top Bottom