Habari waheshimiwa.
Nina kaproject kanakohitaji kama tofali 20,000 hivi kakamilike.
So far nina tofali 3000 ila nimepiga hesabu nikaona zikizobakia nikifyatua mwenyewe nitaokoa kama 40% ya pesa ya kununulia ila mafundi wananikatisha tamaa kuwa nitapata hasara tu ni bora kununua.
Naomba kujua kama yupo aliyefanya hii kitu matokeo yalikuaje.
Natanguliza shhkrani🙏🙏
Habari!
Hapa vitu vingi vinategemeana/sehemu ulipo.
1: Je ubora wa tofali unazopata haulingani na ubora wa mradi wako?
Hili utaweza kulitatua kwa kusimamia wewe binafsi kwa ukaribu uliotukuka.
2: Unahitaji kuokoa pesa
Tafakari juu ya sehemu ulipo:
A: Gharama ya upatikanaji wa mafundi bora kwenye ufyatuaji.
B: Gharama ya upatikanaji wa mashine ya kufyatua au cha kufanana nacho.
C: Gharama ya maji
D: Gharama ya mchanga
E: Gharama ya cement ununuzi na kufikisha site/kama unaweza kupata kwa bei ya jumla pia
F: Gharama ya umeme/ukitumika.
G: Gharama ya wewe kufika eneo la tukio kama si sehemu unayoishi.
H: Gharama ya mlo wako kwa siku kama si nyumbani na itaongezeka kutoka kwenye ule wa kila siku.
I: Thamani ya uwepo wako muda wote/reflect kwenye pesa utakayoiokoa.
3: Tofali iliyotayari:
A: Ubora
B: Ununuzi +kupakia +kushusha+ usafiri
Jibu la mwisho ni: 3 - (1+2)