Je, ni kweli Idd Amini alikuwa shujaa wa Afrika, Nyerere alitumiwa na wazungu kumchafua?

Je, ni kweli Idd Amini alikuwa shujaa wa Afrika, Nyerere alitumiwa na wazungu kumchafua?

..Alivamia ardhi ya Tanganyika.

..kuna jamaa mmoja aliniambia Nyerere hakutaka vita ile.

..anadai kulikuwa na makamanda wa Jwtz ambao ambao walikuwa na hasira na walisisitiza lazima Amin afundishwe adabu.
Dah mwisho wa siku Kenya akatupiga bao....bila ile vita sisi ndo tungeongoza East afrika kiuchumi
 
Basketball 🏀
FB_IMG_1687018823454.jpg
 
Ukweli ni kwamba Idd Amini alikuwa na kukosi chake maalum walikuwa wakivaa nguo za vitenge. Uganda waliwaita ichitenge, walikuwa kama watu wasiojulikana, wakikufuata hurudi. Hata Kikwete alikuwa na watu hawa wakiongozwa na Ramadhani Igwondu aliyemteka na kumtoa kucha na meno Dr. Ulimboka.
Pia magufuli alikuwa na watu wa aina hii. magufuli ni Mtakatifu wa kina Kulwa Jilala na Sukuma gang wote.

Bunge lililopitisha mkataba wa DP World ni matokeo ya utawala mbovu wa kifashisti wa magufuli
Huna tofauti na mtu aliyejipiga kibao
 
Nyerere alitumiwa na Wazungu kumchafua Iddi?

Mengine yote ungeweza kudanganya kwa nia ya kumpamba. Ila hilo la mgongano wake na Mwalimu ungeacha.

Iddi Amini alikuwa na maneno ya hovyo na vitisho. Mwalimu alijitahidi sana kutomzingatia. Mpaka pale Iddi alipojitoa ufahamu kutaka kung'ang'ania eneo la nchi yetu kuwa eneo la Uganda.

Uvumilivu huo usingeuvumilia hata wewe.

Kama ni Wazungu walimtuma Mwalimu kumchafua Iddi, basi hata wakati wa Vita wangempa msaada wa kivita ili kumchakaza Iddi Amini. Badala yake, Iddi Amini ndiyo alipata msaada kutoka nchi wahisani wa Kiislamu (Libya).
Alichofanya Mwalimu ndicho anachofanya Zelesky pale Ukraine, mwanamme rijali huwez kudharauliwa na kuonewa kindezi hivyo pambana hata kama unayepambana naye ana nguvu kukuzidi., Akikupiga bomu unamtungua kwa manati.
 
Iddi amini lipindua inch, yeye akawa raisi,
sasa lkn kabla ya hapo kanisa la roma walikuwa wamejenga kanisa kubwa sasa uganda ili litumike kama kituo kikuu cha makanisa yote ya ukanda wa nchi za mashariki,
baada ya amini kuingia madarakani akachukua kanisa na kulifanya msikiti,
Kitendo kile kilikwenda kuharibu sana utaratibu wa roma,
wakaamua kuandaa mipango ya kumtoa amini madarakani,

Baada ya miaka 50 toka ile vita itokee shirika la ujasusi la marekani litaweka wazi sababu za vita vile

Shirika la ujasusi la marekani huweka hadharani mambo yao kila baada ya miaka 50 toka wafanye jambo,

Kuna mambo meengi sana yapo nyuma ya pazia yamefanywa na marekani kuanzia nani atawale wapi na nani afanye nn
Nitumie hiyo documents ya CIA
 
Nyerere hakupaswa kumruhusu Obote kuishi Tanzania na kuwa na jeshi, sidhani kama ni makosa kusema Nyerere ndio alimchokoza Amin.

Amin kuvamia kagera ni kwamba alitaka kuwa na buffer zone ili majeshi ya Obote yasikanyage ardhi ya Uganda.

Ni kama majeshi ya China yalivyoanza kuisadia Korea kaskazini ili majeshi ya marekani yasikaribie mpaka wa China.
 
Hakuna makubaliano ya jumla juu ya Idd Amin Dada kuwa shujaa wa Afrika. Idd Amin Dada alikuwa rais wa Uganda kuanzia mwaka 1971 hadi 1979, na utawala wake ulijulikana kwa ukatili, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, na ukandamizaji wa kisiasa. Amin alitekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya makabila mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Wachagga, Wahima, na Wanubi, na watu wengi waliteswa, waliuawa au kukamatwa kiholela wakati wa utawala wake.

Ingawa Amin alijitangaza kama mtetezi wa Afrika dhidi ya ukoloni na alifanya hatua kadhaa za sera za Pan-Afrika, kama vile kuwaondoa wanajeshi wa Israel kutoka Uganda, vitendo vyake vilisababisha athari mbaya kwa watu wa Uganda na eneo zima. Amin aliathiri vibaya uchumi wa Uganda, alisababisha kuhama kwa maelfu ya raia na kuchangia katika kuvurugika kwa utulivu wa eneo hilo.

Kwa hivyo, wakati kuna wale ambao wanaweza kuona Amin kama shujaa wa Afrika kutokana na hatua yake dhidi ya ukoloni, athari mbaya za utawala wake kwa watu wa Uganda na eneo zima hufanya wengi kuona Amin kama dikteta mkatili na kiongozi ambaye alikiuka haki za binadamu. Kwa ujumla, maoni juu ya Amin ni tata na hutofautiana sana.
 
Back
Top Bottom