Je, ni kweli kuna majini?

Napataje icho kitabu Cha Tobiti nikipitie.....
 
Wapo sikuhizi wamewekewa sheria wasikutane na binadamu sana, ukiwataka wanauzwa zanzibar ila rule namba moja usimwogope atakuendesha wewe
 
Wanaoishi mikoa ya pwani huenda wanamajibu pia
 
Hii Dunia ina Mambo....Aiseeh...!
 
Igweeeeeeeee..!! 😻
 
Kwa imani na vitabu ndio yapo mazuri na mabaya. Viumbe vya Allah na nasikia ni wengi kuliko sisi bin adam
 
Kisayansi hakuna majini kiimani yapo so inategemea na wwe upo kwenye mtazamo upi
 
raha ya jin akuchunuku mwenyewe
Nilisoma shule ya Bweni , Mara nyingi tulikuwa tunajisomea usiku ,kuna siku tukitoka darasani usiku tukiwa na rafiki yangu tumefika mpaka maeneo ya Bweni tunapolala , ghafla jamaa naona kasimama namwambia vipi huingii ndani kimya haongei kitu , niliona anatimua mbio huku akisema leo utaona, na Mimi ikabidi nimfatilie maana anapokimbilia ni gizani kwenye mto alafu kuna miembe mingi sana tuko wawili tu ,hatimae nikamkamata namwambia vipi umekuaje turudi bwenini jamaa anagomba hata vitu sivielewi , kitu nachokumbuka aliniambia unanishika una nguvu kuliko Mimi hapo halo nikapata ufahamu huenda huyu jamaa siyo yeye nikamjibu hapana lakini wewe ni rafiki yangu siwezi kukuacha peke yako huku mbali alafu giza turudi bwenini basi akanielewa tukarudi kumbe jamaa siyo yeye pale njia nzima anagomba tu baadae tulipofika bwenini niliamsha wenzangu nakumbuka kuna madogo Fulani tokea Tanga, waliamka fasta wakaenda jikoni wakaja na moto kwenye kibati wakatoa Ubani wakachoma huku mmoja akimfunika jamaa na shuka safi nyeupe ndiyo Mara ya kwanza kuona mtu kapandisha jini jamaa aliongea sana kumbe kuna wachawi uwa wanakuja pale shuleni kusumbua wanafunzi , mikutano yao uifanyia maeneo ya miembe mingi mtoni kumbe wakati anakimbia alikuwa anakimbiza mchawi aliyekuja kusumbua wanafunzi bwenini, sasa ajabu yote jamaa aliyokuwa anasema kumbe siyo yeye baadae yule mwamba nakumbuka aliaga ndiyo jamaa akarudia hali yake yaani hata haelewi ndiyo wale madogo kumuelezea yote yaliyotokea...kuna visa nimekutana navyo sana shule ya Bweni kuna jamaa mwingine tulipomaliza shule yeye alienda kusomea ufundi pale pale Tanga lakini alikuwa kapanga ,tulipotezana muda nilipokutana naye wakati fulani ni mtu mwenye upweke mwingi tuliongea mambo mengi ya maisha lakini yeye bado alikuwa hajapata familia nikamuuliza vipi kulikoni mpaka sasa ndiyo akanieleza kuna jini limempenda ndiyo anatimiza haja zake hapo nilistaajabu sana, na kweli jamaa hakuwahi kuwa na rafiki wa kike kwa maana ya mahusiano maana kwa ule umri wetu vijana wote mashababi walikuwa moto kweli siku hizo,usipotembelewa na mabint mtaani utaoneka wewe siyo basi sababu ya maisha tuliachana niliwahi muulizia kipindi fulani nikaambiwa alipata familia lakini mkewe waliachana wakiwa na watoto 2.
 
interesting, mimi nilikua naona tu watu wanapandisha majini wanaongea hovyo wanagaragara nikawa nainjoi siku moja Mr wangu alitoka mihangaikoni nakumbuka ilikua usiku mida ya saa tatu naangalia movie, amerudi amekula tumekaa sasa tunaulizana hbar zakushinda na watoto ghafla ananambia mke wangu leo nimepandisha majini sjui yametokea wapi mm skuchukulia serious nikamjibu wewe na majini wapi na wapi, mwenzetu yameanza lini, ghafla akalala chini akawa n kama anajigeuza geuza mimi nikajua leo tuko location siko serious kabisa namwambia ukimaliza kugaragara hapo ukaoge ukalale naona sikuelew, akaigeukia macho ameyakunja ananambia wanataka kumdhuru kiti hawawe na hawatoweza, nasema hawawezi huku akichanganya na kimasai sasa hapa ndio alinishtua nikasimama naita husband husband akanigeukia niliposimama hapo sasa akili ikanambia huyo si mwenzio kuna mwenzie ndio yupp kichwan be clam and strong nikawa namuuliza nani anataka kumdhuru kiti amemkosea nn akacheka huku anaongea kimasai na mm na mume wangu sio wamasai wala lugha hiyo hatuijui nikamwambia sasa unaniongelea kimasai mm sielew ongea lugha tuelewane nijue namsaidiaje akawa anang'ang'ania sofa nikana hapa ni kuwahi simu nitoke nje nijue nafanya nn kweli nikaiwah sim nikamruka had mlangoni nikatoka nje nikampigia sim mama yake mdogo hatukai naye mbali sana, kufika nikamweleza akaasema yuko wapi mie yuko happ sitting room, tukaingia akamkuta ameinama kama simba akaita jina akaitika akamuuliza una shida gan mara wamasai hao wamekuja juu tena anahangaika kama anataka kufunga rubega hivi mamdogo akasema kuna mtu anamjua tumpeleke akaseme naye tukabeba sio mbali mwendo wa mguu kufika tuliemfata kumuona naye akapandisha wakawa wanaongea kama watu wanaoambiana habar fulan mimi nikasema mngeongea lugha ambayo sote tutaielewa sisi hatujui hiyo lugha mnayoitumia ongeeni kiswahili bas ndio huyo tuliemfata akasema huyu amepanda n kweli kuna watu walikua wanamjaribu mumeo lakini wamefeli na kingine huyu amekuja kwa dharura anauliza ni kwa nn mkoba wa bibi yake mzaa mama aliefariki watoto wanauchezea wanatakiwa uwekwe juu sio chin sababu mwenyewe kishafariki wee mie naona haya ni mapya nikamgeukia mamdogo n kweli huo mkoba upo akasema ndio na kweli vitu vyake wanangu wanavichezea hatuon kama vina maana ikabidi tu twende kwa mamdogo nahuyo mkaka na mune wangu pamoja uke mkoba ukawekwa juu nikarud kwangu lakini nje kwangu kuna hii miembe ya kisasa akasimama hapo akaniambia mke wangu uko sehem salama huku anajipiga kifuani usijali hakuna atakayeweza kukudhuru sasa mm namuogopa namuuliza huyo anayeongea ni nani wewe au jini wako akaniambia mm nasema kwaniaba ya kiti nikajua huyu mnyama anaye bado mamdogo akamwambia safiri salama bas muache kiti alale ana watoto wadogo utamtesa mwenzie safiri huku anampiga piga mgongon kuingiandan nikahakikisha visu vyote mapanga nimeyaficha lakini nililala matumatu that day kuamia asbh namwelezea hajui hata kimoja zaidi ya kulalamika kichwa kinamuuma bas had leo hua namtania kwa hiyo nimeolewa na ww na jini wako tunacheeeka ila hakuwah kupandisha tena zaidi akilala usiku anashtuka anakaa kitandani mm nasema kumekucha bas namuuliza uko sawa namuita akiitika najua ni yeye yuko sawa nalala zangu akiamka asbh anakwambia kulikuja watu jana mmoja akataka kuingia sjajua n kina nan namwambia madhali hawakuingia yaache maisha yanaendelea.
 
Duuh ..
 
We ulisikia ukiwa na hamu ya kuwaona wanakuja tu pasipo shida inayowafanya waje binafsi nishakutana nalo kipindi nipo mdogo kama darasa la tatu tunaambiwa tuwaishule teacher mwenye zamu yake mkali nikampitia mchizi wangu tuakiwasha Kuwai shule alooh like jini nilikua nikilitazama sioni mwisho wake pia miguuni pake alikua na kwato tu siku iliyofuaata baada ya tukio ilo niliugua mnoooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…