Ngoja na mimi nichangie kidogo hapa;
Mm nipo Dodoma toka 2017, Dom ilikuwa na watu wengi sana wanaojihusisha na masuala ya ujenzi mda huo nyumba nyingi sana zimejengwa, Ilazo, Swaswa, Nzuguni, Meriwa, Kisasa, Iyumbu, Mkonze pia Michese (hii ni mitaa mipya kabisa tulioijenga sisi, ikumbukwe mm n mkandarasi)
Kabla ya hapo mitaa iliyokuwa na watu ilikuwa ni Nkuhungu, Maili 1 & 2, Majengo, Changombe(kwa warangi), kuna mtaa umenitoka ila ni karibu na CBE zilipo ofisi za mapasi naona siku hiz uongozi wa mji wamevunja wanampango wa kuweka bustani, pia kulikuwa na vijumba kidogo juu ya station ya TRC kama unaenda Ntyuka mitaa ya Pestana
Ipo hivi Dodoma imejenga sana kuliko Mwanza kwa kipindi hiki hakuna ubishi, maana mitaa niliyotaja hapo mwanzo yote ni mipya, changamoto ni moja tu hiyo mitaa mpya haina watu, utakuta nyumba moja wanaishi watu wanne tu, yaani familia ya baba mama mtoto na beki tatu
Na ndio maana hata upande wa usafiri Dom ni changamoto sana, Dom hakuna daladala za kutosha nadhani hii ni sababu ya uchache wa watu thats why daladala zote za Dom zinaishia sehemu moja na zinatosha (sabasaba) na zingine kidogo Majengo, My friend Mwanza hakuna eneo unaweza kuweka daladala za mji mzima sehemu moja zikatosha
Pia hapo hapo kwenye usafiri Dom ina route chache sana za daladala naweza kuziweka hapa, Nane nane - 77, Mipango-77, Ntyuka-77, Kwa massta (Nzugun)-77, Nkuhungu-77, Chan'gombe-77, Swaswa-77, Msalato-77,
pia kuna kidogo zinaishia majengo ambazo ni Mnada mpya- Majengo, Mkonze-Majengo pia. zipo daladala kama mbili au tatu zinajaribu kwenda Michese, unaweza nikumbusha nimesahau route ipi ya daradara hapo mkuu, maana ake route za daladala Dom hazizidi 11
Wakati huo huo mtu anaetoka Nanenane kwenda Chang'ombe kwa mfano hawezi kupata route ya moja kwa moja ni lazima aingie sabasaba achukue daladala lingine aendelee na safari, kuna sehemu kama Kikuyu hakuna daladala kabisa ni mwendo wa bajaji , njoo Kisasa anzia hapo Kwa mnama njoo mpka La Liga zunguka hiyo ring road Kisasa sekondari, Amazon ingia ndani ndani kote hakuna usafiri
Kufikia hatua mnaiongelea Mwanza najua mtakuwa mmeshafika mnapajua vizuri mm sitaki kueleza maana ndio nyumbani mnaweza kusema ni sehem gan kwa Mwanza pamoja na kuwa jiografia yake ni milima ni sehemu gani unaweza unga dalala ukiitoa Nyashana?( kwa ambao mnaiponda tu Mwanza kwa kusikia mnakosea sana) Mm mji yote Tz naijua
Tafuteni mafundi ujenzi au watu waliopo kwenye sekta ya ujenzi muulize kuhusu kasi ya ujenzi ilivyo Dom sasa hivi mtajua kuwa Dom pia imeanza kwenda taratibu,, ni tofauti sana na ilivyokuwa before na sababu ni kuwa nyumba zimekuwa nyingi lkn hazina watu, (maana Dom nyumba wanajengewa wageni na tayari wameshapata, wenyeji wapo wapo tu)
Nenda Kisasa, Swawa, Ilazo kote 30% ya nyumba hazina watu, na hapa nishauri tu uwekezaji wa real estate unaenda kudorora Dom, watu wamejenga lakini hakuna wapangaji Dom haina watu, mfano Dodoma soko la maana lenye watu lipo moja tu (sabasaba) na limebeba bidhaa zote japokuwa majengo kidogo inavyakula, ikitoka city center ya Dom center ndogo ndogo kama Buzuruga, Mecco, Nyakato, Kona ya Bwiru, Buhongwa, Nyegezi, Sabasaba(mbao), Nyasaka nk kwa Mwanza Dom huzikuti na hata ukizikuta ni ndogo sana kama Makuru, Meriwa, Kwa mnama
Maanake ni kwamba mjasiriamali mdogo wa genge la matunda na mboga mboga wa Mwanza kama yupo Buzuruga anachukulia bidhaa zake Mecco sokon kama yupo Buhongwa anachukulia hapo hapo Buhongwa ila Dom wote wanaenda Sabasaba mpaka mtu wa Chamwino anahemea sabasaba
Dodoma majengo marefu yaliyokamilika mpaka sasa ni matatu tu (Kambarage, PSSSF na Dom city hotel kwingine kote ni vijengo vya ghorofa tano kushuka chini
Ukubwa wa mji Dom inaanzia Nala upande wa magharibi, Mkonze na Ntyuka Kusini magharibi, Ng'ong'ona, UDOM, Iyumbu upande wa Kusini mashariki, Nane nane, Ilazo upande wa magharibi (hapa Ihumya naitoa maana hapo katikati Elishadai na St Peters kuna kipori, Chama Msalato na Mipango upande wa kasikazini hapo Dom ndio ilipo Mtumba ipo nje sana na katikati kuna eneo kubwa sana la wazi tunaitoa japo ipo nda ya halmashauri
Dom nimeifahamu yote ndan ya wiki moja na hakuna sehem unanidanganya,,,,, oyaaaaa eeeeeh? Njoo Mwanza sasa!!!
Kiukwel huwaga naumia sana kusikia mtu anaiongelea Mwanza na Dom, Mwanza ina manispaa mbili ndan ya mji (Ilemela na Nyamagana) Dom haina, Mwanza imekuwa jiji rasmi awamu ya tatu 2002 Dom ikawa 2017
Nyakato kuna viwanda vya kila aina Nondo, Soda(koka na peps zinatoka ndan ya mji) wakati Dom zinatoka Dar, Bia SBT na TBL wanafyatua ndani ya mji, idadi ya hotels route za safari za ndege ATCL na Precision Mwanza ina safari nyingi kuliko mji wowote ukiitoa Dar, Reli ya mwendokasi Dom hakuna fly over hakuna kote wameweka kifusi, Mwanza Fly Over ipo hakuna kifusi
Duh! Nyie endeleeen kuifananisha Mwanza na KiDodoma chenu, kuna jamaa amewahi kuniambia Dom kuna nyumba za kishua nikazitafuta Area D, Mlimwa C sikuziona kidogoooooo nikazikuta Michese zenye za ghorofa moja moja, nikamuuliza unaijua Kapripoint wewe, Bwiru kupata kiwanja tu mil 150 na kuendelea hapo bado hujavunja mawe maana unanunua mlima wenye mawe uvunje mwenyewe ndio kiwe kiwanja na kuvunja tu inagharimu mil 100 zingine ndio uanze kujenga hapo tayari mil 200 na kitu zimetumika huna hata msingi