ChoiceVariable unajihangaisha bure , Mwanza ni Jiji kubwa hapa TZ lina Manispaa mbili , utahangaika sana na kupost sana project za serikali , Mwanza hawategemei serikali , ngoja nikupe mfano : kwanza Brazil mji mkuu wao ni Brasilia umejengwa kiserikali ila maisha yapo Rio de Janeiro na Sao Paulo ,
Pili: Myanmar (Burma) mji mkuu wao ulikuwa Rangoon sasa ni Naypyidaw
Point yangu ni kuwa serikali inaweza kuweka miundombinu hapo kwa mahitaji yake ya sasa ila majiji Toka enzi na enzi yanajengwa na biashara , sasa hapo Dodoma Kuna biashara gani unaweza kufanya labda kuomba omba ! Ndio maana soko la Ndugai liko tupu mpaka Mama alisema wabalidilishie matumizi.
Watu wanatafuta fursa za biashara ndio maana wanakimbilia mijini, nyie biashara zenu za msimu tena wakati wa Bunge , kaa barabarani hapo Dom afu hesabu gari za abiria na mizigo zinapita hapo kwenda Mwanza afu hesabu zinazoishia hapo Dom , ndio maana Dodoma ni njia panda tu.
Hongera kwa picha zako lile bwawa, Mwanza walipewa ziwa bure na Mungu hawahitaji bwawa,
Nasikia jamaa wanapambana kinyama ili treni ya umeme ifanye kazi ili wawe wanarudi Dar jioni .
Hakuna anayetaka kukaa jangwani , mjini mjini tu