Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Unahisi tukiachana na CBD tukahesabu jengo moja moja la ghorofa mpaka lingine kwa mji mzima mwanza inatoboa kwa Dom?

Vipi ushaitembelea chinangali, CBE, Majengo,mazengo,nyerere square, sabasaba, developed cities area n.k huko kote majengo marefu yanazidi inuka tu ndugu yangu kitu pekee mwanza inaizidi Dom kwa sasa ni ile density/kusongamana kwa maghorofa katika eneo finyu la CBD yao ukilinganisha na Dom.

Dodoma CBD imetanuka nje ya kariakoo yao ndogo inayoitenganisha na CBD nakuleta mwonekano wa kisasa na majengo mazuri yaliyoachiana uwazi wa kupumua ukilinganisha na Zoo na siku nyumba za bati au kawaida zikishaondoka zote kupisha ghorofa CBD ya Zoo ikatafute ligi yake kwenye suala la CBD.
 
Shughuli gani za kiuchumi zipo hapo Dodoma ambazo unaweza ukazilinganisha na Mwanza. Mwanza ndo kitovu cha biashara kanda ya ziwa na pia inaunganisha mpaka na nchi jirani. Hela nyingi za dhahabu uko Kahama, Geita zinakuja Mwanza. Ukiachana na dhahabu, fishing industry ipo juu sana.
 
Hizo ni kodi za Watanzania zilizokusanywa mikoani ndizo zinazojenga hapo acha ushamba eti magorofa majengo ya serikali hayo we unaona fahari.
 
Hali ya hewa Dodoma inakwaza sana...miti ipandwe kwa wingi tena kwa lazima...
 
We mgogo acha mabalaaa

Ivi pale Dodoma Wana garden nzuri kweli ?

Na hili la kisema Basi nzuri Zina anzia Dodoma kwenda Dsm ...hapa umepaishaaaa
 
Acha uongo wakulinganisha manispaa na jiji na mwishowe unajidumaza kwa kukosa exposure tafuta nauli ufike Dom kwanza afu uje ufute comment yako
jiji imetamkwa tu lakini dodoma hakuna quality za kuitwa jiji mji umejaa omba omba kila mahali ile airport pale ukishuka unaenda kupanda bodaboda alafu hata bunge sijui kwanini wali allocate likae pale barabarani yani bunge linapakana ukuta na chuo jamani mi nilitegemea liwe sehem flani nje ya mji waswahili hawafiki kirahisi sasa bunge nalo liko katikati ya mji hivi gari la matangazo likipita pale sauti haifiki ndani mule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…