Dodoma inaendelea kuhamisha makao makuu na shughuli zote za kiserikali kwake, uwekezaji wa serikali kwenye taasisi, wizara, makazi bora na vitega uchumi vyake kipaumbele ni Dodoma, sekta binafsi zinaendelea kuwekeza, viwanda na viwanja vipya vinaendelea kujengwa, miundombinu kama barabara za lami na reli, bandari kavu n.k
Vitu vingi vilivyokuwa vinaifanya Dar iwe tegemeo na kimbilio la watu wengi kwa kila kitu toka mikoani na nchi jirani vinaanza kuondoshwa kidogo kidogo;
ikiwemo kufuata huduma za kiserikali dar, ajira, usafiri wa anga,ulazima wa kufuata mizigo bandarini, miundombinu mizuri, huduma za kijamii, elimu ya juu, mazingira ya kibiashara na uwekezaji, real estate, n.k
Vitu kama hivi kama siyo vyote vitakuwa vinapatikana Dodoma hivyo Dar lazima tu kasi yake ya ukuaji na uchumi lazima itetereke kimtindo japo haiwezi kuyumba kutokana na umuhimu wa mji huu kiuchumi, population na uwekezaji mkubwa uliopo, kikubwa ni kuwa itabakia kuwa kama Mwanza ikijipambanua kibiashara tu na siyo vinginevyo.