Endeleeni kujifariji tu Mwanza hakuna mtaa wowote unaofika ubora wa mpangilio wa mitaa ya Dom labda kidogo Capri Point.Capripoint wakati inapumuliwa kisogoni na mitaa kama Bwiru, Ilemela, mwanachi, majengo na ibanda mtu wa hivyo haijui Mwanza, bado kuna mitaa hata hiyo Ilazo na kisasa haiwezi kutia miguu kama vile Nyasaka, buswelu, kiseke, nyamhongolo, mkolani n.k kutwa nzima kupost picha za Igogo kakipande kadogo ka mlimani kamekuwa ni fimbo ya kutuchapia.
Nakupa mifano michache
-UZUNGUNI huko kote kumepangiliwa lami tupu hakuna barabara ya vumbi hata moja
-KILIMANI kwa waheshimiwa-huko kote kumepangiliwa hakuna barabara hata moja ya vumbi yaani hadi vibarabara vinavyoingia kwenye nyumba za watu zote ni za lami
-KISASA huko kote ni full lami +mfumo wa kisasa wa uondoshaji wa majitaka na takataka zingine
-ILAZO huko huwezi kuona hata choo tu cha uswahilini tena huko ndio balaa nyumbazote ni zile za fashion mpya utadhani wakaazi wa kule wameambiana .
Hapo bado sijakuongezea mitaa mingine kama Area E(kwa waheshimiwa), Area D- kwa waziri mkuu,Mlimwa C,Maghorofani,Miyuji Proper,Itega,Area A,Magereza,Kisasa extension,Medeli NHC n.k
Mwanza hakuna mtaa wowote uliopangiliwa 100% mitaa angalau inayojitahidi na yenyewe imechanganyika na uswazi+vijumba vilivyojengwa bila mpangilio. Tatizo lenu hamtaki kukubali ukweli Dom unayoiona leo imeanza kupangiliwa tangu enzi za Nyerere sasa utalinganishaje na Mwanza ambayo mpaka leo barabara tu za mitaa bado ni changamoto.