Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Ndugu zangu wa Kanisa kubwa duniani, Kanisa Katoliki - poleni sana kwa msiba mzito. Wakati maombolezo yakiendelea, naomba tuongee kiutu uzima; kwa heshima na upendo.
Kwanza ninawapongeza: mkiwa Kanisani, mnaonyesha heshima kubwa kwa Mungu. Sasa naomba mnijibu swali hilo: Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?
Nimesikia mnafundisha kwamba Mtume Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu kuwa msingi wa Kanisa au Papa wa kwanza. Mnanukuu Mathayo 16:18 na kusema kwamba katika Andiko hilo Yesu alimwambia Petro, “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.” Kwa tafsiri yenu, “mwamba” huo ni Petro mwenyewe, na hivyo mnamuona kama Papa wa kwanza. Mnaamini kwamba, mamlaka ya Petro kama kiongozi wa mitume yaliendelezwa na Mapapa waliomfuata, wakiwa viongozi wa juu wa Kanisa la Kristo duniani. Ni kweli?
Kama ni kweli, mbona mtazamo wa Kiprostestanti unatofautiana na mafundisho yenu. Waprotestanti wanasisitiza kuwa msingi wa Kanisa sio mtu binafsi, bali ni Yesu Kristo mwenyewe (1 Wakorintho 3:11), na kwamba “mwamba” aliouzungumzia Yesu ni Yeye mwenyewe(Yesu) kama Petro alivyokiri: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16).
Kwa mtazamo wa Kiprostestanti, Petro hakuwa Papa, kwa sababu hakuna ushahidi wa kibiblia unaoonyesha kuwa alipewa mamlaka ya kipekee juu ya mitume wengine. Na wakati wa Kanisa la kwanza mfumo uliopo leo wa kipapa, haukuwepo.
Waprotestanti wanaeleza tena kwamba Viongozi wa kwanza wa Kanisa walifanya maamuzi yao kwa ushirikiano (Mdo 15), sio kwa mamlaka ya mtu mmoja(Papa). Wanasimama na Andiko la Waefeso 5:23 linalosema kwamba Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa. Wanaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeliongoza Kanisa lote sasa, na sio kiongozi mmoja wa kimwili. Wananukuu Yohana 16:13
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote."
Hoja hizo mnazijibuje?
Ntashukuru sana nikipata majibu ya swali langu na majibu kuhusu hoja hizo za Kiprotestanti. Majibu yajengwe kwenye Maandiko Matakatifu(Biblia). Tumsifu Yesu Kristo.