Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Aliachiwa mamlaka kwa Andiko lipi, mkuu. Tafadhali weka vifungu vya Biblia hapa
mbona sehemu za biblia ni nyingi inaonyesha wazi kabisa

Yesu ali deal sana na Petro sehemu nyingi kuna sehemu hadi anamuuliza Je unanipenda ? pero akajibu ndio akamwambia Chunga kondoo zangu,

kunasehemu
"Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewaomba kuwapepeta kama vile ngano; lakini mimi nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka, waimarishe ndugu zako."

kuna sehemu ndo hiyo unayoikataa sijui kwa misingi gani anasema
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."

ki Teolojia Yesu alikua anamuimarisha petro tangu mwanzo alikwepo nae katika maeneo muhimu kwa upekee
hata anavyoenda kubadilika sura alikua na petro pia

Yaani kimsingi Yesu alikua anamjenga petro kua kiongozi wa wengine na azidi kia imara hata Yesu atakapo paa
 
mbona sehemu za biblia ni nyingi inaonyesha wazi kabisa

Yesu ali deal sana na Petro sehemu nyingi kuna sehemu hadi anamuuliza Je unanipenda ? pero akajibu ndio akamwambia Chunga kondoo zangu,
Maandiko uliyotoa hayamtaji Petro kuwa ndiye kiongozi wa juu wa kanisa lote. Soma vizuri kitabu cha Matendo ya Mitume, utaona kuwa Petro alikuwa miongoni mwa mitume wengine. Hakupewa mamlaka ya kipekee.

Kwa mfano katika Matendo 15 tunasoma juu ya kikao kilichofanyika Yerusalem. Petro aliongea na mitume wengine waliongea, lakini mwishoni aliyetoa uamuzi wa nini kifanyike alikuwa Yakobo. Sikiliza anavyosema kuanzia mstari wa 13:
"Walipomaliza kuongea, Yakobo alianza kusema: “Ndugu zangu, nisikilizeni! Simoni ameeleza jinsi Mungu hapo awali alivyojishughulisha na watu wa mataifa mengine, akachagua baadhi yao wawe watu wake...Kwa hiyo, uamuzi wangu ni huu: Tusiwataabishe watu wa mataifa wanaomgeukia Mungu. Bali tuwapelekee barua kuwaambia wasile vyakula vilivyotiwa unajisi kwa kutambikiwa vinyago vya miungu; wajiepushe na uasherati; wasile mnyama yeyote aliyenyongwa, na wasinywe damu."

Kama Petro angekuwa ndiye mkuu(papa) uamuzi usingetolewa na Yakobo.

Maandiko mengine yanayoonyesha tena kwamba Petro hakuwa papa wala kiongozi mkuu wa Kanisa yapo katika Wagalatia 2:11-14. Hapo Paulo anamkemea Petro hadharani kwa makosa yake. Ulisikia wapi Papa anakemewa na mtu aliye chini ya uongozi wake?

Maandiko uliyonukuu “Chunga kondoo zangu” siyo ushahidi wa upapa.
Yesu alipomwambia Petro “chunga kondoo zangu” (Yohana 21:15-17), sio kwamba alikuwa anampa wadhifa wa juu bali alikuwa akimrejesha baada ya kumkana mara tatu. Ndio sababu alimuuliza, unanipenda?

Kuchunga kondoo ni kazi ya kila mchungaji.
Petro mwenyewe aliwaambia wazee wa kanisa:
1 Pet 5:2
"Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.”

Katika kitabu cha Wakolosai 1:18 tunasoma kuwa Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa, yaani Kiongozi Mkuu wa Kanisa, na siyo Petro
“Naye ndiye kichwa cha mwili(Kanisa)”

Kanisa la kweli halijengwi juu ya mwanadamu bali juu ya Kristo. Kwahiyo ndugu yangu, kwa ushahidi wa Maandiko hayo, cheo cha Upapa sio cha kibiblia.
 
basi sawa wewe amini unavyo amini, haujui Teolojia, unachambua biblia kama unachambua riwaya,

mimi naijua biblia vizuri na nimesoma seminari naweza ata kuanzisha kanisa la kilokole ma pastor wenu wengi tu wakakaa

sasa wewe amini huko hivohivo,

ila hili ndo Kanisa Takatifu Katoliki La Mitume, halitikisiki
lipo imara kwa miaka elfumbili sasa

Kanisa Katoliki ndo limeshikilia Ukristo, maandiko na nyaraka zote za ukristo, hata Kanisa kuu la Mtakatifu Petro limejengwa sehemu alipozikwa mtume Petro
 
Duh, kama kwa kusoma tu seminari unajivuna, basi siku ukipata PhD 20 za theology, dunia nzima itajua.

Ingekuwa heri ukajisifu kuwa unamjua Mungu, kuliko kujisifu kwamba umesoma Teolojia seminari.
Yeremia 9:23-24
"Mwenye hekima asijisifu kwa hekima yake... Bali ajisifuye na ajisifu hivi, ya kwamba ananifahamu mimi...”

Hiyo elimu uliyopata seminari, mbona umeshindwa kuitumia kuweka hapa "nondo" za kuthibitisha pasina shaka kwamba Petro alikuwa Papa?

Sasa, kwakuwa hakuna mtu aliyeweza kujibu swali langu, nahitimisha uzi huu kwa ujasiri nikisema:
PETRO HAKUWA PAPA WA KWANZA. PETRO ALIKUWA MTUME TU KAMA MITUME WENZAKE.

Tumsifu Yesu Kristo aliye Kimbilio letu na Mwamba wetu wa milele.

Wote tuseme: "Amina"
 
ok sawa Kila mtu si anaweza kuhitimisha anavyotaka

mimi nimehitimisha kwamba
Petro alikua kiongozi wa kanisa la mwanzo Petro alipewa mamlaka na yesu Myenyewe kuongoza kanisa na kuwaongoza wenzake

Matukio Mengi kwenye injiki yanaweka ukaribu wa Yesu na Petro ikimuonyesha jinsi alikua akimuandaa kuwa kiongozi wa wenzake

"Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewaomba kuwapepeta kama vile ngano; lakini mimi nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka, waimarishe ndugu zako."

Mwisho kabisa Moja kwa moja akamwambia

"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni"

mambo yote na mengine mengi hajawaambia mitume Wote alimwambia Petro tena kwa kumtaja kwa jina

ili kufunga mjadala huu basi ngoja nikupe historia ya viongozi wakuu wa kanisa kama ilivyoandaliwa na AI

Hii ni historia nzito sana na ya kipekee kwa Kanisa Katoliki. Tuichambue vizuri kidogo:

---

### 1. Mtume Petro – Kiongozi wa Kwanza
- Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu mwenyewe:
“Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu…” (Mathayo 16:18)
  • Aliongoza Kanisa la kwanza huko Yerusalemu kisha akaenda Roma, ambako aliuawa kifo cha msalaba kichwa chini.
  • Anachukuliwa kama Askofu wa kwanza wa Roma, na hivyo Papa wa kwanza, ingawa hakuitwa kwa jina hilo wakati huo.

---

### 2. Viongozi Waliomfuata Petro (Karne ya 1–3)
Katika kipindi hiki cha mwanzo, viongozi wa Kanisa la Roma walijulikana kama Maaskofu wa Roma, si “Papa” bado kwa jina rasmi.

Baadhi ya hao ni:
  • Lino (Linus) – Alimfuata Petro (ametajwa pia kwenye 2 Timotheo 4:21)
  • Klementi wa Roma (Clement I) – Maarufu sana kwa barua zake kwa Wakristo wa Korintho.
  • Ignasi wa Antiokia (ingawa si wa Roma, alikuwa wa muhimu sana kimataifa)
  • Anacletus, Evaristus, Sixtus I, na wengine.

Kwa ujumla, hadi kufikia mwaka 300, kulikuwa na takriban 30+ wa viongozi waliofuata Petro kama Maaskofu wa Roma.

---

### 3. Kuitwa Kwao “Papa” Kulianza Lini?
  • Neno “Papa” (kutoka Kigiriki pappas = baba) lilianza kutumika taratibu karne ya 3–4, lakini halikuwa rasmi kwa Roma pekee.
  • Papa Leo I (Leo Mkuu) aliyeongoza mwaka 440–461 alitambua mamlaka ya kipekee ya Askofu wa Roma.
  • Mwaka 1073, Papa Gregory VII alitangaza rasmi kuwa jina “Papa” ni la Askofu wa Roma pekee, si wa viongozi wengine wa makanisa mengine kama Aleksandria au Antiokia waliokuwa wakilitumia pia.

---

### 4. Kwa Nini Roma?
  • Kwa sababu Petro na Paulo waliuawa Roma – mji mkuu wa Dola ya Kirumi – Roma ikawa “kitovu cha Kanisa”.
  • Petro alionekana kama msingi wa Kanisa, na Roma kuwa mji wa ushahidi wake wa mwisho.

---

### Kwa Muhtasari:

| Mstari | Jina | Jukumu |
|--------|------|--------|
| 1 | Petro | Kiongozi wa kwanza, Askofu wa Roma, Papa wa kwanza |
| 2 | Lino | Mfuasi wa Petro, aliyeongoza Roma baada ya Petro |
| 3 | Klementi I | Maarufu kwa maandiko yake ya imani |
| … | … | Maaskofu wa Roma (30+ hadi mwaka 300) |
| ~440 | Leo Mkuu | Alianza kuimarisha cheo cha Papa |
| 1073 | Gregory VII | Alifanya jina “Papa” kuwa rasmi kwa Roma tu |

---

Ukihitaji listi ya mapapa wote kuanzia Petro hadi leo au mapapa wa mwanzo 10 au 20, naweza kukutengenezea pia. Unataka?
 
Hitimisho huwa ni moja tu. Na liliishatolewa kwamba Petro sio mwamba na pia sio Papa wa kwanza. Ushahidi wa kutosha umetolewa kutoka kwenye Biblia. Period
 
Luka 1:41-49,55
[41]Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
[42]akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
[43]Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
[44]Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
[45]Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
[46]Mariamu akasema,
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
[47]Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
[48]Kwa kuwa ameutazama
Unyonge wa mjakazi wake.
Kwa maana, tazama, tokea sasa
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
[49]Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,
Na jina lake ni takatifu.
[55]Kama alivyowaambia baba zetu,
Ibrahimu na uzao wake hata milele.

Kwa hiyo sisi wakatoliki hatumweshimu kwa mafundisho ya kukalili, ila sisi hufundishwa kusikia, kutafakali na kuyaishi, hatubebwi na mafundisho ya baba mchungaji,

Kuhusu Petro na hao wengine siwezi kukujibu kwa sababu hata vitabu ambavyo ningekujibia nyie hamvikubali, mnaviita jina BAYA, kwa hiyo relax , jifunze , utafakali na utachuja
Umejitahidi kuhamisha mada kwa andiko hili.

Lakini bado haujaonesha mahali Petro na hao watakatifu wenu walipoabudiwa
 
Ukipata Muda soma kitabu Cha makabayo,which I know you are strictly prohibited 🚫 in your faith, tafuta uhuru wako, acha kuyaishi maelekezo ya baba mchungaji
 
Screenshot_2025-04-27-08-45-00-004_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
 
Swali la Kwanza ni kama Sijalielewa Hivi Unazungumzia mamlaka Ipi ya Kimungu ambayo unahisi Kanisa lolote linayo yaani mamlaka ya Kiungozi au kikuhani?

Swali la Pili:
Yesu hakuacha Kanisa ,Aliacha Mitume wake! Na Mitume wake hawakuacha Kanisa pia!

Swali la tatu!

Wazo la Petro kuwa papa wa kwanza ni msimamo wa baadaye wa Kanisa Katoliki nadhani ni kwenye Kaerne ya Pili mapaka ya Tatu hivi na si mafundisho ya mitume wenyewe. Hakuna mahali Petro alijitambulisha kama kiongozi wa ulimwengu wa Kikristo...
Na hata Paulo ameenda Rumi mara Nyingi ameenda Antiokia Mara Nyingi hakuwahi kumtambulisha Petrk kama kiongozi wa Kanisa..

Kuhsu Mtiririko wa mapapa ulianza kufuatiliwa rasmi katika karne ya 3–4, lakini ulirasimishwa kisiasa na kiteolojia wakati wa Papa Gregory I (590–604 BK). Yeye si muasisi wa Kipapa, maana Mapapa walikuwa wengi Dunia Nzima kila Nchinna Kila Ukanda ila lakini yeye ndiye aliyepatia Upapa sura Mpya ya ya kisasa na Kisiasa (papa kama kiongozi mkuu wa ulimwengu wa Kikristo) ambayo hapo Kabla haikuwepo na Rasmi papa wa Roma Akawa Ni papa wa Dunia Nzima..
Swali la kwanza ni hivi, sasa hivi kuna makanisa mengi na kila kanisa lina uongozi wake, wengine maaskofu, wachungaji, manabii, mitume mpaka wengine wanajiita yesu huko Kenya, sasa kwa hayo makanisa ni upi uongozi wa kimungu unaofuata maagizo ya biblia juu ya uongozi wa kanisa?

Ila kabla ya hapo, kanisa ni nini? Kama hao hawakuacha kanisa, wakitaja kanisa walikua wanamaanisha kitu gani?
 
Kwakuwa Najibu kwa Kufuata Maandiko na Nitakujibu kwa Upande wa Christian Theology kwa Ujumla na Nitasema Kuwa kanisa halimaanishi jengo au taasisi ya kidini kama tunavyoona leo..
Neno "kanisa" linatokana na neno la Kigiriki "ekklesia",

Tuanze kwa Kuliangalia Hili neno!..

ἐκκλησία (ekklēsía)

Hili neno linatokana na mzizi wa maneno mawili:

ἐκ (ek) = "kutoka"
καλέω (kaleō) = "kuita"

linalomaanisha "walioitwa kutoka nje" au "kusanyiko la waumini Kutoka Nje!

Kanisa ni watu, si jengo.
Yesu aliposema “Nitakalijenga Kanisa Langu” (Mathayo 16:18), hakumaanisha jengo, bali mwili wa waumini watakaoishi kwa kufuata mafundisho yake.

Katika Agano Jipya, Paulo analiita kanisa “mwili wa Kristo” (1 Wakorintho 12:27, Waefeso 1:22-23). Hii inamaanisha kuwa kanisa lina uhusiano wa moja kwa moja na Kristo kama kichwa chake..

Je Uongozi wa Kanisa Kwa Mujibu wa Biblia Ni Upi hili si ndo swali lako la Msingi Vishu Mtata (Ndo Msingi wa Swali)..

Sasa kwanza Kwa Mujibu wa Uktisto Uongozi wa Kikuhani Ulifutwa kwa Sababu Inaaminika Kuhani Ni Mmoja Peke yake Ambaye ni Yesu na Katika Hilo.hakuwa na Naibu wala Kaimu..
Sasa Hata Kwenye Senhedrin Kiongozi mkuu ni Kuhani Si ndiyo 😀
Haya Tuache Hilo Tuangalie Uongozi wa Petro na Paulo baada ya Yesu kwishaondoka..

Kwa Mujibu Wa Biblia Uongozi Haukuwa wa Mtu mmoja au kwamba Kuna Mfumo wa Juu wa Uomgozi..

Huu Ndo uongozi Ulivyokuwa Kuanzia Juu..

a) Mitume wa Yesu 12

  • Walikuwa mashahidi wa moja kwa moja wa huduma, kifo na ufufuo wa Yesu.
  • Waliweka misingi ya mafundisho na waliongoza kwa mamlaka ya kiroho.
  • Walihubiri, walifundisha, waliombea wagonjwa, na kuongoza mikutano ya kanisa.
  • KAma Utakumbuka Alichaguliwa mathiya Kuchukua nafasi ya mtume wa 12 ambaye alikuwa yuda baada ya Kufariki..
  • na Paulo anaingia kwenye Kundi hili baada ya Kusema Alipewa Utume na Yesu mwenyewe kwa watu wa Mataifa Galatia 1:1
Ukitoka Kwenye Mitume Hao Chini Yao Walikuwepo Mashemasi ambao nao walikuwa na Cheo Kinachokaribiana na Mitume Unamkumbuka Stephano? Alikuwa Shemasi..

b) Mashemasi (Deacons)

  • Matendo 6:1-6: Mashemasi 7 walichaguliwa kusaidia kazi za kila siku (kama kugawa chakula), ili mitume wajikite kwenye Neno na maombi.
  • Hii ilikuwa mwanzo wa mgawanyo wa majukumu kati ya kiroho na huduma za kawaida.
  • Hawa nitakutajia Kipindi cha Mitume walikuwa (Filipo (baadaye alihubiri kwa nguvu – Matendo 8), Prokoro,Nikanori,Timoni,Parmena na Nikolao (mgeuzi wa dini kutoka Antiokia))

c) Wazee (Elders/Presbyters)
  • Wazee waliwekwa katika makanisa mapya (Matendo 14:23, Tito 1:5).
  • Paulo na mitume walikuwa na desturi ya kuweka wazee ili kuliongoza kanisa kwa njia ya usimamizi wa kiroho.
  • Wazee walikuwa viongozi wa heshima, waliojali tabia, mafundisho sahihi, na malezi ya waumini.

d) Waangalizi (Bishops/Overseers)

Maneno mchungaji (pastor), mzee (elder), na askofu (bishop) mara nyingi yalitumiwa kwa kubadilishana.

Waefeso 4:11 inasema Yesu alitoa wengine kuwa wachungaji na waalimu kwa ajili ya kuijenga kanisa.

1 Timotheo 3 na Tito 1 zinaleta sifa za viongozi hawa – kuwa na tabia safi, waaminifu, wasio na tamaa, waadilifu.

Sasa Huu Ndo ulikuwa Uongozi Rasmi ila Kufikia Karne ya 2 Mwishoni Walibadilisha Msimamo Rasmi kanisa Lilipokusa Chini ya Katholic na Kuweka Misingi yao Iliyopo sasa..

Swala la kwamba nani yupo Sahihu Kulingana na Biblia Hakuna Kanisa lolote au Dhehebu lolote lilio sahihi Kwa sababu wote wametohoa Mifumo kutoka Katika Upotofu Uliofanywa Kutoka roma..

Yaani Walichukua Mifumo Mibovu Ya Kanisa Na ambayo walikuwa wameirithi..
 
Aisee pasi na kuweka hisia na ushabiki kando hakyanani wengi wanaabudu wasivyovijua.
Hii mifumo ya kanisa inawapa watu umungu mtu, watu wanatukuzwa kama miungu .
 
Back
Top Bottom