Munamuge
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 907
- 903
Hapa sasa unakosa elimu ndogo ya Biblia kwamba kila verse inakua na ujumbe wake maalum (conceptual meaning) ambao unatokana na lengo maalum la kitabu ama sura hiyo. Lakini maana hizi hazipingani kwenye dhumuni kuu la Mungu kutuumba ili tumtumikie, kutukomboa kutoka utumwa wa dhambi na kutuahidi kuwa siku moja tutarejea katika makao yake ya milele na kufurahi pamoja na watakatifu wake.Unarudia pointi zile zile. Nimekuuliza: Daudi na Isaya wamesema kwamba Mwamba ni Yesu.
Yesu hawezi kujipinga kwa kumwita Petro Mwamba.
Soma tena Andiko hili:
Zaburi 73:26
"Hata nikikosa nguvu mwilini na rohoni, wewe, ee Mungu, u mwamba wangu.."
Halafu umekiri mwenyewe kwamba kulitokea migawanyiko. Sasa jiulize: Yesu alisema milango ya kuzimu haitalishinda. Ilikuwaje sasa migawanyiko ikatokea? Migawanyiko ni ishara ya ushindi?
Ukiongelea kitu kimoja kutajwa kwa maana tofauti katika Biblia unaweza kuelezeaje hivi vifungu?
1. Uumbaji kufanyika kwa njia mbili tofauti (Mwanzo 1:1 na kuendelea na ule wa Mwanzo 2:4-25.
2. Mungu kuumba mwanamke na mwanaume kwa pamoja na baadae tena Mungu kumuumba mwanamke mwishoni kutoka katika ubavu wa Adam (Mwa 1:27 na Mwa 2:21)
3. Baba mzazi wa Yusufu aliekua mume wa Mama yake Yesu, je ni Yakobo (Mat 1:16) ama Eli (Luk 3:23)
4. Yohana Mbatizaji ndie alikua Elia ambae waisrael waliamini atarudi? Yesu alimtambulisha hivyo alipokua anawafundisha makutano (Mat 11:14) lakini Yohana mwenyewe alikana hilo alipoulizwa na makuhani na walawi (Yn 1:21)
5. Yesu kumpa sifa kedekede Simoni Petro katika vipindi tofauti, lakini pia kumwita shetani baada ya Petro kutaka kuonesha imani yake kubwa kwa Yesu kwamba hawezi kupatwa na mambo mabaya (Mat 16:23). Kwahiyo hapo napo utatuuliza kuwa Je Petro ndie aliekabidhiwa kuchunga kondoo kweli kwenye injili ya Yohana baada ya Yesu kufufuka na kuwatokea mitume kule pwani ya Thiberia (Yn 21:15-17) ama ni shetani?
Biblia sio kitabu cha Chinua Achebe ambacho unaweza kukisoma na kukifanyia nukuu kadri unavyojiskia.