Ndugu zangu Wakatoliki bado hamjajibu swali langu. Mliojaribu kujibu, mmetaja mstari ule ule wa Mt 16:18
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."
Siamini kwamba katika mstari huo au kifungu hicho Mwamba ni Petro. Siamini kwa sababu katika Maandiko yafuatayo imeelezwa wazi kuwa
Mwamba ni Mungu. Haya ni Maandiko ya Agano la Kale. Wakati huo Petro alikuwa bado hajazaliwa:
Zaburi 62:6
Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika.
Zaburi 18:2
Mwenyezi Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu;
Isaya 26:4
Mtumaini Mwenyezi Mungu milele, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwamba wa milele.
Maandiko hayo yanaonyesha pasina shaka kwamba Mwamba ni Mungu. Na Yesu kwakuwa ni Mungu Mwana, Yeye pia ni Mwamba. Ndio sababu katika
1 Wakorintho 10:4 Yesu ametajwa kuwa ni mwamba
"Wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo."
Biblia inasema kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa(2 Kor 13:1). Daudi, Isaya na Petro mwenyewe wamesema kwamba
Mwamba ni Mungu - Mwamba ni Yesu. Kwahiyo ni dhahiri hata katika mstari ule wa Mt 16:18, mwamba ni Yesu. Kwa maana hiyo Petro hastahili kuitwa Mwamba na kwakuwa sio Mwamba, hastahili pia kuitwa Papa. Kwa mantiki hiyo, sio kweli kwamba Mtume Petro ni Papa Mtakatifu wa kwanza. Nope!
Hayo ni maoni yangu kulingana na Maandiko.
Karibuni wote mliochangia uzi huu tuendelee kujadiliana:
Lwiva Phaul Lior Eyce Chasaga Genius Man The Worst pharao Munamuge Mnywani mgen publito KimMinA Mufupi Monetary doctor mubhwe geniesama Ozone_ Mwambwaro Che mittoga JF Member Freyzem Paspii0 Madumbikaya Demi Powder Saint Ivuga Hassanjk matunduizi hahaha always done Zabron Hamis Shadow7 mdesi Msudu Kida ze great Barca Enthusiastic kitali Deinstein 01 Farolito Daudi1 Rozela Beira Boy NAMBA MOJA AJAYE NCHINI Mwami Ntale UMBEEE Vyamavingi Proved okiwira Sangamwalogesha Lupweko tungatagaga MwananchiOG Intuition Tumwesige senior Erickb52 GEBA2013 Pascal Mayalla adriz Manjagata Rabbon Rogojin The Idiot Mbaga Jr Infropreneur na wengine...
Ila naomba tusirudie kusema tuliyoyaongea. Hoja zetu za sasa tuzijenge kwenye vifungu hivyo vipya na tujibu swali hili:
"Je, Mwamba anayetajwa na Daudi na Isaya ni Petro? Mbona Petro alikuwa bado hajazaliwa wakati huo?"
Ukristo umejengwa kutoka kwa Yesu Jesus Christ, Yesu Kristo
wanaomuamini Kristo ndio wanaitwa wakristo
Yesu Kristo ndio alimwambia Petro
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."
kabla hakukua na Ukristo Baada ya Happ Ukristo Ulizaliwa
hatakama alirejsea mwamba na sehemu yoyote ile ila hakukua na Ukristo kabla.
Yesu alijenga kanisa la kikristo juu ya Petro na kumwambia
"Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."
Je ukatoliki umetikisika hadi leo ? haujawai hata siku moja au kwa bahati mbaya haujawahi
kanisa lilianza kama kanisa na limebaki bila jina ni " kanisa "
kama alivyosema Yesu juu ya mwamba huu nalijenga kanisa.
baada ya miaka mingi limejulikana kama kanisa la Roma lililoenea duniani
( Roman Catholic )
ikaanzatokea mgawanyiko ndani ya kanisa kukawa na kanisa la magharibi na la mashariki, kanisa hili na Orthodox
Bado La Roma likazidi ku dominate
baada ya miaka mingi zaidi ikatokea mgawanyiko ulioanza kuleta tofauti.
( hapo ni miaka ya 1500 kumbuka kanisa likikua stable kwa miaka yote hiyo )
baada ya mgawanyiko huo tuka pata kanisa kutoka kwa padre Martin Luther
huyu alikua padre aliyeweza kuleta mgawanyiko mkubwa
( ambapo baadae alijuta na kuomba msamaha kwa kuleta mgawanyiko kwenye kanisa)
baadhi ya migawanyiko ndo ilitambulika kua mgawanyiko wa kanisa huenda ilikwepo mingi isiyo ma madhara kwa kanisa
pia baada ya muda mwingi kwenda kuna madhehebu mengine yakaibuka kutoka huko kwingine mfano kutoka Lutheran etc
ila kanisa limebaki kama shina Kanisa Takatifu Katoliki La Mitume.
Bila kujali unacho amini ni ukweli usiopingika kua,
ukristo umejengwa kutokana na imani ya kumuamini Kristo.
na Kristo ndie aliyemuambia Petro maneno hayo
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."
Ukristo Ukaanza Rasmi, ?
kama anglican au kanisa ni lolote Tofauti na Catholic ndo lililoshika msingi wa Ukristo mtuambie ni kanisa Lipi turudi mwenye historia kusoma
ila historia inaeleza
Nami nasema ni Kanisa Takatifu Katoliki La Mitume ndo msingi wa Ukristo Duniani