Sio kweli
Pascal Mayalla
Wasomi wenzako wamejaribu kuthibitisha kwa kutaja kifungu cha Mathayo 16:18 kinachosema:
"Na mimi nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya huu mwamba nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."
Hicho kifungu hakithibitishi kwamba "Mwamba" ni Petro. Hebu tukichambue kwa undani:
Kwanza tuangalie maana ya majina: “Petro” na "Mwamba," kwa Kigiriki(lugha iliyotumika kwa sehemu kubwa kuandika Agano Jipya), Petro ni "
Petros" (mawe madogo au jiwe dogo), na Mwamba ni "
Petra" (Mwamba, Jabari imara au Jiwe kubwa).
Kwa maana hizo, Petro ni jiwe dogo, hastahili kuwa Jiwe Kubwa(Mwamba). Lakini Yesu katika
1 Wakorintho 10:4 anatajwa wazi kuwa ni Mwamba:
"wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea
mwamba wa roho uliowafuata; na
mwamba ule ulikuwa ni Kristo."
Mstari huo kwa tafsiri rahisi tunaweza kuuandika hivi: "Wewe Petro ni jiwe dogo. Mimi Yesu nitalijenga kanisa juu yangu mimi mwenyewe(Yesu) niliye Jiwe Kuu(Mwamba).
Ukisoma pia 1 Petro 2:6-8, Petro mwenyewe amenukuu maandiko yanayoonyesha kuwa Yesu ni Jiwe kuu la pembeni na Mwamba.
Hoja nyingine waliyoitoa Wasomi wenzako imejengwa kwenye kifungu cha Mathayo 16:19(
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni). Je, hizo funguo alipewa Petro tu?
Hapana. Mamlaka ya kufunga na kufungua walipewa wanafunzi wote – sio Petro peke yake.
Katika Mathayo 18:18 Yesu anawapa wanafunzi wote mamlaka ya kufunga na kufungua. "
Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni."
Kifungu hicho kinathibitisha wazi kwamba Yesu ametoa mamlaka hayo kwa Kanisa zima, sio kwa Petro tu.
Kindly offer another perspective, as the arguments presented by others have not adequately addressed my question.