Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Moja ya Matatizo makubwa ya wa Protestant ni kuwashawishi waumini wao wa amini wanachokihubiri kwa kutumia reference ya mafindisho Catholic, ili waichukie iman hiyo. Hata hapa huenda swali limeulizwa ili kila likjibiwa ulipinge ili ku justify uprotestant.
Kwa ushauri, ukienda pale vatcan km alivyosema mchungaji mmoja kuwa kuna ekari za documentary unaweza omba access kwa utaratitibu uliowekwa ujipatie maarifa, hata hawakatazi kabisa.
Besides, Mungu ni mpana kuliko Biblia yenye vitabu 66, maana vingine mlivikataa eti havina uvuvio wa Roho Mtakatifu, hapo ni binadamu tu kwa maoni yao waliona hivyo. Pia kuna Gospels nyingine kibao km the Gospel of Mary, Peter, Baranabas, Thomas etc hazimo kwa Bible ambazo kanisa Katoliki lilijichukulia dondoo zake nakuzitumia kuanda Katekisimu ya kanisa.
La ziada tu nikusaidie, usione wakatoliki wanafanya jambo fulani kwa utaratibu fulani ukadhani wamekurupuka tu na kuanzisha hapana wana misingi yao ambayo wanaisimamia.
Mfano wanasali Rozary of Mary kitu ambacho kinapingwa na wanao protest hawajawahi acha wanaendelea wana misingi yao na wanajua wapi ilianzia na kwanini.
Anyhow ya Ngoswe mwachie Ngoswe
 
Hakuna uthibitisho wa Moja kwa Moja kuwa mtume Petro aliwahi kuwa Askofu wa rumi/roma.

Historia ya kanisa inaonyesha kuwa kanisa liliishi pamoja kwa miaka 1000 mpaka ulipotokea mgogoro wa Kiimani katika mkutano wa Nikea.

Kanisa likagawanyika katika vipande viwili.
1. ORTHODOX CATHOLIC CHURCH
2.ROMAN CATHOLIC CHURCH.

Kwa majibu wa mapokeo ya Roman Catholic Church wanamini Petro ni Papa /Askofu wa kwanza wa jimbo la Rumi.

Wengine hawaamini ivo, Biblia haisemi kwa uwazi sana juu ya hilo, Ila kwa Msaada zaidi soma kitabu cha matendo ya Mitume ukiwa na ufahamu Huru.
 
Ndugu zangu wa Kanisa kubwa duniani, Kanisa Katoliki - poleni sana kwa msiba mzito. Wakati maombolezo yakiendelea, naomba tuongee kiutu uzima; kwa heshima na upendo.

Kwanza ninawapongeza: mkiwa Kanisani, mnaonyesha heshima kubwa kwa Mungu. Sasa naomba mnijibu swali hilo: Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Nimesikia mnafundisha kwamba Mtume Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu kuwa msingi wa Kanisa au Papa wa kwanza. Mnanukuu Mathayo 16:18 na kusema kwamba katika Andiko hilo Yesu alimwambia Petro, “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.” Kwa tafsiri yenu, “mwamba” huo ni Petro mwenyewe, na hivyo mnamuona kama Papa wa kwanza. Mnaamini kwamba, mamlaka ya Petro kama kiongozi wa mitume yaliendelezwa na Mapapa waliomfuata, wakiwa viongozi wa juu wa Kanisa la Kristo duniani. Ni kweli?

Kama ni kweli, mbona mtazamo wa Kiprostestanti unatofautiana na mafundisho yenu. Waprotestanti wanasisitiza kuwa msingi wa Kanisa sio mtu binafsi, bali ni Yesu Kristo mwenyewe (1 Wakorintho 3:11), na kwamba “mwamba” aliouzungumzia Yesu ni Yeye mwenyewe(Yesu) kama Petro alivyokiri: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16).

Kwa mtazamo wa Kiprostestanti, Petro hakuwa Papa, kwa sababu hakuna ushahidi wa kibiblia unaoonyesha kuwa alipewa mamlaka ya kipekee juu ya mitume wengine. Na wakati wa Kanisa la kwanza mfumo uliopo leo wa kipapa, haukuwepo.

Waprotestanti wanaeleza tena kwamba Viongozi wa kwanza wa Kanisa walifanya maamuzi yao kwa ushirikiano (Mdo 15), sio kwa mamlaka ya mtu mmoja(Papa). Wanasimama na Andiko la Waefeso 5:23 linalosema kwamba Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa. Wanaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeliongoza Kanisa lote sasa, na sio kiongozi mmoja wa kimwili. Wananukuu Yohana 16:13
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote."

Hoja hizo mnazijibuje?

Ntashukuru sana nikipata majibu ya swali langu na majibu kuhusu hoja hizo za Kiprotestanti. Majibu yajengwe kwenye Maandiko Matakatifu(Biblia). Tumsifu Yesu Kristo.
Tatizo nyie Wambolostant huwa mmejiandaa kubishana hata kabla hatujajibu nyie tayari mna majibu yenu hivyo hata tulikuambia kwamba Pedro ndiye Papa wa kwanza utatubishia!
 
uporostentanti ulianza lini na ukatoliki ulianza lini

Yesu alivyoondoka wafuasi wake walikua na early comunity ambayo ndio kanisa ka kwanza kutokana ni wafuasi wa kristo wala hawakujulikana kama wa kristo ila ilokua ni early comunity ambayo ilitokana na wafuasi wa kristo wakifuata mafundisho ya Yesu
Petro alikua kiongozi


baada ya kuendelea na kuendelea ba kuendelea walikuja jua wakitambulika kama wakristo na baada ya kukua na kukua kuna watu walianza jujitenga kwa sababu mbalimbali

tukapata wa Lutheran kutoka kwa padre martin Luther nawengine na wengine hadi sasa. ( hao wote ndo wa prostentati unaowasemea )

je petro alikua kiongozi wa kanisa lipi


actually sioni umuhimu wa kufuata sana dini fulani cha muhimu zaidi ni maisha yako

ila kuhusu historia katoliki ni shina na makanisa mengine yote ni matawi tu na wote mnajua hilo


biblia unayotumia wewe uliyoqute hapo imepangwa hivyo ilivyo na kanisa katoliki


jumla ya injili zote ni zaidi ya 12 hadi ishirini ila kanisa katoliki liloteua injili nne zikae kwenye bibilia, ratiba zote za kikanisa hata pasaka uliyosherehekea jana imepangwa na kanisa katoliki

callender unayoitumia saivi inaitwa gregorian callender imepangwa na papa Gregory

kwanini kanisa katoliki lina nguvu ya kufanya yote hayo na nyie mkafuata kwasababu ndo la kwanza na ndo lenye mizizi ya ukristo

je utawezaje kuongelea historia ya ukristo bila kuzungumzia kanisa katoliki. ?

"juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa na halito tikisika"

Tangu ukristo umeanza kanisa katoliki halijawai kutikisika wala kua namba mbili, ni namba moja kwa miaka elfu mbili na halitotikisika hadi dunia iishe
 
Biblia ni hekaya kama hekaya zingine.

Hiyo Church history haiondoi ukweli kwamba Biblia ni hekaya.

Yesu hajawahi kuwepo.

Hao wanaojiita mapapa ni wajanja fulani waliokaa chini kuunda dini ya ukristo kulaghai wajinga.
Utaifananisha na zile hadithi za Mwamedi? Kababu kale kalikuwaga kaongo kaongo sana!
 
Waprotestanti nimewasikia kwa undani. Ila Wakatoliki sijasikia hoja zao kwa kina. Ndio sababu natafuta kusikia na kuthibitisha kutoka kwenye vinywa vyao wenyewe. Halafu kwa taarifa yako, Wakatoliki wanasema hata Mtume Petro alizikwa kwenye Kanisa lao, Vatican! Kama ni hivyo, hao si ndio wenye majibu mazuri ya maswali yangu?

Nimesikia pia kwamba baada ya Mtume Petro, Wakatoliki wanaamini kuwa Papa aliyefuata alikuwa Linus – ambaye anatajwa kama Papa wa pili (mnamo mwaka 67–76 BK).

Orodha ya Mapapa wa awali kwa mtazamo wa RC ni kama ifuatavyo:
Mtume Petro (c. 33–67)
Linus (c. 67–76)
Anacletus (au Cletus) (c. 76–88)
Clement I (c. 88–97)
Evaristus (c. 97–105)

Taarifa hizo sina uhakika nazo. Wakiniambia wenyewe na kunipa uthibitisho nitashukuru sana.

Hii ndo list ya Mapapa tangu wa kwanza hadi 266. Huhitaji kutumia nguvu. Google tu utaona. Na kanisa katoliki linajua sana kuhifadhi history yake
 
HAKUNA UPAPA ALIOUACHA MTUME YEYOTE!

PAPA NI KIONGOZI WA KUZIMU ANAEWAKILISHA HUKU DUNIANI KWA KUWEKA TAWALA ZOTE ZILIZOPO BILA MAPATANO NAE HUWEZI TAWALA!!!

SASA JE PETRO ALIKUA NA MAPATANO GANI NA SERIKALI YA KIRUMI!!?
Hiv hii Biblia ninani aliyeihariri na kupangilia vitabu na kuifadhi mpaka leo
 

Hii ndo list ya Mapapa tangu wa kwanza hadi 266. Huhitaji kutumia nguvu. Google tu utaona. Na kanisa katoliki linajua sana kuhifadhi history yake
Nahitaji ushahidi wa Biblia. Tukianzia kwa Petro, ni nani aliyempa cheo cha Upapa? Wikipedia sio Biblia.
 
Back
Top Bottom