Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Unaumwa wewe! Ni Biblia gani inazungumzia upadre, uaskofu, uchungaji?
Duh, wewe inaonekana Biblia hujawahi kuisoma kabisa. Katika vifungu vifuatavyo, Askofu na Mchungaji wanatajwa:
Waefeso 4:11
"Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na waalimu."

1 Timotheo 3:1-2
"Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, mwenye busara, anayeheshimika, mkaribishaji wageni, ajuaye kufundisha;"

Ila Papa sijaona, ndo sababu nahitaji mnipatie vifungu
 
Ndugu zangu wa Kanisa kubwa duniani, Kanisa Katoliki - poleni sana kwa msiba mzito. Wakati maombolezo yakiendelea, naomba tuongee kiutu uzima; kwa heshima na upendo.

Kwanza ninawapongeza: mkiwa Kanisani, mnaonyesha heshima kubwa kwa Mungu. Sasa naomba mnijibu swali hilo: Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Nimesikia mnafundisha kwamba Mtume Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu kuwa msingi wa Kanisa au Papa wa kwanza. Mnanukuu Mathayo 16:18 na kusema kwamba katika Andiko hilo Yesu alimwambia Petro, “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.” Kwa tafsiri yenu, “mwamba” huo ni Petro mwenyewe, na hivyo mnamuona kama Papa wa kwanza. Mnaamini kwamba, mamlaka ya Petro kama kiongozi wa mitume yaliendelezwa na Mapapa waliomfuata, wakiwa viongozi wa juu wa Kanisa la Kristo duniani. Ni kweli?

Kama ni kweli, mbona mtazamo wa Kiprostestanti unatofautiana na mafundisho yenu. Waprotestanti wanasisitiza kuwa msingi wa Kanisa sio mtu binafsi, bali ni Yesu Kristo mwenyewe (1 Wakorintho 3:11), na kwamba “mwamba” aliouzungumzia Yesu ni Yeye mwenyewe(Yesu) kama Petro alivyokiri: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16).

Kwa mtazamo wa Kiprostestanti, Petro hakuwa Papa, kwa sababu hakuna ushahidi wa kibiblia unaoonyesha kuwa alipewa mamlaka ya kipekee juu ya mitume wengine. Na wakati wa Kanisa la kwanza mfumo uliopo leo wa kipapa, haukuwepo.

Waprotestanti wanaeleza tena kwamba Viongozi wa kwanza wa Kanisa walifanya maamuzi yao kwa ushirikiano (Mdo 15), sio kwa mamlaka ya mtu mmoja(Papa). Wanasimama na Andiko la Waefeso 5:23 linalosema kwamba Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa. Wanaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeliongoza Kanisa lote sasa, na sio kiongozi mmoja wa kimwili. Wananukuu Yohana 16:13
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote."

Hoja hizo mnazijibuje?

Ntashukuru sana nikipata majibu ya swali langu na majibu kuhusu hoja hizo za Kiprotestanti. Majibu yajengwe kwenye Maandiko Matakatifu(Biblia). Tumsifu Yesu Kristo.

Pope ina maana baba..au kiongozi. Ni neno la kilatini na kimsingi linampa cheo cha kuwa kiongozi. Msingi wa kanisa Katoliki ni Yesu Kristu wenyewe.

Yesu aliliacha kanisa katika utaratibu. Ndio maana alimwambia Mtume Petro tena mara tatu, awachunge kondoo zake. Sio kwamba yeye ametelekeza kanisa, ila aliliacha katika utaratibu ambao uwe enedelevu.

Waprotesant, sababu ya kukosekana kwa mfumo kama huo, watu wengi wameanzisha makanisa yao, na kuingiza yale wanayoyaona yanawafaa wao.

Mfano siku ya pentekoste, watu walinena kwa lugha mbalimbali ila walisikilizana. Siku hizi wanaonena kwa vinywa wao wenyewe hawajui wanaongea nini na hata wanaosikiliza. Yna vionjo vyetu vya kibinadamuna mengi yanakosa mifumo thabiti ya kiungozi.

Na kukusaidia, kwenye kalamu ya mwisho Yesu aliyofanya na wanafunzi wake, aliweka PACT. Alimega mkate usio na chachu na kugeuza divai, iwe agano la milele la sadaka yake msalabani. Baadae mtume Paul akasema Yesu ni yeye yule yule jana leo na milele.

Hivyo basi, mpaka kesho, kwenye ibada ya misa takatifu, toka enzi na enzi, sadaka ile ile aliyofanya Yesu, iko hai na tunamkumbuka Yesu aliye hai.

Ni wakatoliki pekee ndio wanaadhimisha ibada aliyofanya Yesu siku ya Alhamisi Kuu. Unajua maana ya agano la milele alilosema Yesu?
 
Ndugu zangu wa Kanisa kubwa duniani, Kanisa Katoliki - poleni sana kwa msiba mzito. Wakati maombolezo yakiendelea, naomba tuongee kiutu uzima; kwa heshima na upendo.

Kwanza ninawapongeza: mkiwa Kanisani, mnaonyesha heshima kubwa kwa Mungu. Sasa naomba mnijibu swali hilo: Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Nimesikia mnafundisha kwamba Mtume Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu kuwa msingi wa Kanisa au Papa wa kwanza. Mnanukuu Mathayo 16:18 na kusema kwamba katika Andiko hilo Yesu alimwambia Petro, “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.” Kwa tafsiri yenu, “mwamba” huo ni Petro mwenyewe, na hivyo mnamuona kama Papa wa kwanza. Mnaamini kwamba, mamlaka ya Petro kama kiongozi wa mitume yaliendelezwa na Mapapa waliomfuata, wakiwa viongozi wa juu wa Kanisa la Kristo duniani. Ni kweli?

Kama ni kweli, mbona mtazamo wa Kiprostestanti unatofautiana na mafundisho yenu. Waprotestanti wanasisitiza kuwa msingi wa Kanisa sio mtu binafsi, bali ni Yesu Kristo mwenyewe (1 Wakorintho 3:11), na kwamba “mwamba” aliouzungumzia Yesu ni Yeye mwenyewe(Yesu) kama Petro alivyokiri: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16).

Kwa mtazamo wa Kiprostestanti, Petro hakuwa Papa, kwa sababu hakuna ushahidi wa kibiblia unaoonyesha kuwa alipewa mamlaka ya kipekee juu ya mitume wengine. Na wakati wa Kanisa la kwanza mfumo uliopo leo wa kipapa, haukuwepo.

Waprotestanti wanaeleza tena kwamba Viongozi wa kwanza wa Kanisa walifanya maamuzi yao kwa ushirikiano (Mdo 15), sio kwa mamlaka ya mtu mmoja(Papa). Wanasimama na Andiko la Waefeso 5:23 linalosema kwamba Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa. Wanaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeliongoza Kanisa lote sasa, na sio kiongozi mmoja wa kimwili. Wananukuu Yohana 16:13
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote."

Hoja hizo mnazijibuje?

Ntashukuru sana nikipata majibu ya swali langu na majibu kuhusu hoja hizo za Kiprotestanti. Majibu yajengwe kwenye Maandiko Matakatifu(Biblia). Tumsifu Yesu Kristo.
Pascal Mayalla
 
kwani cheo cha papa nani alikianzisha? mbona kwenye Bibilia sijakutana na cheo cha mtu aitwaye Papa, mimi najua Papa ni samaki mkubwa wa Baharini
 
Mathayo 16 : 18

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
 
Unauliza Swali kwa Catholic alafu wakati huohuo unasema "Waprotestant wenzenu" are you serious? Unaelewa maana ya neno "Protestant", Hao walitofautiana mtazamo hivyo wakajitenga na hiyo ndiyo sababu kuu, Sasa iweje utake tuwe na mtazamo sawa na protestant?

Pili, Yesu alimpoint Petro na kumueleze kwamba "Wewe Ndiye Petro" Hakusema "Mimi ndiye Petro" alimnyooshea kidole Petro,

Mathayo 16 : 18

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

Yohana 21 : 15

Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.

Msingi wa Kanisa ni Kristu na Kiti cha Mtume Petro kama Mlishi wa Kondoo zake kinabaki Palepale. Petro aliyeitwa Simoni alibadilishwa Jina na kukabidhiwa usimamizi wa Kanisa la Kristu, Ndiyo maana kila Papa Lazima atambulike kwa Jina Jipya. Papa ni "Vicar of Christ" Yaani 'Mchungi wa kondoo wa Bwana' Na kiti hicho kimerithiwa Tangu Petro mpaka Fransisko, na sasa tunaelekea kumpata Mchungi mpya atakayekalia kiti cha Petro Mtume.

Tumsifu Yesu Kristu
 
Ndugu zangu wa Kanisa kubwa duniani, Kanisa Katoliki - poleni sana kwa msiba mzito. Wakati maombolezo yakiendelea, naomba tuongee kiutu uzima; kwa heshima na upendo.

Kwanza ninawapongeza: mkiwa Kanisani, mnaonyesha heshima kubwa kwa Mungu. Sasa naomba mnijibu swali hilo: Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Nimesikia mnafundisha kwamba Mtume Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu kuwa msingi wa Kanisa au Papa wa kwanza. Mnanukuu Mathayo 16:18 na kusema kwamba katika Andiko hilo Yesu alimwambia Petro, “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.” Kwa tafsiri yenu, “mwamba” huo ni Petro mwenyewe, na hivyo mnamuona kama Papa wa kwanza. Mnaamini kwamba, mamlaka ya Petro kama kiongozi wa mitume yaliendelezwa na Mapapa waliomfuata, wakiwa viongozi wa juu wa Kanisa la Kristo duniani. Ni kweli?

Kama ni kweli, mbona mtazamo wa Kiprostestanti unatofautiana na mafundisho yenu. Waprotestanti wanasisitiza kuwa msingi wa Kanisa sio mtu binafsi, bali ni Yesu Kristo mwenyewe (1 Wakorintho 3:11), na kwamba “mwamba” aliouzungumzia Yesu ni Yeye mwenyewe(Yesu) kama Petro alivyokiri: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16).

Kwa mtazamo wa Kiprostestanti, Petro hakuwa Papa, kwa sababu hakuna ushahidi wa kibiblia unaoonyesha kuwa alipewa mamlaka ya kipekee juu ya mitume wengine. Na wakati wa Kanisa la kwanza mfumo uliopo leo wa kipapa, haukuwepo.

Waprotestanti wanaeleza tena kwamba Viongozi wa kwanza wa Kanisa walifanya maamuzi yao kwa ushirikiano (Mdo 15), sio kwa mamlaka ya mtu mmoja(Papa). Wanasimama na Andiko la Waefeso 5:23 linalosema kwamba Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa. Wanaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeliongoza Kanisa lote sasa, na sio kiongozi mmoja wa kimwili. Wananukuu Yohana 16:13
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote."

Hoja hizo mnazijibuje?

Ntashukuru sana nikipata majibu ya swali langu na majibu kuhusu hoja hizo za Kiprotestanti. Majibu yajengwe kwenye Maandiko Matakatifu(Biblia). Tumsifu Yesu Kristo.
Ni uongo wa wakatoliki, Biblia haisemi hivyo.
 
Wengine hawaamini ivo, Biblia haisemi kwa uwazi sana juu ya hilo, Ila kwa Msaada zaidi soma kitabu cha matendo ya Mitume ukiwa na ufahamu Huru.
Kitabu cha Matendo ya mitume hakijamtaja Petro kama Papa...
 
Ingawa haifahamiki kiundani kuwa Papa wa kwanza ni Simon Petro, lakini Yesu alitaka Petro awe na mamlaka kama Papa katika Ukristo:

Utawala wa Papa na Vatican umefanya jitihada kubwa kuutangaza na kuueneza Ukristo kuliko utawala wowote ule ulio katika imani ya Kikristo:

Tukianzia kabla ya ukoloni, Wamisionary wengi wa kwanza kuja maeneo mengi ya Afrika walikuwa ni Wakatoriki chini ya Utawala wa Papa.
Leo Waafrika wengi ni wakristo kwa juhudi za Papa:

Wakati wa Ukoloni utawala wa Papa uliendelea kueneza dini ya Kikristo kwa kujiwekea mamlaka maeneo ambayo waliyatawala ili kuilinda dini ya Kikristo:

Ndio maana utaona katika kila Nchi, kuna Jimbo, Parokia, Kigango, kama mamlaka ya kiutawala ya Ki-Papa ili kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Wakristo katika maeneo husika:

Katika maeneo hayo ya Mamlaka Papa alihakikisha kunajengwa Makanisa na huduma za Kijamii kama Hospitali, Shule, Vyuo na taasisi nyingine za kimaendeleo ili kuwahudumia Wakristo na raia wengine:

Pia mamlaka ya Upapa ilihakikisha inajiingiza katika mahusiano na Kila serikali ya nchi ili kuupa nguvu Ukristo:

Hivyo Papa alihakikisha kila nchi ina mwakilishi toka makao makuu ya Upapa Vatikan {Ubalozi wa Vatikan}

Katika dunia ya sasa Papa anaendela kutumia njia za Kidiplomasia, kimataifa ili kuulinda na kuueneza Ukristo katika nchi ambazo zimeupiga marufuku Ukristo:

Nchi kama Cuba, China, North Korea, na zile zenye utawala wa Kiislamu, Papa anaendelea kuzishawishi ili ziupokee Ukristo na anaendelea kufanikiwa siku hadi siku:

Leo nchi kama Cuba, China, Saudi Arabia, Somalia, zimeanza kuupokea Ukristo kwa Nguvu ya Upapa:

Mamlaka ya Upapa yana nguvu na ushawishi mkubwa kimataifa katika nyanja zote za maisha, ndio mana watumishi wake, Mapadre, Maaskofu nk, ni wasomi wabobevu katika fani zote:

Pamoja ya kuwa Papa kama binadamu na ana mapungufu yake, lakini Mamlaka ya Upapa ina utawala makini, na pia ina nguvu na ushawishi mkubwa katika hii dunia kama Yesu Kristo alivyo msimika
Simon Petro:

Mathayo 16:18
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
 
Mathayo 16 : 18

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Asante MwananchiOG kwa mstari huo.
Huo mstari(Mathayo 16:18) hauthibitishi kwamba "Mwamba" ni Petro. Hebu tuuchambue kwa kina:

"Na mimi nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya huu mwamba nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."

Kwanza tuangalie maana ya majina: “Petro” na "Mwamba," kwa Kigiriki(lugha iliyotumika kwa sehemu kubwa kuandika Agano Jipya), Petro ni "Petros" (mawe madogo au jiwe dogo linalohamishika), na Mwamba ni "Petra" (Jabari imara au Jiwe kubwa).

Kwa maana hizo, Petro ni jiwe dogo. Hastahili kuwa Jiwe Kubwa(Mwamba). Lakini Yesu katika 1 Wakorintho 10:4 anatajwa wazi kuwa ni Mwamba:

"wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo."

Kwahiyo mstari ulioutaja, kwa tafsiri rahisi tunaweza kuuandika hivi: "Wewe Petro ni jiwe dogo. Mimi Yesu nitalijenga kanisa juu yangu mimi mwenyewe(Yesu) niliye Jiwe Kuu(Mwamba).

Ukisoma pia 1 Petro 2:6-8, Petro mwenyewe amenukuu maandiko yanayoonyesha kuwa Yesu ni Jiwe kuu la pembeni na Mwamba.

Haya, twende kwenye hoja yako ya pili uliyoijenga kwenye Mathayo 16:19(Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni). Je, hizo funguo alipewa Petro tu? Hapana. Mamlaka ya kufunga na kufungua walipewa wanafunzi wote – sio Petro peke yake.

Katika Mathayo 18:18 Yesu anawapa wanafunzi wote mamlaka ya kufunga na kufungua. "Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni."

Mstari huo unathibitisha wazi kwamba Yesu ametoa mamlaka hayo kwa Kanisa zima, sio kwa Petro tu.
 
Ingawa haifahamiki kiundani kuwa Papa wa kwanza ni Simon Petro, lakini Yesu alitaka Petro awe na mamlaka kama Papa katika Ukristo:

Utawala wa Papa na Vatican umefanya jitihada kubwa kuutangaza na kuueneza Ukristo kuliko utawala wowote ule ulio katika imani ya Kikristo:

Tukianzia kabla ya ukoloni, Wamisionary wengi wa kwanza kuja maeneo mengi ya Afrika walikuwa ni Wakatoriki chini ya Utawala wa Papa.
Leo Waafrika wengi ni wakristo kwa juhudi za Papa:

Wakati wa Ukoloni utawala wa Papa uliendelea kueneza dini ya Kikristo kwa kujiwekea mamlaka maeneo ambayo waliyatawala ili kuilinda dini ya Kikristo:

Ndio maana utaona katika kila Nchi, kuna Jimbo, Parokia, Kigango, kama mamlaka ya kiutawala ya Ki-Papa ili kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Wakristo katika maeneo husika:

Katika maeneo hayo ya Mamlaka Papa alihakikisha kunajengwa Makanisa na huduma za Kijamii kama Hospitali, Shule, Vyuo na taasisi nyingine za kimaendeleo ili kuwahudumia Wakristo na raia wengine:

Pia mamlaka ya Upapa ilihakikisha inajiingiza katika mahusiano na Kila serikali ya nchi ili kuupa nguvu Ukristo:

Hivyo Papa alihakikisha kila nchi ina mwakilishi toka makao makuu ya Upapa Vatikan {Ubalozi wa Vatikan}

Katika dunia ya sasa Papa anaendela kutumia njia za Kidiplomasia, kimataifa ili kuulinda na kuueneza Ukristo katika nchi ambazo zimeupiga marufuku Ukristo:

Nchi kama Cuba, China, North Korea, na zile zenye utawala wa Kiislamu, Papa anaendelea kuzishawishi ili ziupokee Ukristo na anaendelea kufanikiwa siku hadi siku:

Leo nchi kama Cuba, China, Saudi Arabia, Somalia, zimeanza kuupokea Ukristo kwa Nguvu ya Upapa:

Mamlaka ya Upapa yana nguvu na ushawishi mkubwa kimataifa katika nyanja zote za maisha, ndio mana watumishi wake, Mapadre, Maaskofu nk, ni wasomi wabobevu katika fani zote:

Pamoja ya kuwa Papa kama binadamu na ana mapungufu yake, lakini Mamlaka ya Upapa ina utawala makini, na pia ina nguvu na ushawishi mkubwa katika hii dunia kama Yesu Kristo alivyo msimika
Simon Petro:

Mathayo 16:18
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Che mittoga
Mstari ulioutaja hauthibitishi kuwa Mwamba ni Petro. Soma kwa undani jinsi nilivyouchambua mstari huo katika post #74 na kuthibitisha kuwa Mwamba ni Yesu mwenyewe.
 
Ni kweli!.
P
Sio kweli Pascal Mayalla
Wasomi wenzako wamejaribu kuthibitisha kwa kutaja kifungu cha Mathayo 16:18 kinachosema: "Na mimi nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya huu mwamba nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."

Hicho kifungu hakithibitishi kwamba "Mwamba" ni Petro. Hebu tukichambue kwa undani:

Kwanza tuangalie maana ya majina: “Petro” na "Mwamba," kwa Kigiriki(lugha iliyotumika kwa sehemu kubwa kuandika Agano Jipya), Petro ni "Petros" (mawe madogo au jiwe dogo), na Mwamba ni "Petra" (Mwamba, Jabari imara au Jiwe kubwa).

Kwa maana hizo, Petro ni jiwe dogo, hastahili kuwa Jiwe Kubwa(Mwamba). Lakini Yesu katika
1 Wakorintho 10:4 anatajwa wazi kuwa ni Mwamba:

"wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo."

Mstari huo kwa tafsiri rahisi tunaweza kuuandika hivi: "Wewe Petro ni jiwe dogo. Mimi Yesu nitalijenga kanisa juu yangu mimi mwenyewe(Yesu) niliye Jiwe Kuu(Mwamba).

Ukisoma pia 1 Petro 2:6-8, Petro mwenyewe amenukuu maandiko yanayoonyesha kuwa Yesu ni Jiwe kuu la pembeni na Mwamba.

Hoja nyingine waliyoitoa Wasomi wenzako imejengwa kwenye kifungu cha Mathayo 16:19(Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni). Je, hizo funguo alipewa Petro tu? Hapana. Mamlaka ya kufunga na kufungua walipewa wanafunzi wote – sio Petro peke yake.

Katika Mathayo 18:18 Yesu anawapa wanafunzi wote mamlaka ya kufunga na kufungua. "Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni."

Kifungu hicho kinathibitisha wazi kwamba Yesu ametoa mamlaka hayo kwa Kanisa zima, sio kwa Petro tu.

Kindly offer another perspective, as the arguments presented by others have not adequately addressed my question.
 
Back
Top Bottom