Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

yesu na mitume nani mkubwa ? maana unazani labda mtume ni mtu flani wa ajabu sana ndio unavyozania

hebu niambie mtume na yesu nani mkubwa kama jibu ni yesu nenda ukasome habari zake kwenye biblia na ufanya matendo kama yake kama ulimuona akiabudu sanamy na wewe abudu kama ulimuona akimuombea maria nawe hivyo hivyo na kama pia petro kwenye biblia aliabudu sanamu na wewe abudu na kama alisherekea kuzaliwa kwa yesu au kufufuka kwake na wewe nenda ukafanye. lakini kama hakufanya wewe utachagua mwenyewe hatima yako ipo hapo.
"nikasome kwenye biblia"

biblia ime haririwa na kupangwa hivyo na Catholic au hujui hilo

Catholic ina mambo mengi ambayo haikuweka kwenye biblia kwa sababu mbali mbali na imebaki kua mapokeo ya Kanisa

mambo mengine unayoongelea sanamu n.k, ni uelewa wako potofu na mdogo juu ya maswala ya Kanisa Katoliki
 
sasa kufanya maamuzi ndio kuwa kiongozi kila mtu alifanya maamuzi una akili ndogo sana

yesu kuwatuma mitume alifanya maamuzi pia

mitume kukubali kutumwa walifanya maamuzi pia kiufupi hujui unachokiongea na hujui vitu vingi tatizo linaanzia hapo
Mjadala wowote unaohusu imani ni lazima wote mnaojadili muongozwe na Roho Wa Mungu,wewe umepungukiwa na hekima ya Kimungu,kilichokufanya umwite mwenzako ana akili ndogo sana ni nini?

Wewe unayejiita Genius Man nadiriki kusema huu mjadala kwako ni mkubwa maana unaamini unajua kila kitu,huna lugha ya majadiliano na unataka ukuu ambao hauna na hii ni homa mnayo wasabato mnaoabudu siku badala ya Mungu.
 
"nikasome kwenye biblia"

biblia ime haririwa na kupangwa hivyo na Catholic au hujui hilo

Catholic ina mambo mengi ambayo haikuweka kwenye biblia kwa sababu mbali mbali na imebaki kua mapokeo ya Kanisa

mambo mengine unayoongelea sanamu n.k, ni uelewa wako potofu na mdogo juu ya maswala ya Kanisa Katoliki
Ok, nimekuelewa kumbe unafanya ushabiki kwasababu unamtizamo hasi kuhusu mungu, kuna makampuni mengi yanachapisha biblia hivi leo hata mimi naweza kununua mashine ya kuchapisha biblia tena ni rahisi kuliko.

Nachoona kwako umepungukiwa sana uwezo wa akili na huna unachokijua sasa cha kufanya tufunge haya mabishano maana mimi sio mbumbumbu.

kakae na wenzako muanze kudanganyana na haya mambo ya vijiweni na ushabiki wa usiokuwa na maana. hivyo nipo sahihi kusema huna akili
 
Mjadala wowote unaohusu imani ni lazima wote mnaojadili muongozwe na Roho Wa Mungu,wewe umepungukiwa na hekima ya Kimungu,kilichokufanya umwite mwenzako ana akili ndogo sana ni nini?

Wewe unayejiita Genius Man nadiriki kusema huu mjadala kwako ni mkubwa maana unaamini unajua kila kitu,huna lugha ya majadiliano na unataka ukuu ambao hauna na hii ni homa mnayo wasabato mnaoabudu siku badala ya Mungu.
samahani sana, hata biblia kuna nukuu zinazo wataja watu flani ni vipofu, au hawana hekima hivyo kwa kipimo changu hili neno huna akili limetamkwa kwa mtu sahihi, kama mtu hana kitu flani ukimwambia huna hiki ni sahihi kama hana na sio tusi mfano naweza kukyambia wewe "huna gari, huna nyumba, huna nguo" yote haya ni maneno yasiyokuwa na shida. inategemea na uelewa wako kunielewa hivyo nipo sahihi
 
Che mittoga
Mstari ulioutaja hauthibitishi kuwa Mwamba ni Petro. Soma kwa undani jinsi nilivyouchambua mstari huo katika post #74 na kuthibitisha kuwa Mwamba ni Yesu mwenyewe.
Kila mtu afuate uchambuzi wake dada. Kuchambua kwako haimaanishi uko sahihi. Ndio maana bible iko katika mafumbo na mapokeo kadri utakavyoongozwa ndivyo sahihi. Waache wakatoliki wamuite papa wa kwanza kua ni Petro mtume maana haimdhuru mtu.
 
Ndugu zangu wa Kanisa kubwa duniani, Kanisa Katoliki - poleni sana kwa msiba mzito. Wakati maombolezo yakiendelea, naomba tuongee kiutu uzima; kwa heshima na upendo.

Kwanza ninawapongeza: mkiwa Kanisani, mnaonyesha heshima kubwa kwa Mungu. Sasa naomba mnijibu swali hilo: Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?

Nimesikia mnafundisha kwamba Mtume Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu kuwa msingi wa Kanisa au Papa wa kwanza. Mnanukuu Mathayo 16:18 na kusema kwamba katika Andiko hilo Yesu alimwambia Petro, “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.” Kwa tafsiri yenu, “mwamba” huo ni Petro mwenyewe, na hivyo mnamuona kama Papa wa kwanza. Mnaamini kwamba, mamlaka ya Petro kama kiongozi wa mitume yaliendelezwa na Mapapa waliomfuata, wakiwa viongozi wa juu wa Kanisa la Kristo duniani. Ni kweli?

Kama ni kweli, mbona mtazamo wa Kiprostestanti unatofautiana na mafundisho yenu. Waprotestanti wanasisitiza kuwa msingi wa Kanisa sio mtu binafsi, bali ni Yesu Kristo mwenyewe (1 Wakorintho 3:11), na kwamba “mwamba” aliouzungumzia Yesu ni Yeye mwenyewe(Yesu) kama Petro alivyokiri: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16).

Kwa mtazamo wa Kiprostestanti, Petro hakuwa Papa, kwa sababu hakuna ushahidi wa kibiblia unaoonyesha kuwa alipewa mamlaka ya kipekee juu ya mitume wengine. Na wakati wa Kanisa la kwanza mfumo uliopo leo wa kipapa, haukuwepo.

Waprotestanti wanaeleza tena kwamba Viongozi wa kwanza wa Kanisa walifanya maamuzi yao kwa ushirikiano (Mdo 15), sio kwa mamlaka ya mtu mmoja(Papa). Wanasimama na Andiko la Waefeso 5:23 linalosema kwamba Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa. Wanaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeliongoza Kanisa lote sasa, na sio kiongozi mmoja wa kimwili. Wananukuu Yohana 16:13
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote."

Hoja hizo mnazijibuje?

Ntashukuru sana nikipata majibu ya swali langu na majibu kuhusu hoja hizo za Kiprotestanti. Majibu yajengwe kwenye Maandiko Matakatifu(Biblia). Tumsifu Yesu Kristo.

Sawa, kwa kukazia comment ya Member Namba Moja papa ni mwakilishi wa Devil mwenyewe. Kuna CODE: zinasema huyu ndie Pope wa mwisho anaekuja ni Anti Christ au mpinga Kristo, ila atakuwa amepoa sana miaka kibao akiwa kama pope wa kawaida halafu atakuwa "activated" kuanza sasa kukamilisha New World Order na ile 666.
 
Mjadala wowote unaohusu imani ni lazima wote mnaojadili muongozwe na Roho Wa Mungu,wewe umepungukiwa na hekima ya Kimungu,kilichokufanya umwite mwenzako ana akili ndogo sana ni nini?

Wewe unayejiita Genius Man nadiriki kusema huu mjadala kwako ni mkubwa maana unaamini unajua kila kitu,huna lugha ya majadiliano na unataka ukuu ambao hauna na hii ni homa mnayo wasabato mnaoabudu siku badala ya Mungu.
Wasabato ninawashangaa zaidi kwenye kitu kimoja jinsi jumamosi walivyoipa heshima kubwa

lakini je jumamosi imetokanaje ?

hii callender tunayoitumia saivi ilipangwa hivi na papa Gregory miaka ya 1500 huko
Screenshot_20250423-145916.png

iliyokua inatumia kabla, jumamosi haijua hii yaani zimepishana, na sababu za kubadilisha zipo ni nyingi

kanisa ka wasabato limeanza miaka ya 1800
Screenshot_20250423-150005.png

wamekuta hii kalender iliyoanzishwa na papa miaka 300 nyuma tayari inatumika

sasa inakuaje unaiabudu siku kwa nguvu hivi wakati kalende inavyopangwa ingeweza kuwekwa pia kwa namna nyingine tofauti na hii ?

kalender zimepita kadhaa hapo nyuma, je siku mnayoiabudu ni jumamosi ya Gregorian Callender ?

kabla ya gregorian Callender kulikua na Julian Callender

sasa jumamosi sijui kwanini mnaiona tofauti sana
 
Sawa, kwa kukazia comment ya Member Namba Moja papa ni mwakilishi wa Devil mwenyewe. Kuna CODE: zinasema huyu ndie Pope wa mwisho anaekuja ni Anti Christ au mpinga Kristo, ila atakuwa amepoa sana miaka kibao akiwa kama pope wa kawaida halafu atakuwa "activated" kuanza sasa kukamilisha New World Order na ile 666.
Hakuna kielelezo chochote kuwa papa anayekuja ni ant christ, kwasababu uwepo wa cheo cha upapa tayari ni ant christ huyo, kwa sasa ni vigumu sana kupata historia sahihi ya zamani ili kuthibitisha kuwa unabii ulishatimia au bado likini huyu ant christ amesha kuweko na katimiza unabii au bado maana neno upapa kama upapa ndio ant christ inamaana hata huyu aliyekufa ni ant christ pia.

Kwahiyo kuwa makini sana na utambue kuwa ant christ amesha kuwako kwa karne nyingi ila kwasababu ya uwepo wa vyanzo vingi vya kihistoria vyengine vya uongo vyengine vya ukweli hii inakuwa ni ngumu kufuatilia ili kuthibitisha unabii kuwa tayari au bado ila ninacho jua ni kwamba umebaki mda mchache tu yesu anarudi nina wasiwasi kuwa unabii ushatimia ila bado nafuatili
 
Ok, nimekuelewa kumbe unafanya ushabiki kwasababu unamtizamo hasi kuhusu mungu, kuna makampuni mengi yanachapisha biblia hivi leo hata mimi naweza kununua mashine ya kuchapisha biblia tena ni rahisi kuliko.

Nachoona kwako umepungukiwa sana uwezo wa akili na huna unachokijua sasa cha kufanya tufunge haya mabishano maana mimi sio mbumbumbu.

kakae na wenzako muanze kudanganyana na haya mambo ya vijiweni na ushabiki wa usiokuwa na maana. hivyo nipo sahihi kusema huna akili
sio kuchapisha biblia elewa kupangwa ilivyo hivi

je unajua kuna injili zaidi ya 20 na zote ni sawa tu
kanisa limechagua injili 4 zikae kwenye bible

huo ndo mfano wa kitu nachoongelea sio kuchapisha

kwanza unaijua hiyo biblia imetokanaje hadi ipo hapo

wasabato mmeanza miaka ya 1800 alafu mnajikuta mnaijua sana biblia kuliko watu walio wapangia nini kiwepo kwenye biblia na nini kisiwepo ?
 
Hebu tufunge huu mjadara mkuu
 
Hakuna kielelezo chochote kuwa papa anayekuja ni ant christ, kwasababu uwepo wa cheo cha upapa tayari ni ant christ huyo, kwa sasa ni vigumu sana kupata historia sahihi ya zamani ili kuthibitisha kuwa unabii ulishatimia au bado likini huyu ant christ amesha kuweko na katimiza unabii au bado maana neno upapa kama upapa ndio ant christ inamaana hata huyu aliyekufa ni ant christ pia.

Kwahiyo kuwa makini sana na utambue kuwa ant christ amesha kuwako kwa karne nyingi ila kwasababu ya uwepo wa vyanzo vingi vya kihistoria vyengine vya uongo vyengine vya ukweli hii inakuwa ni ngumu kufuatilia ili kuthibitisha unabii kuwa tayari au bado ila ninacho jua ni kwamba umebaki mda mchache tu yesu anarudi nina wasiwasi kuwa unabii ushatimia ila bado nafuatili
Ok, sio habari zote zinapatikana ktk vyombo rasmi, ni kweli mahubiri mengi sasa hivi ni kupiga hela kuwa tajiri, na hakuna anaetukumbusha habari ya kurudi kwa Yesu.
 
imeandikwa yesu atarudi wakati tusio zani hivyo usisubirie huyo anti christ pengine unabii umeshatimia ila kuna upotoshaji flani maana cheo cha upapa ndio ile anatambulika kama mwakilishi wa kristo duniani yoyote anae kaa kwenye kiti cha enzi cha upapa ni ant christ huyo.
 
Pope ina maana baba..au kiongozi. Ni neno la kilatini na kimsingi linampa cheo cha kuwa kiongozi. Msingi wa kanisa Katoliki ni Yesu Kristu wenyewe.

Yesu aliliacha kanisa katika utaratibu. Ndio maana alimwambia Mtume Petro tena mara tatu, awachunge kondoo zake. Sio kwamba yeye ametelekeza kanisa, ila aliliacha katika utaratibu ambao uwe enedelevu.

Waprotesant, sababu ya kukosekana kwa mfumo kama huo, watu wengi wameanzisha makanisa yao, na kuingiza yale wanayoyaona yanawafaa wao.

Mfano siku ya pentekoste, watu walinena kwa lugha mbalimbali ila walisikilizana. Siku hizi wanaonena kwa vinywa wao wenyewe hawajui wanaongea nini na hata wanaosikiliza. Yna vionjo vyetu vya kibinadamuna mengi yanakosa mifumo thabiti ya kiungozi.

Na kukusaidia, kwenye kalamu ya mwisho Yesu aliyofanya na wanafunzi wake, aliweka PACT. Alimega mkate usio na chachu na kugeuza divai, iwe agano la milele la sadaka yake msalabani. Baadae mtume Paul akasema Yesu ni yeye yule yule jana leo na milele.

Hivyo basi, mpaka kesho, kwenye ibada ya misa takatifu, toka enzi na enzi, sadaka ile ile aliyofanya Yesu, iko hai na tunamkumbuka Yesu aliye hai.

Ni wakatoliki pekee ndio wanaadhimisha ibada aliyofanya Yesu siku ya Alhamisi Kuu. Unajua maana ya agano la milele alilosema Yesu?
Rc mchanga naomba kukuzwa kiimani.
Nisaidie vifunngu vinavyoagiza kusali rozari
Je Yesu alisali rozari?
Pale tunapomsujudia maria, na kumuomba atuombee, kuna ushahidi wa kimaandiko kuhalalisha hayo?
 
Rc mchanga naomba kukuzwa kiimani.
Nisaidie vifunngu vinavyoagiza kusali rozari
Je Yesu alisali rozari?
Pale tunapomsujudia marua, na kumuomba atuombee, kuna ushahidi wa kimaandiko kuhalalisha hayo?
wewe baki hukohuko
 
Back
Top Bottom