Tetesi: Je, ni kweli kwamba ndege ya ATCL, Boeing 787-8 Dreamliner haina Insurance?

Status
Not open for further replies.
Mkuu unaandika very professional, naona mtiririko mtupu wa Logic! ATCL Waje watoe ufafanuzi, hakuna ugomvi! Ndege ni zetu na Roho ni zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Watoe ufanunuzi kwa twitter ya mtu anayeogopa hata kuweka jina lake na ikakopiwa na mtu mwingine ambaye naye anatumia jina la bandia na hawana ushahidi? Hili jambo la kusema ''bisha nikuumbue'' ni mikwala mbuzi ya kizamani sana! Mtu kama una issue ya ukweli unaiweka ili watu waone! Potela pote usiweke jina lako lakini weka ushahidi wa unachoongelea. ATC nitawatetea kwa hili na nawaomba sana wasijibu ujinga kama huu. Watakuwa wana argue na fools.....
 
Kama huna Insurance huwezi kurusha Ndege zako especially Kimataifa

Juzi Kati ATC imerusha Ndege kwenda Zimbabwe Na imepita Anga mbalimbali bila ya Vikwazo
Hii habari Ni ya UOngo

Unachokisema ni kweli lakini nchi hii chochote kinawezekana. Haujasikia mtu kabambikiwa kesi ya mauaji hadi mkuu ameingilia kati haki kupatikana?

Mtoa taarifa amesisitiza ana uhakika na anachokisema, ameomba shirika la ndege lijitokeze kukanusha. Tusubirie
 

Umesoma vizuri kilichoandikwa na kukielewa lakini?
 
kuna mambo mengine lazima utoe proof ya tuhuma kwanza kabla muhusika aje kujibu tuhuma.kwani wakuu mtu aki kutuhumu kuwa unajinsia mbili,akwambie kama unabisha ntakuumbua.Je utavua nguo kumprove wrong?kama unanituhumu,leta ushahidi ili nipinge ushahidi wako,sio nipinge maneno bila ushahidi.Tukubali kuwa vitu vingine lazima viende ki taalamu.Huwez kuwa unajibu kila neno mtu asemalo bila kuleta ushahidi.
 
Angekuwa na uhakika angeweka ushahidi wa anachosema. Hili la kusema bisha nikuumbue ni la kizamani sana sana. Mimi naangalia mambo kwa mapana. Nasema hivi kwa sababu ATC ''wasipobisha'' kama mtuhumu anavyosema ina maana HATAWEKA ushahidi wowote. Na kama hataweka ushahidi wowote basi amefunika uzembe amabo ulitakiwa uanikwe!
 
Weka ushahidi bro.... punguza blah blah...kama unasema hao kampuni bima wame cancel bima ya ndege lazima kuna barua ya kusitisha.....ibandike hapa siku nyingine usilete porojo humu...
 
time. walienda lini na bima imefutwa lini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ushahidi kwamba ziletwe cover zilizo expire au kitu gani kiletwe? Tuhuma nzito kama hii ni zaidi ya expansion joint iliyopelekea kijana wa watu kwenda ndani kwa muda.

Binafsi imegoma kuingia akilini kwa jinsi nnavyoelewa taratibu zinavyoenda, lakini nikitafakari kuanzia mchakato wa manunuzi na umabavu ulivyogubika hizi ndege ukiongezea na uzembe wa viongozi wetu, sishangai kabisa kuwa hawaja renew cover.

Tuhuma zimejitosheleza kila kitu. Shirika ndio wanatakiwa kukanusha. Usishangae wapo kwenye mchakato wa kulipa ndio wajitokeze kwenye vyombo vya habari.
 
Kama huna Insurance huwezi kurusha Ndege zako especially Kimataifa

Juzi Kati ATC imerusha Ndege kwenda Zimbabwe Na imepita Anga mbalimbali bila ya Vikwazo
Hii habari Ni ya UOngo
Sawa, imeendelea na safari za njia hiyo? Mpaka sasa imekwenda mara ngapi?
 
Ushaambiwa mbishe alete ushaidi ,kabisheni kwamba mna insurance basi

Kelele nyingi za nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Vema kama unaangalia mambo kwa mapana. Lakini unaelewa madhara ya hizi tuhuma kibiashara? Nnavyoelewa jamaa wanavyofanya kazi sasa hivi, huyu mleta habari angekua polisi muda huu.

Nimeona kuna watu wanasema isingeweza kwenda safari za kimataifa kama haina insurance, habari inasema kulikua na cover ambayo baada ya muda kwisha haikulipiwa na ilishakua cancelled. Sasa huenda ndege ziliruka wakati cover iko valid.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…