Je, ni kweli kwamba vyakula vya mbegu vya GMO viko kwa ajili ya kuua kizazi cha watu weusi?

Je, ni kweli kwamba vyakula vya mbegu vya GMO viko kwa ajili ya kuua kizazi cha watu weusi?

Je madawa Hospitalini yenyewe ni salama? Tuanzie hapo kwanza
Je madawa Hospitalini yenyewe ni salama? Tuanzie hapo kwanza
Sio salama, wajanja tunajitibu kwa tiba mbadala. Punguza au acha kabisa kutumia sukari, pombe na nyama.

Kula mboga na matunda mwili wako upate alkaline kwa wingi, hakika magonjwa yatakuwa sio sehemu ya maisha yako
 
si kwel, hamna research ilio prove hilo, nabila gmos dunia kwa sasa ingekuwa kwenye shida kubwa, na sasa kuna technology ya kuzalusha nyama maabala amba iko safi kwa mlaji.
 
Nikiwa sokoni ntatambuaje kwamba hii bidhaa ni organic na sio GMO?
Ndizo zilizojaaa.
Anza nyanya kubwa kuliko zamani,
Njoo pia matango, tikiti, karoti, vitunguu maji, vitunguu saumu vyote vimerekebishwa. Ni vikubwa kuliko vya asili na vya asili vimepotea... Havipo.
Mahindi pia kwa sasa si kama zamani mkivuna mnachagua mbegu za kuja kuotesha tena. Siku hizi ni kununua mbegu na ukirudia kupanda msimu unaofuata hupati matokea mazuri.
 
Hivi Waafrika hua mnajikuta kina nani labda? 😆😆😆😆

Hivi wazungu wakuue wewe kwa kipi hasa? Muafrika sio tishio kwa maendeleo ya mzungu kwa njia yoyote ile, mzungu hana sababu yoyote ya kumuua muafrika. Na kama mzungu angetaka kutuangamiza mbona tungeshaisha zamani sana? Kwanza wao wanatutegemea sisi kama soko la bidhaa zao nyingi, na pia kama watumwa wa kuzalisha mali na kuwauzia kwa bei ya chini, wakituua hizo bidhaa zao watauza wapi?

Hebu acheni hii mijadala ya kupotezeana mda bana..
 
Hivi Waafrika hua mnajikuta kina nani labda? [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Hivi wazungu wakuue wewe kwa kipi hasa? Muafrika sio tishio kwa maendeleo ya mzungu kwa njia yoyote ile, mzungu hana sababu yoyote ya kumuua muafrika. Na kama mzungu angetaka kutuangamiza mbona tungeshaisha zamani sana? Kwanza wao wanatutegemea sisi kama soko la bidhaa zao nyingi, na pia kama watumwa wa kuzalisha mali na kuwauzia kwa bei ya chini, wakituua hizo bidhaa zao watauza wapi?

Hebu acheni hii mijadala ya kupotezeana mda bana..
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Kwamba kila technologia ni kwaa jili ya kumuua black acheni uzwazwa mambo sio rahisi hivyo

Si wangeponda nyukilia tu afrika wote tukaisha na kisha makomando wakaingia mtaani for diaspora mbona ni suala 1 year tu wanabaki weupe tupo worldwide.

Maana black ndo race yenye watu wachache zaidi na dhaifu duniani
 
Swali ninkwanini wao wazungu wanataka product og? Kwani wao wajinga? Wazungu hawanunui izo product za gmo kwanza gmo hazina ladha jaribu kutumia nyanya hizi za gmo mbaya kishenzi pia ata zikioza wadudu hawana time nazo
 
Dah! Lahaullah! Alafu kwao ndio wanalima zaidi ya huku kwetu! Ila inatisha unapokutana na chungwa, pera au embe ndani halina mbegu au kokwa! Ukalila ukitegemea na ww ukatoe Mbegu thubutu!
 
Matumizi ya simu mlisema INA miale ya kuua kizazi!

5G MLISEMA INAUA KIZAZI!

ARVs mlisema zinaua kizazi!

Broilers mlisema....

Mayai ya kisasa....

CHANJO YA CORONA mlisema zinaua kizazi

ILA YOTE MLIBANA MKAACHIA.

GMO haina ujanja tutatumia tu!
Hivyo vyakula watakula wengine mimi sitakula kabisa,nakula chakula nilicholima mwenyewe kwa mkono wangu,mbolea natumia ya wanyama nao fuga mwenyewe,madawa natumia ya kienyeji nina mwaka wa 15 sijawahi kwenda hospital,tusipende vyakula vya super market,vyakula vyote.vitamu vina madhara,tukianza na kuku hao wa kisasa,cake,biriani,pilau,chips, pizza n.k basi kwanini tusile mihogo ya kuchemsha,majimbi,ndizi,viazi tule kama walivyofanya.wazazi wetu,mikakati ya wazungu ni kupunguza idadi ya watu duniani,ndo maana wa kaleta corona,ili chanjo zitumike kupunguza idadi ya watu,wazungu walishangaa sana mbona watanzania hawapati corona,ili kuendeleza kizazi cha utu mweusi ni bora kuepuka kula artificial foods
 
Nikiwa sokoni ntatambuaje kwamba hii bidhaa ni organic na sio GMO?
Tanzania hatuna sera ya kimasoko kwa bidhaa za kilimo ambazo ziko mtindo wa kilimo hai (Organic) kitu pekee ambacho hatukijui kilimo hai ni kigumu na gharama na kina hasara sana, kingine kwa nchi yetu bei haiko juu, kama uko Moro nenda Sat au tembelea maeneo ya ofisi za SwissAid. But kuna certification ili uwe mkulima wa kilimo hai kwa certifies wa kimataifa
 
Katika miaka ya hivi karibuni Watanzania tumekua tukisikia kuhusu swala la kuwekeza katika kilimo ambacho wanasiasa wanakiita "KILIMO CHA KISASA" ambacho kinahusisha utumiaji wa mbegu ambazo ni Genetically Modified. Lakini ni nini hasa maana ya GMO?, Je ni salama kwa kula?.

GMO ni aina ya mbegu na mimea ambayo imebadilishwa vinasaba (genes) katika maabara ili kuboresha aina fulani ya traits au tabia inayohitajika, kwa mfano kuongeza virutubisho, na kuongeza uwezo wa kujikinga na madawa.

Marekani ndio inaongoza kwa utengenezaji wa aina hii ya mbegu zikizambazwa na makampuni kama Monsanto, Syngenta AG, na DOW Chemicals ambazo nyingi tumekua tukiziona nchini. Hatari zitokanazo na aina hii ya mimea ni nyingi kuliko faida, na nchi nyingi duniani tayari zimezuia matumizi ya aina hii ya mbegu ikiwemo Canada, Argentina, Australia, India na Mexico na msimamo wa EU Ukiwa "Zuia GMO".

Nilibahatika kukaa na msomi mmoja wa Chuo Kikuu Cha elimu ya juu cha Nelson Mandela na akanitajia baadhi tu ya athari nyingi zikiwemo; Kuharibu mfumo wa ikolojia, kuharibu ama kubadilisha kabisa virutubisho katika mimea, Kansa, kuharibu rutuba ya ardhi na kusababisha wakulima kua tegemezi wa madawa ya kilimo, kujitokeza kwa magugu ambayo yanajikinga na madawa ya kuua magugu, na hasara kwa wakulima kutokana na ununuzi wa kiasi kikubwa cha madawa.

Faida chache alizonitajia ni pamoja na ongezeko la mimea inatojikinga na wadudu na magonjwa, kuongezeka kwa food supply, na kua na mimea inayostahimili ukame. Pia aliniambia "Hakuna Mwanasayansi duniani ambaye yuko serious atakayetoa support kwa GMO, UNLESS yuko katika payroll ya hayo makampuni", kwa sababu kiuhalisia, ni makampuni ya Biotech ambao ndio watengenezaji na wasambazaji watakaonufaika kutokana na mauzo ya mbegu na madawa!

Swali la kujiuliza; Je ni Watanzania wangapi wanazijua athari zitokanazo na GMO's?, au wengi wetu tumeangalia faida za kiuchumi kuliko athari za kimaziangira na kiafya?. TUAMKE NDUGU ZANGU
Well said mkuu
 
Dah! Lahaullah! Alafu kwao ndio wanalima zaidi ya huku kwetu! Ila inatisha unapokutana na chungwa, pera au embe ndani halina mbegu au kokwa! Ukalila ukitegemea na ww ukatoe Mbegu thubutu!
Hizo ni aina na sio kwamba injinia imefanyika, matunda inahusu sana njia ya asexual yaani haitegemei kuchavusha au mbegu katika kuzunguka kwake sana sana ila kwningine ni zile zinazotumia mfumo wa mbegu katika kujizalisha yaani sexual reproduction. Ndio maana pichani wameweka nafaka na mbogamboga mkuu
 
Back
Top Bottom