Uhaini upo kwenye Katiba ya JMT 1977, huyu ni yule mtu anayetaka kuipindua serikali, sasa ataipindua vipi serikali mtu asiye hata na rungu mkononi?
- Wajinga wanasema kwa maneno?! kumbe maneno siku hizi yanaweza kuvunja mfupa!.
Katiba hiyo hiyo inazungumzia maandamano kama njia ya kufikisha ujumbe kwa mtawala, hii ni haki ya mtanganyika.
Tatizo limekuja pale mtawala muovu ameanza kuogopa mpaka kivuli chake mwenyewe, hataki kuambiwa ukweli, kwasababu unamuuma, anajua ametusaliti, na tumeukataa usaliti wake.
Sasa ameamua kuwazuia wanaotaka kumfikishia ujumbe kwa njia ya maandamano, ameona awape kosa la uhaini, huyu msaliti aliyetoa bure rasilimali zetu milele, anataka kupigiwa makofi ya kupongezwa kwa unyama aliotufanyia na vizazi vyetu. Hapana.
Adv. Mwabukusi ujumbe wangu kwako; ile njia ya bonde la uvuli wa mauti uliyojua utapitishwa, sasa ndio unapita, STAY STRONG, I know ujumbe wangu unaupata in a very special way, stay strong. You are not alone.