Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 984
- 1,179
Kuna Propaganda mpya dhidi ya Waislamu.
Wako wanaofurahia propaganda hizo.
Wako wanaoamini propaganda hizo.
Wako wanaolipwa kwa kuandaa propaganda hizo.
Propaganda hivi zimaendezwa kwaa media kupitia waandishi
Lakini wapo waandishi waliotaka kujua ukweli wa ugaidi. Kuwa ni magaidi wenyewe ndio wanaojinasibisha na Uislam au ni waandishi wenziwao ndio wanaoufungamanisha Uislam na Ugaidi.
Mmoja wa waandishi hao ni AZORY. Hata hivyo alipotaka kutekeleza jukumu hilo alipotezwa na watu wasiojilikana. Kila mmoja unaelewa ni nani wasiojilikana kuwa ni watu waliosikiliza amri kutoka juu.
Hata hivyo limejitokeza akina Azory wa Bandia. Wameweza kukusanya uchunguzi na kuzungumzia ugaidi wa waislam.
Kundi hilo linauzungumzia ugaidi kwa ustadi zaidi ya waongoza muvi za BOLLYWOOD wa na wasimulia muvi wa kule tandale.
Cha ajabu wameyafanya yote na hatimae kuanza kusambaza kwenye mitandao.
Hata hivyo kikundi hiki kinafanya yote haya kama kwamba tz ni sehemu salama kwao kujificha kwa kutengeza na kusambaza uongo uliotengezwa huku wakikingiwa kifua.
Hata hivyo kwa nyakati kadhaa wakili Peter Madeleka ameitahadharisha jamii na hasa wanahabari kuandika taarifa za kiuchunguzi za uongo zinazopelekelea waislam kuteseka na kuumizwa na kunyang'anywa mali.
Angalia clip hii hasa kuanzia dkk ya 7
View: https://youtu.be/72rIuu-GSf0?si=r6qSCzYwU5qL6llP
Waislam nchini wanaitahadharisha SERIKALI izingatia zaidi maslahi ya Taifa katika kuiendea na kuishughulikia dhana ya ugaidi nchini.
Kuna waandishi hao ambao jf inawalinda wameendelea kuandika makala zinazozungumzia ugaidi wa Waislamu nchini na kwa nchi za jirani.
Kuna waraka wenye anuani ya Njua ya Kibiti kwenda kwenye laana Cabo Delgado.
Moja ya suala linalojitokeza katika makala hiyo ni Uislamu na ugaidi, ingawa mwandishi anadai kuwa magaidi ndio wanao husisha Dini ya Uislamu na ugaidi lakini kwa hakika yeye (Mwandishi) ndiye anayehusisha Uislamu na Ugaidi.
Tunawashauri viongozi wazingatie zaidi maslahi ya Taifa katika suala hili la ugaidi, kwani sasa zimeanza kuibuka propaganda mpya za ugaidi zinazo wanasibisha Waislamu.
Tunaishauri serikali ifute kabisa sheria ya ugaidi na badala yake itumie shera ya uhalifu ambao ipo ili kuwapumzisha na kuwaondolea waislam wasiwasi wa operasheni zinazoibuka baada ya kuanza kwa propadanga hizi ili niweze kuhalalisha uovu wa baadhi ya watendaji wa serikali waovu, wavuta bangi waliopandikizwa chuki kupitia propaganda hizi dhidi ya Waislamu.
Tunaikumbusha Serikali kwamba, Taifa la Tanzania limejengwa juu misingi mitatu ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.
Na huu mpango mpya wa propaganda zenye uongo uliotengenezwa si ktk misingi sahihi ya kuendesha serikali.
Waraka huu umesomwa na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kwa waislam nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.
Ameeleza kuwa mwaka 2002, wakati wa mchakato wa Sheria ya Ugaidi, Wabunge walisema maneno mazito Bungeni, na kufafanua kuwa Tanzania hakuna ugaidi na Sheria hiyo ya Ugaidi inawalenga zaidi raia Waislamu.
Akasema, hivi sasa matokeo ya utekelezaji wa Sheria hiyo yanaonekana wazi kwani wanaokamatwa na kutuhumiwa kwa ugaidi wengi wao ni Masheikh na Waislamu wa kawaida.
Lakini la kusikitisha zaidi ni kwamba hata kesi zake mahakamani zinakwama kusikilizwa na Waislamu wakabaki wafungwa mahabusu wa muda mrefu.
Akizungumzia kuhusu makala hayo Sheikh Ponda, anasema ingawa mwandishi anadai kuwa magaidi ndio wanao husisha Dini ya Uislamu na ugaidi, lakini makala hiyo ipo wazi kuwa yeye ndiye anayehusisha Uislamu na ugaidi.
Akifafanua Sheikh Ponda, amesema Mwandishi wa Makala hiyo amewataja Waislamu wasomi wa Vyuo vya Kiislamu kama Magaidi huku Misikiti, Madrasa, Asasi kama vile vituo vya Yatima na Shule za Kiislamu amevitaja kuwa ni vituo vya Kigaidi.
Aidha amesema, katika makala yake hiyo ameyataja mataifa kadhaa aliyodai kuwa yanayoelekea kusambaratika kutokana na hicho alichokiita ni ugaidi.
Sheikh Ponda amemtanabahisha mwandishi huyo kuwa uandishi wake unatakiwa azingatie maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kuhusu suala hili zito linalohusu uhai wa watu na mustakbali wa Taifa, badala ya kuja na uchambuzi wa taarifa bandia za Intelijensia.
Kwani taarifa sahihi anazo Azory.