Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Daaaah mimi tumebadilishana nguo sana na wasichana wakat wa kombolela za usiku nimemiss
 
Tena sisi tulikua tunaweka mchanga kdgo kwenye mpira ssa hapo ukimbabua mtu tu anaanza kulia
Alafu limpate la uso... Utasikia "Yalaaaaaaaa"... Ukilia maumivu wanakuimbia
" fulani usilie,
Mchezo, ndivyo ulivyo!"
 
Halafu mnajenga na kakibanda kaungo na kweli huku pembeni kukiwa natuvyombo twakujipikilisha ilikuwa ninoma aisee
noma sana ulikuwa hutaki kupoteza chance
Nakumbuka tulimfungisha ndoa mdogo angu na jirani na wakavalishana pete tumetengeneza na majani. Neti ndo tukatumia kama shela [emoji23][emoji23][emoji23]. Baada ya ndoa kuna kakibanda tulijenga na miti eti wakaingia huko no honeymoon...
Mpaka leo dogo ana uhusiano wa kipekee na huyu binti, sijui waliendelezaga honeymoon!!!?
 
kuogelea kwenye mabwawa ukirudi home mtu umepauka hatari wazazi wakishajua kichapo chake utajuta yani.
yani imebidi nisome twice ndio nikaelewa ulichokiandika duu.
Au kucheza kwenye mvua... Niliteseka na nyungunyungu utotoni! Alafu enzi hizo hamna cha kumeza vidonge kama saivi... Mama anachukua kiwembe ana chanja chanja alipopita nyungunyungu na kutia ndimu na chumvi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kilio chake si cha dunia hiii!
 
Kwa hiyo mpaka leo ni wake [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Home tulikuwa tunafikia kipigo kwanza dah[emoji2] [emoji2]
 
Kidali po ulikua mazoezi tosha!!!
Au mpira wa chenga.... Kupigana matobo
kuna mchezo mwingine nimeusahau ulikuwa hivi mnakusanya michanga then mchomeka kakijiti halafu mnaanza kumega atakaekaangusha hako kakijiti tu ni kipigo kifuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…