Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Basi kunakuwa na kitu cha kukisgusa ili masela waache kukupa mingumi... [emoji23] labda mti hivi.. Sasa ukifanikiwa kufika kwenye ule mti unakuta wajomba wameuzingira ule mti daah[emoji23][emoji23]
Hahahahahaaa [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimekumbuka mbali sana yani. Utoto raha sana
 
Kujipikilisha
Mpaka mama alinipatia kasufuria kadunchu na mwiko. Daah, si kwa kupukiza moto kiasi kile.
usitake nambia ulishaanza jua kupika wakati mdogooo [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
usitake nambia ulishaanza jua kupika wakati mdogooo [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mwanzoni ilikua kuchemsha tumchicha, tunaiba michele madukani na kupika!!!
Mama alianza nifundisha ugali nikiwa na miaka 8.... Niliungua tumapaja na uji unavotokota [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huko uchagani tulikuwa na mchezo unaitwa matera. Mnapigane mateke mpaka mbabe ndio anabaki kasimama. Ukiona unazidiwa unachuchumaa
 
Aiseee!!? Mimi penda sana cheza kidari, goroli, mpira Wa miguu, kibaba, mchezo Wa magari ya mbao msukani mti.
 
Baiskeli ya mbao tuliita skuta
 
Ambaye amezaliwa kipindi hiki anashangaa shangaa tuu huu uziii
Kabisa!
Hii michezo saizi imepotea kabisa.

Mimi nimecheza karibia michezo yote,ukuti ukuti,Baba na mama,kombolera,"Senta",kubwa zaidi ambalo halitafutika kwa ubongo wangu-Nikiwa na miaka kama sita hivi tulifungishwa ndoa mimi na binti mmoja (kwakweli alikuwa anamuonekano uliobora na wakuvutia) ilifanyika sherehe moja matata sana ambayo ilipangwa na rika letu tu, mimi na suti na yeye na shela haha Mtaa mzima ulizizima mpaka watu wazima walipigwa na butwaa.

AISEE nikiikumbuka siku hii huwa nacheka mwenyewe moyoni,binti huyo hata Sijui yuko wapi Manaake Familia zilitawanyika.
 
Mchezo wa kombolela kiza kikianza kuingia tunatoa kopo tunatega jiwe atayekuja kubutua lazima aisome namba
 
Huu mchezo haufai kabisa tulishawahi kumzimisha mtoto wa watu kwa kipigo
Yaani ukiwa mnoko wa kitaa usicheze huu mchezo. Utapigwa ujute kuzaliwa. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…