Hahahahaha,
Halafu hii michezo ilikuwaga ina msimu, kuna kipindi mnatengeza magari ya mabati kata sana kopo za cowboy na tanbond baadae msimu unageuka magari ya wire, tiara, gili, kwenda kucheza mpira mkitoka mnaingia kwenye shamba la mtu mnaiba zambarau mara mwenyewe anatokea kimyakimya mnatoka baru mnawaacha wenzenu juu ya mti.
Baiskeli za miti, ndege ya chini bering ikiingia udongo mnaikojolea na kila mtu anahifadhi mkojo coz mnakojolea bering kwa zamu.
Kipindi cha December baruti zinaanza
Kipindi hicho hamna TV wala nini zaidi ya redio mkulima