Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Mi nilikuwa ni mtoto wa games tu

Need for speed
Beach head
Game lingine jina nimelisahau hivi nakumbuka ulikua unaua maadui katika meli unawamaliza then katika treni ili usave watu wema(jina nimelisahau)
Game lingine la kuendesha ndege nalo nimesahau jina lake
Na Euro truck
 
6b8574975a9a6e89f5e06a846b585995.jpg
 
Mpira wa miguu, kujificha, kuwinda ndege, draft, ludo nadhani, kushindana kukimbia etc.
 
Mi nilikuwa ni mtoto wa games tu

Need for speed
Beach head
Game lingine jina nimelisahau hivi nakumbuka ulikua unaua maadui katika meli unawamaliza then katika treni ili usave watu wema(jina nimelisahau)
Game lingine la kuendesha ndege nalo nimesahau jina lake
Na Euro truck
Hilo linaitwa VCOP mambo ya sega hayo....
Kizazi cha 1995 wewe
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hiyo style tulikua tunaiita kije, yani kijembe. Nlikua nkipiga hiyo lazima ntoe banju
Huwa nacheka tu mwenyewe kila nkikumbuka misamiati ya kwenye goroli, kama hii ifuatayo:
Dungu, cha maziwa(goroli flani ina rangi ya maziwa), macho ya paka, kisukwa au king'wasu, kupunwa, banju, kishi, kinatenge, no tenge, majoda, wa mwilo, badala ya pili, tili mpaka kishi, kono, no kono, mwendeo, kila, fagi, no fagi n.k
 
Hilo linaitwa VCOP mambo ya sega hayo....

Kuna ile ya kwenye meli mwishoni nakumbuka kulikua na maadui kama wanapaa flani hivi kama sijakosea, na kuna moja nakumbuka kama adui kuu lilikua linarusha mpaka magari
 
View attachment 474250View attachment 474251
Kama kuna alie icheza michezo hii, akuje pm tuyajenge.....[emoji39] [emoji39] [emoji39]
Hahahahaha,
Halafu hii michezo ilikuwaga ina msimu, kuna kipindi mnatengeza magari ya mabati kata sana kopo za cowboy na tanbond baadae msimu unageuka magari ya wire, tiara, gili, kwenda kucheza mpira mkitoka mnaingia kwenye shamba la mtu mnaiba zambarau mara mwenyewe anatokea kimyakimya mnatoka baru mnawaacha wenzenu juu ya mti.

Baiskeli za miti, ndege ya chini bering ikiingia udongo mnaikojolea na kila mtu anahifadhi mkojo coz mnakojolea bering kwa zamu.

Kipindi cha December baruti zinaanza

Kipindi hicho hamna TV wala nini zaidi ya redio mkulima
 
Huwa nafeel shame unapokutana na yule ambaye mlichezaga wote huo mchezoo then jinsia tofauti asee huwa namkwepaga kaisaa
Alafu kweli!!! Yaani jinsia zote mnajikuta kwenye rede ya wote [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aiseee mimi utotoni nimecheza michezo yote. Kujipikilisha, baba mama, kuchezesha vitoto, kombolela, dama, senta, namsaka mke wangu, kucheza mabunduki, mpira kombe ikiwa pakti moja ya karang. My favourite play ulikua GOROLI mpaka leo nikiwaona watoto wanacheza natamani namm niombe namba
Kwenye mchezo wa kuchezesha basi unaombeaje sahani/kikombe kivunjike??? Alafu ndo upate ile ya rangirangi na triangle eti ndo mdada...
Mdako, full kukuta mashimo uwanjani, au ndani sakafu imechorwa na mkaa au kokoto [emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna ule wimbo wa kuhusu maboga (kitu kama hicho), mnabong'oa alafu mwenye mwimbishaji anakuja kubonyeza makalio kutafuta lililoiva. Wakaka walikua wanapenda kuimbisha aisee!
 
Back
Top Bottom