Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Njia nzuri ni ile ya kuchagua. Viongozi wawili wa timu wanapokezana kuchagua... Sasa hapo ndo unajua uhodari wako. Kulikua na watu wanakataliwa adi huruma! Mi walikua wananikataa kwenye rede [emoji85][emoji85][emoji85][emoji85]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu itakua ulikua 'unababuliwa' mapema tuu
 
Walikua wanajua mtu lazima ubembeleze urafiki kwake. Ole wako uwe na kitu afu umnyime, utaskia na usije kwetu [emoji23] [emoji23]
Ukijipeleka kwao sasa hiyo aibu yake utakavyo fukuzwa na kusukumizwa... "Toka kwetu" [emoji34]
 
Hahahahaaa, ndo maana ulikua unabaki mwisho mkuu. Kuna wengine walikua mafundi hawababuliwi mpaka wanaokoa wenzao
Daah kuna waliokua wanaruka kama ndama isee!!! Watu wanapiga sarakazi kukwepa mpira. Kuna mmoja alikua akiamua anadaka mpira wala hakosei.
 
Kama haukuwa mtoto wa geti kali lazima michezo mingi ya utotoni utakuwa unaikumba binafsi nilikuwa napenda michezo mitatu tu ambayo ni;

1. Michezo ya vita hapo unaashumu wewe ni Rambo ukiwa na bunduki ya mabomba ya mipapai.

2. Komborela

3. Mpira huku magoli yakiwa ndala au mawe.

Je, wewe ulikuwa unapenda michezo gani?
Kombolela
 
kuna mchezo mwingine nimeusahau ulikuwa hivi mnakusanya michanga then mchomeka kakijiti halafu mnaanza kumega atakaekaangusha hako kakijiti tu ni kipigo kifuata.
Naukumbuka ilikuwa mnachagua mti au mahali pa kukimbilia kushika kama ukiangusha kijiti sasa unakuta unachagulia mti wa mbali balaa.. Sasa ukiangusha kijiti kile usiombe watu wakudake... Mpaka uufikie mti kichwa kinauma..
 
Utotoni nlikua napenda pia kufuga samaki na kuuza. Enzi hizo kulikua na samaki kama gapi, texido, zebra, gulam, red, gold n.k. Am sure waliowahi kufuga samaki watakua wanajua haya majina
 
Utotoni nlikua napenda pia kufuga samaki na kuuza. Enzi hizo kulikua na samaki kama gapi, texido, zebra, gulam, red, gold n.k. Am sure waliowahi kufuga samaki watakua wanajua haya majina
Sisi kulikua na ma madimbwi yana kambare, ukirudi nyumbani mwili wote umejaa tope na kambare wako. Alafu tunakamata vile sijui vichura vidogo tunafuga tunadhani samaki
 
Nakumbuka siku moja tulienda kuangua maembe kwenye kambi ya jeshi, walitokea wajeda!! Acha watubalase.
 
kuna mchezo mwingine nimeusahau ulikuwa hivi mnakusanya michanga then mchomeka kakijiti halafu mnaanza kumega atakaekaangusha hako kakijiti tu ni kipigo kifuata.
Kula mbakshie baba[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom