Habar zenu ndugu zang samahan najua si sehem husika ila kuuliza hili Ila binge penda kuuliza kutokana na ufaham wa watu wenda hil nalo nikapata ufumbuzi
Nahitaj kuwa connected na mtu ambaye tayal ana nunua HISA za CRDB,NMB,TCC,TWIGER CEMENT na zngne Au anae ijua Vzr zaid huu uwezekaji wa hisa
mkuu mi sijawekeza popote bado ila nimesoma sana kuhusu stocks na bonds, nimebaini kwamba ukitaka kuishi bila stress hapa duniani basi kuwa BONDHOLDERS Na siyo SHAREHOLDERS. Why??
bondholders kwa lugha nyepesi ni mkataba wa mkopo ambao unaonesha kuwa unamkopa mtu flani kama vile serikari,kampuni,shirika kwa masharti ya kwamba baadae urudishiwe pesa yako pamoja na riba juu.
SHAREHOLDERS, ni namna ya kununua umiliki kwa kampuni flani.. unanunua units ambazo ndo hisa kwa jina lingine.. yaani unachukua hela yako unampa mwenye kampuni ili aongeze capital na mwisho wa siku unufaike na wewe kwa faida na hasara itakayopatikana kwenye kampuni hiyo, sasa dhamani ya units zako zinapanda na kushuka haziko fixed yaani.. ikitokea kampuni imefirisika basi na wewe unakuwa umepoteza pesa zako nazani umeanza kupata picha mkuu, kununua umiliki ni much risks kwa sababu hela yako huna uhakika 100% stocks ni more risk better utrade forex tu japo nayo ni risk.
mkuu sasa nazani umeeelewa unataka kukopesha pesa zako kwa kampuni flani au unataka kununua umiliki wa kampuni flani???
best option and it is low risk ni kuikopesha serikari kwa riba maana serikari haitokuja kufirisika leo wala kesho.. sasa unaikopeshaje serikari? serikari itaomba mkopo kwako kwa kutoa BONDS za muda mfupi (treasury bond) na za muda mrefu.
wapi napata hizo bonds?
1. BONDS zinatolewa na benkii kuu hapa utapata gawio lako ama faida ya riba yako mala mbili kwa mwaka.
2.UTT BONDS, hii ni mutual fund iko chini ya wizara ya fedha na mipango, hapa unapewa gawio lako kwa mwezi.. japo niliwahi kuwapigia simu nikapata maelezo mazuri kuhusu hesabu inayotumika kupata gawio la mwezi... maana kuna pesa unalipwa ya kujikimu na nyingine inabaki kwenye account yako ya UTT, ukichukua pesa yako uliyoweka ukagawa kwa dhamani ya kipande cha bond jibu utakalopata ni hela yako ya kujikimu halafu ukichukua asilimia moja ya pesa zako ulizowekeza ukatoa pesa ya kujikumu hiyo ndo itakuwa ni balance itakuwa inasomeka kwenye account yako ya UTT ila pia na yenyewe unaweza itoa kwa kujaza fomu crdb bank na kuitoa.. pesa ya kujikimu yenyewe inaingia automatically kwenye account yako bank.. na ile balance itakayokuwa inasomeka kwenye app ya UTT utaitoa kwa kujaza fomu CRDB bank.
hii ni knowledge yangu tu, sijafanya bado kwa vitendo.
ila napambana kufa na kupona nimiliki BOND za deep cash.
asanteni.