Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Yaani unamaanisha licha ya gawio la at least 10% kwa mwaka, hivyo vipande vinapanda thamani pia? Yaani kama hisa?Kwa vile thamani ya kipande (Net asset value per unit) hukokotolewa kila siku kwa kila mfuko wao, unaweza kukokotoa thamani ya uwekezaji wako kila utakapo.
Mimi kwa mfano huwa ninakokotoa thamani ya uwekezaji wangu mara 1 kila wiki. Unaweza kukokotoa hata kila siku.
Thamani za vipande siku kwa siku zinapatikana katika website ya utt, kwenye application ya utt ukiwa nayo, na mara nyingine huchapwa katika baadhi ya magazeti.