Je, Ni msanii gani wa Bongofleva aliyepotea katika muziki unatamani arudi katika muziki?

Je, Ni msanii gani wa Bongofleva aliyepotea katika muziki unatamani arudi katika muziki?

University corner,
Solid groud family,
Uswahilini matola,
Wagosi wa kaya,
Daz dundaz,
Mr.paul,
Mike T,
Vumilia,
Mb dog,
Gk,
Noorah, n.k

Kiufupi ni wengi sana,
Nilikua naipenda bongo flavour ya zamani, kwa sasa hata sijui wanaimba nini.

Mb dog is back week hii kaa mkao wa kula
 
Poline zongo,stara thomas na kuna wimbo una maneno yanasema"macho yanaona mbali,lkn ni vigumu sikio lako kuliona,nahisi unaitwa utanikumbuka"..aloimba na kuandika ule wimbo anajua sana,siku hizi waliopo wanaimba utumbo mtupu..

Stara thomas anaimba gosspel
 
Terry Fanani junky heavy, sasa mtu mzima na akili zake anakula unga umlaumu Jay yeye ndio anamnunulia ngada? Lawama nyingine hizi.

Uko sahihi kiasi chake,labda unafahamu historia ya hard blasters? Awali hakuepo jay,alikuepo teacher kaka yake Jay..the crew haikukick kivile but was like a family..baada ya tiacher kwenda ughaibuni..jay akajoin crew..nakweli crew ikang'aa na akang'aa yeye kwa kiasi kikubwa..akawasahau wenzake na kuinitiate sole based projects..HBC ikafa taratibu,dispointment na stress za maisha kama ilivyokuwa kwa wengu mziki usipo walipa akaingia kwenye wingu la kutumia madawa...baadae Mr. 2,sugu akamuokota nakuanza kumuhudumia na kumpeleka rehab...watumiaji wa madawa ya kulevya si watu wakutengwa ni watu wakukaa nao pamoja nakujaribu kuwarudisha kwenye mstari,mwisho wasiku wanatugusa sisi sote.
 
Juma nature anatangatanga tu dah!

George kasera "squizer" attack

Man Dojo na Domo kaya


Hao nilipenda warudi vzur maana wanarudi lkn rudi yao haitoshi,haiendani na soko,juz George katoa nymbo mbili,moja kaimba na belle na hii nyngne ya karbuni hazijafanya poa

Man dojo na domokaya hakuna kibao walitoa kibaya,waache poda warudi kdogo kdogo kama Aboubakar katwila "q chilla"
 
mandojo domo kaya ohhh jaman enz zile jamaniii! nikupe nn mpnz,hatupatani,ukimpenda m2 basi imebak moments tu..
 
Back
Top Bottom