Je, ni nani aliyeharibu CHADEMA kati ya Mbowe aliyepeleka wanachama Bungeni na Lissu aliyeondoa wanachama Bungeni?

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,651
Reaction score
1,129
Je, ni nani aliyeharibu CHADEMA kati ya Mbowe aliyepeleka wanachama Bungeni na Lissu aliyeondoa wanachama Bungeni?

HIi ni hoja nzito sana na sii ya kuchukuliwa kirahisi

Ili Chama cha Siasa kikue lazima kiwe na idadi kubwa ya Wanachama wenye wadhifa mkubwa katika nchi

Mbowe alizalisha viongozi wengi na wakubwa sana akiwemo Lissu anayejivunia leo kuwa kiongozi wa CHADEMA

Lissu baada ya kukabidhiwa wadhifa wa kiongozi mkuu wa CHADEMA hali ilibadilika sana

Kwanza aliwaeleza Wanachama wake kuwa wale wote wanaotaka kuwa Wabunge wasahau hilo

Kauli hiyo haikuishia hapo pasipo matendo, badala yake alitenda na kuhakikisha hakuna Mwanachama aliyepata nafasi ya Ubunge

Lengo la hoja hii nikutaka CHADEMA ijisahihishe makosa yake na sio kudhihaki

Nalazimika kutumia lugha kali kwasababu hata CHADEMA ni wakali vilevile

Namna nzuri ya kuzungumza nao ni ile ya kukabana koo na kuchaniana mashati
 
Rubbish! Chawa mkubwa we
 
Unatuchosha maelezo mengi pumbazalation nyingi.

Umefungia chama,umefunga wanachama,ubambika kesi,unanyima ruzuku alafu unakuja kusema Chadema imeuliwa.

Abdul wa makachu muombeni NSSF mapema la sivyo siku ikifika mtaacha kutumia hiyo ofisi hapo mikocheni.
 
Twende kwa hoja aliyeua CHADEMA kati ya Mbowe na Lissu ni yupi?
 
Mambo mengine yanahitaji akili na maarifa sio kudesa, ukiona huelewi ujue ipo juu sana ya upeo wako, unaachana nayo tu unafanya mengine! Mbona uchawa una topic nyingi tu sisiemuni? Kwani kila kitu humu duniani lazima ukijue?
 
Mambo mengine yanahitaji akili na maarifa sio kudesa, ukiona huelewi ujue ipo juu sana ya upeo wako, unaachana nayo tu unafanya mengine! Mbona uchawa una topic nyingi tu sisiemuni? Kwani kila kitu humu duniani lazima ukijue?
Lakini huu ndio ukweli
Bado wanakaza shingo wakati meli inazama labda itakapozama yote ndipo watakumbuka kosa lao
 
Kwa mtazamo wangu na wawengi ninaouona chadema kwasasa inapendwa zaidi kuliko wakati wa mbowe na ndio maana inapata vikwazo kuliko wakati mwingine wowote na ccm inajua kwamba chadema Ina nguvu kuliko ccm ndio maana wamewafunga kamba nyuma mgongoni ili wapambane nayo ikiwa mnadhani ccm Ina nguvu basi mwachieni lissu huru na hata Dola yote ikiwa ccm kama kawaida Bado ccm hamtoboi. Chadema Kwa Sasa ni far way strong than ever before.
 
Chadema iko imara kuliko jana na juzi. Chadema ya sasa sio Chama tu cha siasa, bali ni imani na imani sio rahisi kuiteteresha.
 
Kwasasa chuki ya watanzania dhidi ya ccm serikali na Samia binafsi ni kubwa mno na hii ni deep hatered na matukio ya MO29 ndio yameongeza chuki mara dufu kwasasa kama unadhani ccm inapendwa Fanya tafiti ndogo tu wapitisheni na uniform zao pikipiki na zile baskeli zenu halafu utanipa mrejesho.
 
Pengine iko hivyo lakini hapendi Wanasheria wamsaidie huwa anataka ajisaidie mwenyewe hii inashangaza sana hata Wanasheria wengine wenye mapenzi mema naye, si sahihi mtu kuamini anaweza kila jambo mengine ni ya kusaidiwa
 
An
Pengine iko hivyo lakini hapendi Wanasheria wamsaidie huwa anataka ajisaidie mwenyewe hii inashangaza sana hata Wanasheria wengine wenye malenzi mema naye, si sahihi mtu kuamini anaweza kila jambo mengine ni ya kusaidiwa
Anataka awafundishe Sheria na historia itamkumbuka Kwa mengi.
 
Nitachunguza ili nijue fukuto hilo ni la kiasi gani hoja yako ni nzito sana ina maana kubwa sana
 
Jiulize kwanini mama yenu Jana wakati anaongea na jwtz aliitaja chadema na ccm tu? Na kimsingi aliitaja chadema.
Ni kweli CHADEMA ina moto, gear ishachanganya tayari msikubali tena kupoteza Wananchama kwa makosa madogo madogo kama haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…